Wednesday, November 1, 2017

ACHA KUTESEKA KWA AJIRI YA MAPENZI



Ni mara nyingi sana utasikia vijana wanalia na kuteseka kwaajiri ya mapenzi kisa kikubwa kikiwa ni usariti...usariti katika mapenzi imekuwa aina fulani hivi ya maisha ya kisasa mbaya zaidi mtu anaweza akampenda fulani wakahaidiana mengi lakini mwisho wa siku anaachwa bila kuagwa, utalia, utanung'unika na kukonda lakini ukweli utabaki pale pale kuwa umeachwa na kamwe huwezi kuibadili hiyo hali iwe ndoto...

kijana mwenzangu ukiachwa jiulize ulipokosea pengine wewe ndio chanzo, kaa chini tafakari mapungufu yako yote naamini utagundua tu makosa uliyokuwa unayafanya kwa kurudia rudia...

ila siku hizi kutokana na utandawazi usariti mwingi chanzo ni simu, wengi huwa awapendi sana wawapo na wapendwa wao kisha hao wapendwa wao wakawa wapo makini sana na simu zao huku wakijisahau kuna mtu pembeni anaye hitaji faraja ya moyo, inauma sana umetoka na mpendwa wako ila yeye hana muda na wewe zaidi ya kukodolea macho yake kwenye simu yake.

WENGI WANAJITAKIA

Mapenzi si tendo la Ndoa tu peke yake na kamwe usimuone mtu anakupenda tu eti kwakuwa anakupa penzi kila unapohitaji kuna wengine ni mabingwa wa kuigiza anaweza akakupa penzi kwakuwa kuna vitu vingi anahitaji kutoka kwako. wewe unazama mzima mzima miguu hadi kuchwa unajisahau mwisho wa siku unaachwa unaanza kulia kuwa umetendwa lakini ulisahau kumchunguza kuwa huyo alikuwa mtu sahihi kwako?

mtu anayekupenda kwa dhati ni yule atakaye kujari na kukuthamini lakini ukiona mpenzi wako anakuwekea mipaka kwenye baadhi ya vitu vyake, ukiona mpenzi wako ukiwa naye kama ajiamini na wengi utakuta hawezi kukuachia simu yake kabisa {shituka ndugu yangu huna chako hako}

HAKIKISHA UNAMPATA MWENYE SIFA UZIPENDAZO

unajua kila mtu huwa anapenda mpenzi wake awe na sifa au muonekano fulani, kuna wengine wanapenda wanene, wembamba, wafupi, warefu, weupe au weusi. wapo wenzangu na mimi wanapenda wapate wapenzi wanaojiweza kimali. lakini wengine wamejiwekea kuwa akiwa mrefu, mwembamba awe amesoma ata asipo kuwa na fedha huyo ananifaa.

ni vigumu kunielewa hapo lakini namaanisha kuwa hakikisha unapata mpenzi ambaye anazo sifa zisizopungua nne unazozihitaji, lakini ukipata mpenzi ambaye hana sifa ata moja unayoipenda huyo huto dumu naye kwani utakuwa umeudhurumu moyo na katika maisha hakuna kitu kibaya kama kuudhurumu moyo siku zote moyo uliodhurumiwa huwa na sifa ya kutokuridhika. kila utakachopewa kamwe akiwezi kukukata kiu yako. ila ukikutana na yule mwenye sifa unazozitaka ukampenda akakuelewa ata akikupa maji ya kunywa ya moto utayanywa na kiu itakatika.

kikubwa ni kuhakikisha unapata kile unacho taka.


UKIPENDWA PENDEKA

akuna kitu kigumu siku hizi kumpata anayekupenda kwa dhati, wengi walioishia kuumizwa ni wale ambao walishindwa kudhihirisha upendo wao kwa wapenzi wao. kuna vitu vizarauliwa lakini zawadi ndogo ya pipi inaweza kumfanya mtu akakupenda adi akajiona kuwa duniani mpo wewe na yeye tu. zawadi ni kitu muhimu sana usipuuze.

>>>epuka malumbano

>>>jifunze kutumia lugha nzuri

>>>kuwa mkarimu

>>>acha utani na marafiki wa jinsia tofauti na yako

>>>epuka kutumia simu/laptop uwapo na mpenzi wako

>>>kubari kushindwa

>>>wapende ndugu wa mpenzi wako

yapo mengi sana lakini naamini ukiyafuata hayo machache hutoumizwa kwenye mapenzi