Tuesday, July 3, 2018

Jinsi Ya Kujizuia Kutofanya Mapenzi Katika Mahusiano Mapya

Kuingia katika mahusiano mapya ya kimapenzi huwa ni furaha na kuchanganya pia. Unaingiwa na hisia ambazo hujawahi kuwa nazo na pia kupenda kwa dhati. Mpenzi wako anakufurahisha na wewe pia unamfurahusha. Lakini inaweza kutokezea sitofahamu wakati ambapo wewe hutaki ama hujiskii kufanya mapenzi lakini yeye akawa na hamu ya kufanya tendo hilo. Sababu zozote zile uko nazo, una haki ya kujizuia kutofanya tendo la ngono mpaka ile siku ambayo utajiskia kuwa umefikia siku yako. Mwili ni wako na maamuzi ni yako.

So utafanyaje umzuie mpenzi wako kutofanya ngono na wewe?

Mambo ya kufanya kumzui mpenzi wako kutofanya mapenzi nawe

1. Usilale kwake
Iwapo hautaki kufanya mapenzi na mpenzi wako, basi ni vizuri usijiingize katika hali ambazo zitachangia nyinyi wawili kuingiwa na hamu ya mapenzi. Iwapo umetoka deti na mpenzi wako, usijaribu kumsindikiza hadi kwake ama kuenda njia moja. Pia hutakiwi kuwa unazunguka sehemu ambazo mpenzi wako anaishi wakati kama huo kwa sababu inaweza kuchangia pakubwa kuingiwa na tamaa. 
2. Usiwe mlevi
Kuna baadhi ya watu wanafikiria ya kuwa matumizi ya vinywaji ukiwa na mpenzi wako inapunguza hisia za kufanya mapenzi. Well, labda inaweza kuwa ni kweli lakini kulingana na utafiti ni kuwa mtu mlevi anapoteza mwelekeo wa kufanya maamuzi yafaayo. Hivyo ukiwa umeathirika na ulevi pamoja na mpenzi wako, kuna asilimia kubwa ya kufanya maamuzi ambayo si sawa.

3. Toa visababu ambavyo havitomkwanza mpenzi wako
Unaweza kutoa visababu kama vile unaumwa na kichwa, hujiskii vizuri nk. Ingawa kutumia uongo kwa mpenzi wako si jambo zuri, ni muhimu sana iwapo itakuja kwa maswala ya kufanya mapenzi ama kama hujiskii kufanya mambo mengine ambayo yanahusiana na wewe. Hivyo ni muhimu kupatia mambo mengine kipao mbele.

4. Fungua roho yako
Hii ndio njia nzuri zaidi kujizuia kutofanya mapenzi. Kukaa na mpenzi wako katika kikao na kumueleza ndani na nje kuhusiana na wewe kujizuia kutofanya mapenzi ni jambo nzuri zaidi kwa nyote wawili. Kumueleza ukweli mpenzi wako kutatoa ile nafasi ya kwako kuonekana kama unayapenda mahusiano yenu na hauhitaji kuficha ama kudanganya katika mahusiano yenu.
Iwapo atakubali basi itadhahirisha ya kuwa yeye anatilia maanani mahusiano yenu. Kama atakataa basi bila shaka mahusiano yenu hayatokuwa marefu.