Tuesday, November 14, 2017

Mbinu Za Kuchepuka Bila Kukamatwa, Zipo Hapa !

Baada ya taarifa kuenea mitandaoni kuwa mkuu wa kanisa letu anatuhumiwa kubeba mrembo wa watu, nimeona kuna emergency ya kuandika juu ya hii mada. Lengo langu sio ku promote uchepukaji, but no, my position is, mtu anapochepuka humkosea Mwenyezi Mungu, lakini pia humkosea mwenzi wake. Unapomkosea Mwenyezi Mungu ni rahisi kusamehewa ukiomba msamaha, na Mungu anaweza akakupa ka adhabu mambo yakaisha.

Kimbembe mpenzi wako akikudaka, sio rahisi sana kurejesha mahusiano mema na mpenzi wako, that is why am here to 'prevent a major catastrophes' btn you and your partner from happening:

Rule No 1 ya kuchepuka bila kudakwa

Usinogewe na penzi la mchepuko! Mwizi huwa hadakwi siku ya kwanza. Wengi wanaochepuka huwa wananogewa na kujisahau mpaka wanaanza kupiga piga simu na kutuma text hovyo. Mara hujiachia na kujisahau kuwa wanachofanya kinatakiwa kiwe siri. Ukiona umeshaanza kunogewa na penzi la mchepuko, au yeye keshaanza konogewa na wewe, piga chini, ni bora utafute mchepuko mwingine na uanze nao mwanzo...

Rule No 2 ya kuchepuka bila kudakwa
Msifanyie mambo yenu 'machoni pa watu'
Kama mnavyojua kuwa penzi ni kikohozi, basi usikohoe mahali ambapo watu wanajua sauti yako. Kama unachepuka ni bora ukachepukie mbali kabisa na maeneo ambayo umezoeleka. Hii itapunguza kuenea kwa info juu ya uchepukaji wenu.

Rule No 3 ya kuchepuka bila kudakwa
Kumbuka, hakuna siri ya watu watatu. Usimhadithie mtu YEYOTE juu ya uhusiano wako na mchepuko. Mkiweza kuifanya hii ikawa siri yenu wawili, itawasaidia kuliongezea uhai penzi lenu la siri. Pale unapo mwambia rafiki yako, naye atamwambia mwingine na mwingine na mwishowe siri itavuja sehemu isiyotakiwa kufika, so from there mtawekewa mitego na kuanza kufuatiliwa kwa siri.

Rule No 4, ya kuchepuka bila kudakwa
Simu ni adui wa penzi mchepuko
Watu wengi wanaochepuka hudakwa sana kwa njia ya simu. Kuwa muwazi kwa mchepuko wako kuwa upo kwenye serious relationship/ ndoa na so ajicontrol hasa kupiga piga simu na kutuma vi text. Kama vip ni bora utafute kisimu special kwa ajili ya mchepuko wako. Kisajili kwa jina la mtu asiye na uhusiano wowote kabisa na wewe. Then uwe unakitumia kuwasiliana na mchepuko wako. Ili mambo yakibuma, inakuwa ni rahisi kwako kukikana hicho kisimu. Unaweza ukasingizia kuwa labda kuna mtu alikisahau kwenye gari wakati umewapa mafundi lifti kwenda site n.k

Rule No 5 ya kuchepuka bila kudakwa
Dont leave any phyisical evidence.
Jaribu kupoteza ushahidi wowote wa yale yatakayotokea kwenye crime scene! Juzi hapa kuna mdau alileta kisa chake kuwa alichepuka na shem wake alafu shem akasahau bikini master bed room, so wife alivyokuja akaikuta na ikawa msala.
So kama ukiwa na mchepuko, hakikisha hakuna ushahidi utakao watia hatiani pasi na kuacha shaka. Huu ni uzembe mkubwa sana ambao unawafanya watu wadakwe kirahisi.

Hitimisho:
Nadhani ukifuata kanuni hizo hapo juu itakuwa ni msingi mzuri wa kutunza penzi/ ndoa yako kwa mda mrefu zaidi. Mwisho naomba nikuache na agalizo kutoka Mithali 14:12 Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, Lakini mwisho wake ni njia za mauti.