Monday, October 30, 2017

KAMA UMESHINDWA KABISA KUTOA KITAMBI NA KUPUNGUA UZITO KABISA SULUHISHO HILI HAPA...

  
Huenda wewe msomaji umeshakata tama kabisa ya kupungua uzito baada ya kutumia njia mbalimbali bila mafanikio, lakini naomba nikupe matumaini kwamba swala la kupunguza uzito na kutoa kitambi linawezekana kabisa na sio gumu kama watu wanavyofikiria. Leo ntaenda kutoa elimu muhimu sana ambayo ukiifuata kwa makini utapungua uzito. Pamoja na kua daktari,  miaka ya nyuma nilikua mnene sana hivyo naongea mambo ambayo nimeyapitia.
Kiukweli unene unatesa sana kimwili na kisaikolojia, yaani uchovu mara kwa mara, jamii inakuona tofauti sana na huenda hata kupata mpenzi ikawa ngumu kidogo, kukosa baadhi ya kazi na kushindwa hata kuvaa baadhi ya nguo kwa ajili ya unene lakini hebu tuyaache hayo tuongelee maada kuu.
Formula ya unene ni ndogo sana, ukila sana kuliko shughuli au mazoezi unayofanya unaongezeka uzito, ukila kidogo na kufanya mazoezi sana unapungua uzito, kiasi unachokula kikilingana na shughuli na mazoezi unayofanya unabaki kwenye uzito ule ule. Lakini kupunguza uzito inatakiwa mtu ubadilishe MFUMO  wako wa maisha kabisa kama ifuatavyo.
Kuhusu ulaji wa chakula;
Epuka vyakula vya kukaanga sana na wanga; vyakula vinavyonenepesha ni vyakula vya wanga na mafuta kama ugali, wali,mihogo,viazi,chapati,maandazi na ngano zote,nyama ya mafuta kabisa,chips na kadhalika..vyakula hivi vinatakiwa viliwe sana na watu wanaofanya kazi ngumu kama wanaolima, kupasua mbao, kubeba mizigo na zingine ngumu kama kazi zako ni kushinda umekaa unatakiwa ule kidogo sana aina hii ya vyakula.yaani badala ya kula ugali mkubwa au wali mwingi na mboga kidogo unatakiwa ule ugali mdogo au wali kidogo na mboga nyingi kama maharage,mchicha,njegere,samaki,nyama ya kuku kwani mboga hizo hazinenepeshi.
Kunywa maji mengi; hakikisha unakunywa maji mengi kama nusu lita au lita moja nusu saa kabla na nusu saa baada ya kula, hii itakufanya ujaze tumbo maji ujisikie kushiba na ule kidogo pia maji mengi yanasaidia mwili kuchoma mafuta  vizuri na kuondoa sumu mwilini.
Ratiba ya kula: mwili unatakiwa upate chakula kingi asubuhi, chakula cha kawaida mchana, na chakula kidogo sana jioni lakini kwa bahati mbaya hii ni tofauti kwa jamii yetu kwani kifungua kinywa hua ni kidogo, cha mchana kingi kidogo afu usiku ndio kingi zaidi, usipoacha ratiba hii ya kula, unene hautakuisha, kwani mwili unachoma mafuta mengi asubuhi na mchana.... wakati chakula cha usiku kikiwa kingi mwili hukibadilisha chakula hicho kua mafuta na kuhifadhi tumboni na kutoa kitambi.
Kula milo midogo midogo: utafiti umeonyesha ile milo mikubwa inayojaza tumbo ndio imafanya watu wanenepe sana na milo midogo midogo hata mara nne kwa siku inaongeza kasi ya mwili kuchoma mafuta, hivyo epuka kula mpaka kulijaza tumbo kabisa, kula kawaida ukina umeshiba acha sio lazima chakula kiishe.
Kula ukiwa una njaa tu;epuka kula kwasababu eti muda umefika, kula ukiwa na njaa tu na ukiona njaa imekubana usiku kula vyakula ambavyo hata ukila ndoo nzima huwezi kunenepa mfano karoti mbichi, matunda, mboga za majani, juice ya kujitengenezea  ambayo haijaongezwa sukari na kadhalika.
Epuka kushindaa njaa; watu wengi hushinda njaa wakidhani eti watapungua uzito , unaposhinda njaa mwili unadhani uko kwenye shida ya chakula hivyo ukila baadae mwili  unahifadhi mafuta mengi zaidi kwa matumizi ya baadae na watu wengi wanaoshinda njaa hula chakula kingi jioni na kuleta shida niliyotaja hapo juu na hata hivyo huwezi kushinda njaa maisha yote hivyo kinachotakiwa ni kupata mfumo mpya wa maisha ili uuzoee.
Epuka kula kwenye sahani moja na watu wengine; ukila na watu huwezi kujua kiasi gani hua unakula hivyo ni rahisi sana kula chakula kingi bila kujua, hivyo pakua kwenye sahani yako ndogo{achana na sahani kubwa itakufanya upakue kingi] halafu kula peke yako.
Kula taratibu;  mishipa ya fahamu inachukua muda wa dakika 20 kutambua kama umeshiba baada ya kula,  hivyo ukila ndani ya dakika tano ukamaliza kula, utajikuta hujashiba kwasababu mishipa ya fahamu haijatoa taarifa kwenye ubongo lakini ukila kwa dakika ishirini taratibu chakula kilekile unachokula kila siku unaweza ukajikuta unakibakiza. Kula taratibu inaweza kua changamoto kidogo hivyo hakikisha unajipa kila siku muda wa kutosha wa kula yaani usile ukiwa na haraka unawahi sehemu. Lakini pia kama umezoea kula haraka utapata shida kula taratibu hivyo jaribu kufanya mambo mengine wakati unakula kama kutumia simu, kuangalia TV au kuongea na mtu huku ukiangalia saa yako.
