Tuesday, November 14, 2017

KWA WANAWAKE, FAHAMU DALILI 10 ZA MWANAUME ANAYEKUPENDA KWA DHATI......

Bila shaka hujambo msomaji wangu, leo ngoja tuone ni dalili zipi mwanaume huwa nazo kwa mwanamke ampendaye kwa dhati. Kuna dalili kumi za mwanaume anayakupenada kama ifuatavyo hapa chini.......
ANAVYOTAZAMA
Mwanasaikolojia Zick Rubin kutoka Chuo cha Havard nchini Marekani aliwahi kusema kwamba watu wanaopendana hutumia asilimia 75 kutazamana kuliko wasiopendana, ambao kiwango chao ni asilimia 30-50.
Hii ina maana kwamba mwanaume anapotumia muda wake mwingi kumtazama msichana na kugeuka taratibu kuangalia vitu vingine kama mtu asiyependa kuacha kumwangalia, ujue anampenda.
MIPANGO
Mwanaume anayekupenda atakushirikisha kwenye mipango yake hasa ya muda mrefu. Mfano akitaka kununua kiwanja, kujenga nyumba atakuambia na pengine kutaka mchango wako wa hali na mali katika kulifanikisha hilo. Ukiona mwanaume anakuficha mambo yake, tambua kuwa huyo ana walakini kwenye penzi la dhati na la muda mrefu.
ATAONESHA HUZUNI
Katika maisha ya mapenzi kuna wakati wa kuhuzunika. Mwanaume mwenye upendo wa dhati atashirikiana nawe wakati wa huzuni na kuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa unapata furaha maana wewe ndiye uliye furaha yake maishani mwake.

ATAKUAMINI
Dalili nyingine ya kupendwa na mwanaume ni kuaminiwa kwenye maisha kwa ujumla. Yaani mwanaume anayekupenda hatakuficha kitu, mfano pesa zake, atakupa uhuru kwenye simu yake na kukuamini katika usimamizi wa miradi yake na hata kukupa kila aina ya nafasi ujaribu kusimama wewe kama wewe mfano atakuwezesha biashara, kazi ilimradi usibaki kuwa tegemezi na mara nyingi huwa na moyo wa kusamehe sana pale unapo mkosea maana anajua hutorudia kwa sababu anakwamini
.
ATAKUPA NAFASI
Ninapozungumzia nafasi nina maana atakukaribisha kwake bila hofu na kukupa nafasi ya kuingia na kutoka bila mipaka, atakupa nafasi ya kuweka vitu vyako kwenye kabati na kuruhusu nguo, picha na vitu vyako kuonekana wakati wote chumbani kwake pasipo na haofu kwa maana hiyo uko peke yako.

UTAKUWA MWANAFAMILIA
Mwanaume aliyefikia chaguo la mwisho kwa mwanamke humshirikisha mpenzi wake kwenye masuala yake ya kifamilia, mfano atamwalika kwenye vikao vya harusi, kipaimara, atatoa nafasi ya kuambatana naye kuona wagonjwa, kusalimia ndugu na atakuwa huru kukutambulisha kwao na kwa marafiki zake wote alionao.

ATAZUNGUMZA NAWE KUHUSU WATOTO
Kwa kuwa wanaume wengi hufikiria kuwa na familia, mwanaume anayekupenda atazungumza nawe mipango ya kupata watoto kwa kuwa atakuwa amekuchagua wewe kuwa mama wa wanaye na atapenda mazungumzo hayo.

ATAKUSAIDIA
Kwa kuwa kukwama ni sehemu ya maisha yetu, mwanaume anayekupenda atakuwa tayari kukusaidia unapokwama. Kila mara atahakikisha kuwa unakuwa na mafanikio na yeye atakuwa tayari kukupunguzia usumbufu wa maisha, kwa kukufuata kazini, kukusaidia baadhi ya mambo na hata ya nyumbani.

ATAJITOLEA
Ninaposema kujitolea ninamaanisha atakuwa tayari kufanya mambo yako na kuyaweka yake nyuma. Kwa mfano akiwa anapenda mpira na siku hiyo kuna mechi, lakini muda huo ukamwambia akufuate kwa mjomba wako atakuwa tayari kuacha furaha yake na kukujali wewe. Huyu ni mwanaume anayekupenda kwa dhati.

ATAAMBATANA NAWE
Wapenzi wengi wasiokuwa na mapenzi ya dhati huona aibu kuambatana na wapenzi wao kwenye mikusanyiko ya watu, lakini mwanaume anayekupenda atafurahia kutoka moyoni kuongozana nawe kwenye halaiki ya watu na kufurahia uwepo wako bila kuona aibu.
Mada hii inaishia hapa, hebu jiulize mwanadada, huyo uliyenaye anakufanyia haya, kama sivyo kwa kiwango kikubwa utakuwa na kazi ya kuhakiki penzi lako na pengine kujenga misingi mipya ya uhusiano wenu kabla haujavunjika.
Pole na samahani kwa yeyote aliyeguswa na mada hii
.