Wanaume wanao-cheat wake zao wana sababu nyingine ya kuhofu zaidi ya wasiwasi wa kubambwa na wake zao. Utafiti umeonyesha wana uwezekano mkubwa zaidi ya kufa kifo cha ghafla kwa ugonjwa wa moyo (heart atack) wakati wakifanya ngono ya usaliti (cheating sex).
Ugunduzi huo umetoka katika ripoti iliyochapishwa na American Heart Association, wakati wakifanya uchunguzi kuona kama ni salama kwa wagonjwa waliopata matatizo ya moyo kuanza ngono baada ya matibabu.
Utafiti umegundua wagonjwa wnaweza kuanza ngono wiki moja baada ya heart attack, al muradi wanaweza kupanda ngazi kadhaa bila tatizo au kujisikia vibaya.
Tahadhari kwa waume: ngono nje ya ndoa yako (cheating) inaongeza shinikizo zaidi kwenye moyo wako kuliko kawaida
Moja ya vitu vilivyogundulika wakati wa utafiti huo viliwashangaza watu. Iligundulika kuwa hatari ya kukumbwa na kifo cha ghafla wakati wa ngono inaongezeka wakati wa ngono ya usaliti kwa wanaume waliooa na kusaliti wake zao.
Hii ni kwa sababu ni mara nyingi na wanawake wanaume hao wana-cheat na wanawake vijana zaidi katika mazingira wasioyazoea au yasiyo ya kawaida ili kuepuka kubambwa, kitu ambacho kinaongeza stress.
wanasayansi, wakiongozwa na Profesa Glenn Levine, kutoka Baylor College of Medicine ya Houston Texas, alisema autopsy(upimaji wa chanzo cha kifo kwa maiti) zimeonyesha kuwa katika vifo vya ghafla vilivyotokea wakati wa ngono, asilimia 93 ya vifo hivyo vilitokea wakati ya ngono ya usaliti.
Ripoti hiyo imeshauri madaktari walazimike kuzungumzia ngono na hatari zake kwa wagonjwa wa moyo sababu imeonyesha ni wagonjwa wachache sana wanaoelewa athari hizo.