Saturday, September 8, 2018

Mapenzi Sio Kujifungia Chumbani tu na Kufanya Tendo

Mapenzi ni ubunifu, unaweza ukaona kitu kidogo lakini kitu hiko ukikifanya kwa mlango wa mapenzi kinakuwa kikubwa na hakiwezi kusahaulika kirahisi kwa mwenza wako. ukizungumzia mapenzi watu weusi wengi tunajua mapenzi ni kujifungia chumbani na kutiana tu, hapa ndo wazungu wanapotupiga bonge la gepu pale wakiwakamata dada zetu.

Basi ili kufanya mapenzi yako yaonekane mapya kila siku si lazima kila siku mjifungie chumbani kufanya staili mpya au sio lazima kila siku mtoke kwenda kula dina sehemu nzuri.

Unaweza ukamchukua mpenzi wako ukaenda nae sehemu ilio tulivu kisha mkaanza kusoma vitabu(hii inategemea na nyie wawili mnapendelea vitabu vya aina gani ila sio vya kemia au physics

Inapendeza sana mkiwa mmekaa pamoja mkisoma vitabu, mkabadilishana mawazo kwa kile kilichoandikwa kwenye kitabu. inaweza mkaenda beach(tulivu) au sehem ambayo unahisi mtakaa mtatulia bila usumbufu, mkasoma vitabu vyenu taratiiibu.