Tuesday, October 17, 2017

Hakuna Mwanamke Ambaye Hapendi Vitu Vizuri, Atakuvumilia Kama Anaamini Huna…

\
Mwanaume usijidanganye kuwa “Mimi mke wangu hapendi vitu vizuri” hakuna kitu kama hicho, kila mwanamke hupenda vitu vizuri na wanawake wengi hujali zaidi muonekano wao kuliko  kitu kingine chochote. Hii ndiyo maana hata kule kijijini ambapo binti mdogo hana uwezo wa kununua viatu lakini ndala zake au yeboyebo ataziosha vizuri ili kupendeza kuliko mtoto wa kiume ambaye hata kuoga inakuwa shida.

Mwanamke anajifanya hapendi vitu vizuri kwakuwa anajua uwezo wako na anakupenda. Mwanamke anayekupenda akiona huwezi kumnunulia kitu flani atajifanya kutokukipenda ili tu asikukwaze, lakini hamiaanishi kuwa hakipendi kitu husika. Kwasababu hiyo basi kama mwanaume unapaswa kufahamu kuwa, kulingana na uwezo wako hakikisha unamdekeza mwenza wako, kwani atakuvumilia tu pale anapojua kuwa huna uwezo.

Niwanawake wachache sana ambao watajua kuwa una uwezo mkubwa wa kuwanunulia vitu vizuri halafu ukajifanya mbahili au ukasema hawapendi vitu vizuri halafu wakakuvumilia. Atavumilia tu pale anapojua kuwa huna, kama unacho na humdekezi atatafuta mtu wa kumdekeza na hapa naomba nifafanue kidogo, “Atatafuta mtu wa kumdekeza..” kwa maana kwamba kwa mwanamke inakuwa na maana zaidi kama akifanyiwa kitu cha kimapenzi na mwanaume.
Mwanamke mwenye uweo zakununua nguo ya laki mbili hataipenda ile nguo kama atakavyopenda nguo ya elfu hamsini aliyonunuliwa na mpenzi wake. Hivyo usione tu kwakuwa anafanyakazi basi ukajisahau ukasema atanunua mwenyewe pesa anazo. Hapo nisawa na kumuambia ajidekeze kitu ambacho hakina maana kwake, mdekeze wewe hata kama ni kwa kidogo kiasi gani ulichonacho. Mpe vitu vya kusimulia kwa mashoga zake na yeye aweze kusema “Hii kaninunulia baba flani…” ajihisi naye ana mwanaume.