Friday, October 5, 2018

JE..! UNAJUA NAMNA YA KUMPATA MCHUMBA MZURI ANAYEKUFAA POPOTE PALE?

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhnTp2NStRn27yLqkV8K-gon89X4XbfFR11nAJzne2n7wmUYd5hJVakbZtg5cb-WG4mDWNE8vAaGk14yub1LOSt8UASP8_MHx3Zxi7kca6FrcVRKc15ex3FJRnwbV16h3rqdsYsgNtKpQg/s640/beautiful-couple.jpgMoja ya HUZUNI kuu maishani ni pale mwanaume au mwanamke anapoingia katika ndoa na matumaini makubwa pamoja na matarajio makubwa sana, pale tu matarajio hayo na matumaini hayo yanapoharibika baada ya miezi au miaka michache. Na hii hutokana tu majuto mazito ayapatayo mwanandoa kutokana na kazi kubwa ambayo huyu mwanaume mtanashati au mwanamke mzuri aliifanya awali nayo ni katika kummchagua mwenzi wake wa maisha ambaye alidhania kuwa ni dhahabu kumbe ni chuma cha kutu tena kilichoharibika. Huu uharibifu unapotokea haubakii tu kwa wazazi bali huathiri  hata kizazi kijacho. Je umewahi kujiuliza kuwa kwanini haya yanatokea?  Kitabu hiki kimebaini sababu zinazopelekea haya kutokea na kutoa njia za kuelekea mafanikio ya mahusiano yaliyo na furaha hasa tukijikita katika njia sahii na madhubuti za kutafuta mchumba.
NJIA SAHIHI ZA KUTAFUTA MCHUMBA
Uchumba ni mahusiano mazuri yanayoendeshwa baina ya vijana wawili wa jinsia tofauti yaani mwanamke na mwanaume kwa malengo ya kuwa na familia kati ya kijana wa kiume na kijana wa kike. Na sababu ya mahusiano  mazuri ya uchumba ni kuingia katika ushirikiano makini kwa njia ya ndoa, kwa kuongezea mahusiano haya ya uchumba yanalenga hasa katika kuwa na mtu ambaye anafaa na mtu muhimu katika mahusiano ya ndoa. Pia washauri mbambali  wanahusia kuwa mahusiano  haya ya uchumba yanawaruhusu hawa wapendanao kumjua mwenzake kinagaubaga bila kuwa na mgandamizo wa kingono, mihemko au hisia za mwili. Kumtafuta mchumba ama mwenzi anaekufaa mwenye tabia kama zako si uchaguzi unaohusisha kumchagua mtu ambaye atakusaidia kuishi katika kipindi cha upweke. Hii humanisha kuwa mwenzi ama mchumba utakae mchagua anapaswa kuwa ni yule ambae katika ukuaji wenu miaka  thelathini, hamsini na sitini ya uzeeni bado utaendelea kumpenda. Kumchagua mwenzi ama mchumba wa maisha umakini wa hali ya juu wa  kijana awe yeyote   unatakiwa mno, kujikabidhi kikwelikweli katika biashara ya muhimu, na inahitaji wingi wa fikra makini, utambuzi wa majukumu, zikiambatana na uwazi. Jambo la kuzingatia wewe kijana ambaye unamsaka mtu muhimu katika maisha yako (mwenzi wako) ni kuwa usiingie kwenye hii hatua ya  uchumba mpaka jambo hili limedhihirika. Najua kwa namna moja ama nyingine unaweza usinielewe ninalolimanisha, sasa basi haya ndio mambo yatayokupelekea mpaka kufikia uamuzi wa kuingia katika mahusiano  ya uchumba na hata kuamua kutafuta mchumba unaye mtaka. Jambo mojawapo la kuelewa hapa ni kwamba elewa  kwa kina umuhimu wa maamuzi mazito unayo enda kuyafanya kwa kuzingatia swala lenyewe la ndoa, na kifungo ambacho unaenda kukianzisha kupitia mahusiano ya uchumba mda mchache kabla ya kuamua kuingia katika uchumba. Ungana nami kupitia kitabu hiki kujifunza njia madhubuti za kusaka umpendae mahali popote pale pale unapokua umefikia uamuzi huu makini wa kumsaka yule unaemtaka kumkabidhi moyo wako kwa njia ya upendo wa kweli.
MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA UNAPOCHAGUA MCHUMBA.
Hapa chini nimekunyambulia mambo muhimu sana yakuzingatia wakati unataka kumchagua yule unyemdhania kuwa ni mchumba wako kama ifuatayo,
     1.  AINISHA SIFA UNAZOHITAJI KUTOKA KWA MTU UNAYEMTAKA.
Ingawa inaweza kuwa vigumu sana kumjua aliye kamili na bora kwako hata ufunge macho na wakati mwingine maneno kukuisha, hivyo basi unaweza kufikiria sifa unazozitaka sana kutoka kwa mtu unayemtarajia awe nazo. Sifa ni za muhimu sana kwako kwasababu zinakusaidia kumpata yule unaye mtaka, na hapa kuna mambo ya kufikiria unapoainisha sifa wa yule anayekufaa:
              aDINI. Kama wewe ni muyahudi kwa hakika utahitaji kuoa mtu aliye sawa na dini yako, japokuwa unaweza kumbadilisha lakini marachache watu wamefanikiwa kwa hili ila uwezekano wa kurudi katika dini ya awali kwa yule aliyebadilishwa  ni mkubwa.
             b.  MAADILI YA KIFAMILIA.
