Monday, July 9, 2018

Utafiti wangu: 'Massage Parlour' ni Z'aidi ya Maduka ya Ngono

Wakuu niliamua kwa mara nyingine kujipa kazi ya kufanya "Utafiti" katika maeneo ya "Massage Parlour" katika jiji la Dsm na vitongoji vyake.Raha ya utafiti wa aina hii ni kujivika "uhusika" haswaa ili upate mambo ya ndani ya kujifunza hasa undani wa jambo lenyewe,ama hakika nimejifunza mengi na kwa kweli hii ndio Dsm,mambo ni motomoto ndani ya kuta nne za vyumba.

Nilianza kwa kutembelea "Massage Parlour" za mitaa ya Sinza(Sitataja majina kwa sababu maalumu).Humu nimejionea mambo mengi sana na mazito,ama hakika mji huu una mambo.Hizi si Massage Parlour tena bali ni maduka ya ngono yasiyo rasmi yenye leseni ya "Massage Centres"

Nilianza mitaa fulani ya Sinza ambapo pale nilikuta Massage yenye bei mbili tofauti,moja ya Tsh 25,000/= na nyingine ni 35,000/=,yaani hiyo ya elfu 25 haina choo na bafu la ndani kwa ndani wakati hiyo ya elfu35 maanake unapata chumba chenye choo ndani,huna haja ya kutoka kwenye korido kwenda kuoga au msalani.Ndani ya chumba unakutana na huduma kadha wa kadha,kwanza unaambiwa unataka huduma ya aina gani?Maana kuna

1)Soft Massage
2)Hard Massage
3)Medium Massage
4)Body to body Massage
5)Honey Massage nk

Huduma hizi zote zinapatikana humo ndani,yaani kama hiyo ya body to body maanake mtoa huduma anatoa kila kitu halafu anakupaka mafuta na kuanza kuusugua mwili wako akiwa mtupu,hiyo hard ni kwa wale wenye kutaka kunyoosha misuli,medium inakuwa kati ya soft na hard na wakati soft hiyo ni hatari sana maana inaamsha mambo yote ya dunia ya mwili.

Kifupi wakati wa kuingia unakuta wadada wamekaa kama sebuleni,na ukiingia pale wanaitana wooote na wanapanga foleni,hairuhusiwi kukubaliana na mmoja wakati wenzake hawapo pale sebuleni/mapokezi.Wakikusanyika wote unaambiwa uchaguwe wa kwenda kukuhudumia.Sasa ukiwa kauzu unapitia mmoja baada ya mwingine then unachaguwa.Yaani wakati wa kuchaguwa kila mtu analegeza macho na madoido ili achaguliwe yeye,inakuwa kama "ng'ombe mnadani".

Baada ya hapo ni kwenda kupata huduma,huko ndani kwenye huduma ni balaa tupu,yaani ukitoka salama ni bahati,yaani ni kama bahati ya UKAWA kuanzisha maandamano mbele ya Central Polisi bila kibali cha maandamano halafu wakaachwa.Kiukweli hii ni aina ya biashara ambayo wale wadada wasioweza kujipanga foleni pale Sinza Ambiance basi wanakuwa huku,na pia kwa wale wasioweza kuopoa pale wanahamia huku.Nimejifunza kuwa biashara hii ni ngumu sana kupambana nayo moja kwa moja sbb binadamu wana mbinu nyingi sana.

Katika utafiti wangu nikagundua wateja wengi ni waume za watu ambao pengine wake zao hwafanyi au hawajui namna ya kufanya hizi massage.Wahudumu wengi wanakiri kuhudumia waume za watu hasa siku za weekend na mida ya jioni baada ya kazi,kwani watu wengi hawapendi kuingia mchana huku wakionekana.Na huduma hizi zinazotafutiana kutokana na mazingira na mazingira.Huko Mikocheni,Mbezi na Masaki bei zake ni kubwa sana.Wachina na Wafilipino wengi wanafanya baishara hii na ile "extra" kwa mgongo wa Massage Parlour.

Kuna centres nyingine wapo kikazi haswaa,hii ni kwa sababu kuna watu wenye matatizo ya neuros(?),migongo na wameshauriwa na madaktari wanatumia sehemu hizi kwa ajili ya matibabu ya migongo na viuno.Hiivyo si wote wapo kwa ajili ya ile "biashara".

Mashoga wengi hushinda na hawa wadada,na hukaa humu na kufanya kazi hiyo,pia wavutaji wa shisha na madawa pia humu ndio centres zao.Mtu anaingia anajidunga anasinzia mpaka anaamka ndio anatoka.Kifupi kila unapozuia hili binadamu anavumbua hili,kila kitu kina majibu yake.Humu ndani ya Masage Parlour ni hatari wakuu...Kuingia bure kutoka lazima uwe umakauka.

Hii ni sehemu ya kwanza ya muendelezo wa utafiti wangu ndani ya hizi Massage Centres...Nipatapo wasaa nitakuja tena hapa kumalizia.

Muwe na siku Njema Wakuu