Usaliti hauishii tu katika kujihusihsa kimapenzi na mtu mwingine hata kufanya mambo ambayo mwenza wako akiyagundua moja kwa moja atajihisi kuwa anaswalitiwa ni usaliti. Ni jambo la kawaida siku hizi kukuta mtu mwenye mpenzi anachat katika mitandao ya kijamii na mtu wa jinsia tofauti. Hapa sizungumzii kuchat kwa kusalimiana bali kuchat kimapenzi.
Kusalimiana kimapenzi, kuongea kimahaba na kuchombezana na kufanya mambo ambayo kiuhalisia walipaswa kufanya na wapenzi wao. Inawezekana unachat na mtu ambaye yuko mbali labda unamdanganya tu ili akutumie pesa na huna mpango wa kuonana naye au hata haiwezekani kuonana naye, lakini kama unamfanya mhusika kuhisi nyinyi ni wapenzi basi unamsaliti mwenza wako.
Lakini chukulia mfano kwa namna yoyote ile mpenzi wako akaziona zile meseji je atakuelewa ukimuambia huyu ni rafiki tu? Au je atakuelewa ukimuambia nilikuwa namtania tu? Tuseme achana na mpenzi wako, vaa viatu vyake na kujiuliza je nikimuona mwenza wangu anachat namna hii na mtu mwingine nitamchukuliaje?
Usiruhusu mambo ya kijinga namna hiyo kukuharibia mahusiano yako. Hii ni hasa kwa wanawake, mwanaume kakusalimia kaanza kukutongoza cha kujilegeza eti umchune kwanza kuwa mstaarabu kumuambia kuwa nina mtu na kwa heri, akama nasumbua sana mblock tu au usijibu sms zake. Lakini kumjibu kuacht naye kimahaba hata kama unatania jua unasaliti kwani mwenzi wako akikufumania hatali kama unatania au la na kumbuka uaminifu ukishapote ahaurudi tena.
Kuna watu wengi wamaharibu mahusiano yao kwakuwa tu walikuwa wanataniana huko katika mitandao ya kijamii, watu wameharibu ndoa zao kwa mitego tu ya kijinga katika mitandao ya kijamii. Mtu anayejiheshimu huweka mipaka katika matumizi ya mitandao ya kijamii na kama rafiki yako katika mitandoa ya kijamii akiivuka hiyo mipaka basi unamuambia kwaheri.