Je umedhamiria kuwa na watoto ama? Na kama ndivyo je ni watoto   wangapi? Ama si nia yenu kuwa na watoto katika hali yoyote? Ingawa mnawezakubadili mawazo yenu lakini pia hili ni jambo la kuangalia wakati unamtafuta mchumba wa kuoa ambaye mtashauriana na kushirikiana mawazo (Ingawa  hutakiwi kuliongelea hili mara tu unapokutana nae).
                     c. UTU WAKO.
Ingawa si rahisi kutabiri utu wa mtu lakini kuna mambo machache ambayo ni muhimu kuyaangalia. Je  mtu utakaemchagua  ua furaha na uchangamfu wako au anayeshirirki pendo lako kama kichekesho tu? Weka hili akilini unapomtafuta mchumba anaekufaa.
d. MTAZAMO KUHUSU UHUSIANO.
Je mtu utakae kuwa naye je ni mtu ambaye ni tegemezi kimawazo? Ama ni mtu ambaye anaweza kusimama peke yake kimawazo? Pale anapokuwa yeye kama yeye? Hili ni jambo la msingi sana kulizingatia.
             e.UHUSIANO NA JAMII.
Je mtu unayetaka kuwa naye ni mcheshi? Je anashirikiana na jamii inayomzunguka? Vipi kuhusu jamii anayoishi nayo inamtafsiri kama msaada kwa jamii ama kero kwa jamii. Je marafiki alionao  ni wa aina gani? Upo  msemo unosema kuwa nionyeshe marafiki zako nikwambie tabia yako Je anapenda kuwa na marafiki wa matawi ya juu tu au wa aina zote? Hili pia ni muhimu sana  kulizingatia.
           f. NIA ZENU.
Mara nyingine mtu uliyempenda mnaweza msiwe na nia moja kwa pamoja, au kuwa na matakwa ya pamoja, unatakiwa kuwa na mambo machache ambayo yanaendana kwa pamoja na yule umpendaye ambayo wote mnapendezwa nayo kwa pamoja ambayo yatafanya mahusiano yenu kuendelea vizuri. Kama wewe tabia yako ni kupenda kusoma vitabu  na umpendaye hapendi hiyo tabia utakosa vitu vya kuzungumza nae.
         2.            USIRIDHIKE
Watu wengi sana  wameridhika sana kwasababu wamewapata watu amabao wanawafanya wao kutokujisikia upweke na kuwa wamependwa hata kama si kwa njia iliyo sahihi. Sababu nyingine ambayo inawafanya watu waridhike ni kwamba wamekuwa na mahusiano labda kwa miaka mitano na kugundua kuwa wanaweza siku moja wakawa ni mke na mume hivo basi kwasababu hii ya kukaa muda mrefu katika mahusiano wengi wameichukua hatua mojawapo. Lakini msisitizo ni huu kuwa tafuta  mtu ambaye unamtaka lakini si kwasababu watu wanataka umuoe au kwasababu wanampenda, ama kwasababu familia inataka uwe nae, au kwasababu unaona aibu kusema kwaheri kwa rafiki wa awali uliyekuwa nae na kujiuliza maswali atanifikiriaje mimi hali ukizingatia tumekuwa nae katika urafiki kwa muda mrefu! Lakini ipo kauli moja kuwa tafuta mtu unayempenda.
         3.   KUWA TAYARI KUKUBALIANA NA BAADHI YA MAMBO
Ijapokuwa umetengeneza orodha ya vitu uvipendavyo na vile usivyovipenda haijalishi ni sehemu gani, itakusaidia sana ambavyo vitakufanya uwe nafuraha, ukweli ni kwamba hautapata mtu ambaye ni mkamilifu asilimia mia, lakini mtu sahihi kwako ni yule anaekufanya kuwa ni mwenyefuraha muda mwingi, na mtu huyo anakidhi pia mahitaji ambayo kwa namna fulani hukujua kama unayo. Usikatae kumchagua mtu eti  kwasababu hakidhi vigezo vyako vyote hasa katika kukidhi mahitaji yako yote, kwasababu hayupo. Lakini usikae na mtu  ambaye unadhania kuwa hakidhi vigezo ama sifa za msingi kwako, ingawa unapaswa kuwa ni mtu usiye na msimamo mkali, lakini jambo la kuzingatia  ni kuwa usikae na mtu ambaye unaamini hatakutimizia kile  ambacho unategemea kukipata mwishoni. Pia weka uwiano katika kumtafuta mtu ambaye  atakufanya wewe kuwa ni mwenye furaha bila ya kutoa baadhi ya vitu amabvyo ni vya thamani kwako kwake.
