Saturday, October 28, 2017

HIKI NDIO CHANZO NA MATIBABU YA HARUFU MBAYA SEHEMU ZA SIRI KWA WANAWAKE.

                                                  
watu wengi hua wanafikiri kwamba uke wa mwanamke hauna harufu kabisa kitu ambacho sio kweli, sehemu yeyote ya mwili iliyojificha hua ina harufu fulani, mfano kwapa, chini ya matiti, katikati ya makalio na kadhalika lakini harufu hiyo hua ya kawaida lakini huweza kua kali kama kuna magonjwa fulani...
hivyo uke wa mwanamke pia una harufu fulani ambayo kitaalamu ni ya kawaida lakini kuna vitu fulani ambavyo huweza kusababisha ile harufu kua kali sana kiasi kwamba hata mtu akipita karibu yake atasikia harufu hiyo. watoto wa kike ambao wanavunja ungo kwa mara ya kwanza hasa shule za msingi wanakua hawajui usafi wa sehemu zao za siri hivyo kutoa harufu mbaya.
wanawake wengi waliolewa na wakishazaa wanajisahau sana na kua bize na mambo mengi ya uleaji wa mtoto na kujiacha wakitoa harufu ya mwili kwa kisingizio cha kua bize na mtoto huku wa kisahau hiyo ni sumu ya ndoa kwani haki ya mume haiondolewi na mtoto. vifuatavyo ni vyanzo vikuu vya harufu sehemu za siri...

magonjwa ya zinaa; magonjwa mbalimbali ya zinaa huleta harufu kali kulingana na aina ya ugonjwa mfano ugonjwa wa gono ambao hutoa uchafu wa njano, ugonjwa wa fangasi ambao hutoa uchafu mweupe, na ugonjwa wa trichomoniasis amabo mgonjwa hutoa uchafu wa rangi ya kijani wenye harufu kali sana.magonjwa yote haya huambukizwa kwa ngono zembe.

jasho la mwili; tabia ya baadhi ya wasichana kuto kuoga kila siku hasa sehemu zenye baridi kali hufanya bakteria kubadilisha maji maji yote ya mwili na jasho kua harufu kali sana.watu wanene sana hutokwa na harufu kali zaidi sababu ya kutokwa jasho jingi na kulihifadhi mwilini.

mabadiliko ya homoni za uzazi;kipindi cha hedhi na kipindi ambapo yai linashuka mwanamke hua na harufu ambayo sio ya kawaida lakini pia kipindi cha uzee yaani zaidi ya miaka 50 homoni za uzazi hupungua sana kiasi kwamba ulinzi wa sehemu za siri kutokana na asidi ya mwili hupungua sana na kusababisha harufu.watu hawa wakipewa oestrogen cream harufu huobdoka.

vyakula unavyotumia;  baadhi ya vyakula huweza kubadilisha harufu ya jasho maji maji yanayotoka sehemu za siri. mfano baadhi ya pombe za kienyeji, vitunguu, pilipili na samaki huchangia mabadiliko ya harufu za sehemu za mwili na sehemu siri hivyo kama wewe una tatizo hilo ni vizuri kuepuka yakula hivyo.

kusafisha uke na sabuni; kawaida uke wa mwanamke unatakiwa usafishwe kwa ndani kwa kutumia maji tu. sasa matumizi ya sabuni na mafuta au kemikali fulani kusafisha huua bakteria fulania ambao kazi yao ni kuzuia maambukizi kutokwa kwa wadudu wengine ambao sio wazuri kwa mwili.

uchafu wa mwili; tabia za kurudia nguo za ndani ni hatari kwani huleta mkusanyiko wa bakteria wengi ambao huweza kua hatari kwa uke wa mwanamke hivyo kwa hali ya kawaida mwanamke anatakiwa avae angalau chupi moja kila siku bila kuirudia kabla ya kuifua.

mwisho;matibabu ya hali hii hutegemea sana chanzo husika cha harufu mfano kama ni ugonjwa wa zinaa utapewa matibabu hospitalini kulinganan na ugonjwa husika.
kupunguza uzito na kuvaa nguo ambazo hazibani sana ni muhimu kwani husaidia kupunguza jasho jingi linalobaki mwilini.
kumbuka harufu mbaya ni hatari kwa jamii na mahusiano yako kwani unaweza ukaachwa na mpenzi wako kama huzingatii hili au ukamfanya hata kutoka nje ya ndoa kama umeolewa.