Kujielewa, Kujipenda, Kujithamini, Kujiamini na Kujikubali. Ukiwa na hizo 5K ni moja ya hatua kubwa ya mafanikio katika kujenga a Strong Personality na utu nafsi wenye ‘Utashi’. Huna haja ya kutambuliwa iwe kwa kutajwa ama kusifiwa bila kujali kama ni sifa mbaya ama nzuri ili kujiona kuwa nawe u mtu kati ya watu. Huna haja ya kila likuhusulo liwe kwa misingi ya kusifiwa, sadikiwa, chelekewa, chekwa na mengine mengi – ili tu kutambua ufanyalo ni msingi na la haja. Huna haja ya kumuegemea mwanadamu mwenzio kwa lolote like lililo kwa misingi ya kukubalika bali tu kwa kujikubali.
Muhimu kuliko yoote, huna haja ya kutafuta Furaha na Amani toka kwa wengine bali utapata hayo ndani yako mweneywe daima!