       4. TAFUTA MTU UNAE ENDANA NAE KITABIA.
Kuendana kitabia ni jambo la muhimu sana na ni jambo linaloimarisha sana uhusiano, hivyo basi unapomtafuta yule wa pekee kwako anatakiwa kuwa ni yule ambaye mtashirikiana nae katika mambo yako unayoyapenda. Hii itakupa uwezo wa kujua mambo anayoyapendelea yeye pia na hata katika kupanga mipango kwa pamoja kwa  urahisi zaidi.
     5.       SHIRIKIANA NA  MARAFIKI
Mahusiano ya kichumba maranyingi yamekuwa yakitokana na marafiki wawili wa jinsi ya tofauti. Ingawa inaweza kuonekana kuwa si kawaida, unaweza kuishia kumuoa rafiki wa binamu yako. Hivyo yakupasa kuwa mkweli kwa marafiki zako, ambao wanakujua kikwelikweli jisi ulivyo na mtu unayetaka kuwa nae. Au waweza kukutana na moja ya marafiki zako ambaye waweza kumwambia juu ya mtu ambaye umevutiwa naeusiwe na aibu au uoga kwa yule  anaekufanya wewe kuwa na furaha duniani nao wakati mwingine wanaweza kuhusika kukusaidia hata namna ya kumpata unayemtaka badala ya wewe kuhusika sana lakini pia itakuwa ni njia mojawapo wewe kupata taarifa ambazo kwa namna moja ama nyingine isingekuwa rahisi kuzipata.
6. AINISHA SIFA AMBAZO HUPENDI UMPENDAYE AWENAZO.
Sifa ambazo hupendi yule umpendaye awe nazo ni muhimu sana kuwa miongoni mwa sifa unazozizingatia wakati unapochagua mchumba wa kuwa nae maishani. Unapoanza kuangaza huku na kule, yule ambaye utamkabidhi moyo wako ni vizuri kuzingatia vitu ambavyo vitaimarisha uhusiano wenu kuwa imara bila kukatishwa kwa namna iwayo yote. Na hapa yapo mambo ya kuzingatia-:
a.      UKOSEFU WA MVUTO
Mvuto wa nje unaweza kukua siku hata siku  lakini hautathiminiki. Ingawaje mtu anaweza kukidhi vigezo kadhaa unavyovitaka lakini kumbuka kuwa huwezi kujilazimisha  mwenyewe kuwa na mvuto kwa mtu mwingine.
b.      KUKOSA MWAFAKA.
Kukosa mwafaka juu ya jambo fulani linalowahusu. Mtu asiye kuwa na siri, mtu mwenye vurugu na asiyekuwa na subira katika mambo fulani fulani na pia  asiyeuzuia mdomo wake katika kuropokaropoka, hilo ni tatizo kubwa,yakupasa kuwa mwangalifu. Lakini huwezi kujua kwasababu unaweza usikubali vitu fulani fulani, lakini kama lipo jambo ambalo linakufafanua kuwa wewe ni nani ambalo mwenzi wako mtarajiwa halitmbui, pia utakuwa na tatizo katika siku zijazo.
c.       UTOFAUTI KIMAZINGIRA.
Unaweza kumpata umpendaye wa maisha yako yote, lakini anaishi sehemu ambayo hata kwa hali yoyote hutaweza kufika kwa mfano wewe uko Tanzania na yeye yuko Uingereza huwezi fika kirahisi , haitakusaidia kwa namna yoyote bali utapoteza muda bure.
Katika kumtafuta yule umpendaye kijana yeyote unayetamani kuwa na mwenzi unayemtaka unapaswa kuwa mwangalifu sana maana hapa ndipo watu wengi hupoteza dira kwasababu walichagua chuma cha kutu badala ya dhahabu yaani yule waliyemdhania kuwa ndiye anafaa kumbe sivyo kamawalivodhani.  Hivyo basi hiki kipengele kinahitaji umakini wa hali ya juu. Hitimisho la mahusiano ya kiuchumba linaweza kuwa chungu, na hivyo basi kupelekea kutafuta msaada kwa wazazi, washauri na marafiki kwa usaidizi na hii ni kwasababu ya kukosa umakini katika swala hili kama kutokufuata njia sahihi wakati wa kumtafuta yule umpendaye. Hivyo uangalifu mkubwa unatakiwa ili kuzuia kuingia katika shimo hili kubwa lenye maumivu makali yasiyokuwa na dawa ya kutuliza maumivu hayo. Ni imani yangu ni  kuwa  kupitia nja tulizoziona hapo juu zikizingatiwa kwa umakini na  kama zilivyo kwa hakika zitakusaidia kumpata yule umpendaye kwa dhati popote pale ulipo.