Funga kula baadhi ya vyakula; simaanishi kushinda njaa hapana, unaweza ukawa unazitoa siku mbili au moja kwa wiki. Siku hizi kula matunda tu na mboga za majani na maji bila kula chakula kingine chochote, hii huumpa muda mwili wa kujisafisha sumu zote na kupungua uzito kirahisi zaidi.
Epuka vyakula vyenye sukari sana; acha kula biskuti,soda,keki,pipi,jojo, chai yenye sukari nyingi  na mengine mengi ambayo hayana msaada kwenye mwili kwani sukari ni moja ya chanzo kikuu cha unene mwilini na vyakula hivyo havina msaada mwilini zaidi ya kuongeza sumu.
Punguza unywaji wa pombe; pombe hasa bia ina ngano nyingi ambayo huongeza uzito hivyo ni vizuri kunywa kidogo kutumia aina zingine za pombe kama wine au whisky.
Punguza ulaji wa chumvi; weka chumvi kidogo sana kwenye chakula chako kwani chumvi huzuia maji yasitoke ndani ya mwili{kumbuka 60% ya binadamu ni maji tu].
Kua na msimamo: wewe ndio unajua unataka nini kwenye mwili wako, usiburuzwe kwenye vikao vya kula sana kwenye sherehe au kitu chochote na kama umeshakula sema umekula.
Piga mswaki baada ya kula mlo; hii sio tu itatunza meno yako lakini pia itakufanya usipate hamu ya kula zaidi na mara kawaida ukishapiga mswaki hautakiwi kula tena, mbinu hii itakusaidia sana.
Pima uzito kila wiki; kama hujui maendeleo yako na hujui unataka ufikishe kilo ngapi bila mzani basi unapoteza muda, kua na mzani kutakufanya upate moyo wa kuendelea na mfumo wako wa maisha lakini hata ukipima mwisho wa wiki na kugundua hujapungua usife moyo endelea tu.
Kuhusu mazoezi; sheria za afya zinasema kama mtu  anakula chakula mazoezi ni lazima, japokua mtu anaweza kupungua kwa chakula tu, mazoezi huweza kusaidia sana kupungua uzito.kufanya mazoezi hasa kwetu afrika ni kama adhabu kwa watu wengi lakini mazoezi ni muhimu sana. Kama kazini unaenda kwa mguu, baiskeli  au kazi zako ni za nguvu sana hii inaweza kua zoezi  tosha. Kulingana na hali ya maisha ya sasa kubana sana, kukosa muda wa kwenda gym au kushindwa kukimbia barabarani sababu ya pikipiki nyingi napendekeza utumie zoezi la kuruka kamba. Fanya hili zoezi nusu saa tu kwa siku ndani ya siku sita za wiki au ruka mara mia mbili tu kwa siku inatosha sana. Shida ya mazoezi sio kuanza bali kuendelea, wengi wenu mtaanza kwa fujo afu mtaacha. Fanya mazoezi kama sehemu ya maisha yako, ukifanya kidogo kila siku ni bora sana kuliko kufanya sana kwa msimu. 
virutubisho vya kupunguza uzito; kuna virutubisho vingi sana vya kupunguza uzito siku hizi... ambavyo nimevitumia kwa wagonjwa wangu na vikafanya kazi  ni mchnganyiko unaitwa clean9, mchanganyiko huu hupunguza hamu ya kula, kuongeza kasi ya kuchoma mafuta na kuondoa sumu mwilini ambazo zinafanya watu wasipungue kwa diet ya kawaida. hutumika kwa siku tisa tu na huweza kupunguza kilo tano mpaka tisa lakini baada ya hapo kama hujaridhika na upungufu huo kuna FIT1 na FIT2 ambayo inatumika kwa siku 30 na kupungua zaidi.kitu cha msingi ni kwamba ukishapungua badilisha mfumo wa maisha kwani ukirudi kulekule kwenye kula bila utaratibu baada ya dozi hizi utanenepa tena. na virutubisho hivi mara nyingi huendana na mazoezi kidogo.
                                           
Usikate tamaa; katika mafanikio yoyote ya binadamu sio unene tu hata mafanikio ya kifedha yanahitaji uvumilivu wa hali ya juu.. wanaokata tama ndio hao kila siku hawafanikiwi, kama umeamua kufanya kitu, usifanye nusunusu fanya kwa akili yako yote na utafanikiwa. Hayo mambo niliyotaja hapo mwanzoni kuhusu chakula na mazoezi  yataonekana magumu mwanzoni lakini baaada ya muda mwili utazoea na wewe ndio utapata kilevi au addiction mwisho itakua ndio maisha yako mapya na vitambi utavisikia redioni. 
mwisho; unaweza kutumia njia ya chakula tu kupunguza uzito lakini njia ya mchangayiko wa chakula na mazoezi ni nzuri zaidi lakini pia ukifanikiwa kupata hivyo virutbisho ukatumia pia ni nzuri..nakutakia maisha mapya...