Ktk makala moja iliyopita nilielezea swala la kujiswafi ili kuondoa utoko nakupunguza harufu/shombo ya uke, vilevile nilisema kuwa kwa kufanya hivyo (kujisafisha huko chini) kunapunguza siku zako za hedhi ikiwa utaendelea kujiswafi wakati uko hedhini.
Sote tunatambua karaha ya hii kitu na baadhi hutunyima raha ikiwa wapenzi wetu hawezi kumudu kufanya ngono wakati uko huko mwezini japokuwa wewe unataka kuliko siku zote.
Sasa ni hivi; kuna uwezekano mkubwa kabisa kuwa siku zako ni kati ya 3-7 lakini wewe unakwenda siku 8-12 na huelewi kwanini wewe wakati wengine wanapiga siku tatu tu?
Unapokuwa hedhini damu huchirizika taratibu lakini si damu yote inayotoka nje ya ikulu na kujaa kwenye "Tampax" au "pads", sasa ili damu hiyo yote itoke yenyewe inamaana itakubidi uisubiri kutegemeana na uwingi wake.
Hivyo, ili kupukuza swala la kusubiri isaidie kwa kidole chako cha kati kuitoa huko iliko kama ambavyo nilielezea awali kwenye swala la kutoa utoko. Endelea kujiswafi mpaka uone maji yanachuruzika bila damu.....kwenye hedhi utahisi uterezi usihofu au kutafuta jitihada za kuumaliza, haumaliziki kwani wakati huo uke unakuwa laini ili kusaidia mabonge ya damu kupenya kwa urahisi (natambua sio wote lakini Mungu ndio alivyoumba hivyo).
Mara baada ya kujiswafi vaa kifaa chako kama kawaida na endelea na shughuli zako, kumbuka kujiswafi kila unapokwenda kuoga na hakika utajikuta unakwenda siku chache zaidi kuliko ilivyo awali.
Pssssss!Awali dada mmoja alikuwa akwenda siku sita (alikuwa bikira so huruhusiwi kujisafisha) lakini tangu alipoingia kwenye ulimwengu wa ulimwengu (mahusiano yakimapenzi) akaanza kujiswafi anapiga siku 3 tu na damu sio nyingi sana kama ilivyokuwa awali.....
Nakutamia siku njema na kila la kheri katika kupunguza siku zako za damu