Thursday, November 9, 2017

Inawezekana Haukuwa Changuo Lake La Kwanza Lakini Wewe Ndiyo Chaguo Lake La Sasa

Katika mapenzi mara nyingi watu tunaowapenda hua hawatupendi hivyo tunalazimika kuwa na chaguo la pili au la tatu. Kwa watu wengi unapojua kuwa mwenza wako kakuoa au kakubali umuoe kwasababu ya kukosana na mpenzi wake wa awali au kwasababu ilishindikana kumpata yule anayempenda inakuondolea kujiamini.
Hii inatokea sana kwa wanawake unajua mwanaume alikuwa akimpenda mtu flani, ukahangaikaweee mpaka akakuoa au hata hukuhangaika lakini baada ya kuachwa tena kwa kuumizwa ndiyo akaja kwako. Hapo wanawake wengi huanza kutokujiamini na mara kadhaa kuanza kujilinganisha na yule wa chaguo la kwanza.
Katika mapenzi unapaswa kufahamu kitu kimoja kwamba kama kakuoa basi wewe ndiyo chagu lake na hakuna cha chaguo la kwanzaau la pili. Hapa nikimaanisha kuwa kama hakumuoa huyo ambaye anajifanya kumpenda au anampenda kweli inamaana kuna sababu ambayo ilifanya iwe hivyo na kuna sababu ambayo imefanya wewe uoe au kuolewa.
Kwa maana hiyo basi wewe umemzidi hiyo sababu, labda ni dini, labda ni kabila, labda ni ndugu, labda ni tabia, labda ni hakuwa akipendwa tu vyakutosha lakini wewe ushaolewa au umeoa hivyo acha kujiona kuwa hustahili. Usingekuwa hustahili hiyo ndoa wala asingekuona na kukutamani.
Acha kuishi katika kivuli cha yule mtu kuwa ukimuona roho inadunda labda watarudiana au labda yeye ana kitu ambacho wewe huna,jua wewe una ambacho yeye hana na ni huyo mwenza wako hivyo asikuumize kichwa. Kama huyo mwenza wako anajifanya nayeye kutomsahau X wake kila siku kumzungumzia muambie ukweli kuwa alimshindwa kipindi hicho ndiyo sasa atamuweza.
Muambie atulie na kuendelea na maisha kwani alishashindwa kumpata na kila saa asikukumbushe kumbushe kuwa ulikuwa chaguo la pili. Asikufanye ujisikie vibaya eti kwakua alikua anampenda mtu mwingine kabla muambie hata wewe kabla yake ulikua unapenda mtu mwingine hivyo asikuumize kichwa kwa kushindwa kwake kumpata aliyekuwa anamtaka.