Mwanaume anayezama katika penzi huanza kuonesha sifa na tabia maalumu.
Kwa kawaida, wanaume na wanawake huonesha na kuelezea hisia zao kwa namna inayotofautiana kabisa, hivyo, wakati mwingine ni vigumu hasa kujua hisia za mumeo. Kila mwanaume ana njia yake ya kuonesha mahabba yake, lakini hizi ni ishara ndogo za jumla ambazo hutoa mwelekeo unaoonesha wakati ambao wanaume wanakuwa wamezama kwenye penzi.
1. HUWA MAKINI
Mwanaume anayependa humakinika unapokuwa karibu naye. Je, anakutazama machoni na kuzungumza nawe moja kwa moja hata kama kuna watu karibu yenu? Hata kama ukiwa mbele ya watu haachi kuelekeza umakini wake kwako.
2. HUKUFANYA KUWA KIPAUMBELE
Hakuna kitu muhimu sana kwa mwanaume analiyependa kama kuwa na mwanamke anayemfanya awe na shauku. Bila shaka atakuwa na kazi zake, atakuwa na marafiki, atakuwa na mambo kayaya anayoyapenda, lakini umuhimu anauweka kwako, anaweka umuhimu wa kuwa pamoja nawe. Anapokuona, hujawa na furaha.
3. JUHUDI NA HARAKATI ZA KUKUVUTA
Mwanaume anayetaka kuuvuta moyo wa mwanamke hufanya juhudi za kumvutia. Anataka mwanamke anamuone kuwa yeye ni mtu maalumu, amuone kuwa ana upekee na umaalumu unaoweza kumvutia na kumvuta kwake.
4. HUKUCHEKESHA
Anapokuwa amekupenda, anataka umakinike. Miongoni mwa njia bora kabisa za kufanya hivyo ni kukuchokoza. Hukupa majina ya utani, hukufanyia utani…. Anafanya chochote ili kukufanya utabasamu. Ni njia yake ya kukuonesha kuwa ni mcheshi kwako.
5. HUKUSIFU
Mwanaume aliyezama kwenye upendo anaweza kuwa mchunguzaji sana; hii ni sehemu ya namna anavyotaka kuuvuta moyo wako. Hilo linaweza kuonekana kwa namna anavyokumwagia sifa. Huchambua muonekano wako na kuutambua urembo wako maridhawa.
6. HUTAFUTA NJIA YA KUTOA
Mwanaume anapokuwa kwenye kilele cha mapenzi, hutafuta vitu vidogo vidogo anavyoweza kukupatia ili kuonesha mapenzi kwako kama vile zawadi ndogo ndogo na kadhalika.
7. HUONA WIVU
Sio wanaume wote wenye wivu, na wivu uliopindukia sio mzuri, lakini mwanaume wako hapendi uugawe umakini wako kwa wanaume wengine, hapendi uwatazame wanaume wengine. Hilo linapotokea, huanza kukosa amani na kuhisi kitisho dhidi ya himaya ya moyo wake.
8. HUJIZUNGUMZIA
Wanaume hupata wakati mgumu kuzungumzia hisia zao. Kama anafunguka na kujizungumzia mbele yako, inaonesha kuwa anakuamini. Hii ni ishara kuwa uhusiano wako ni muhimu sana na hafanyi mzaha.
9. ANATAKA MARAFIKI ZAKE WAKUONE
Anaona fakhari kuwa na wewe. Kwa ajili hiyo, anataka dunia ikuone, ikiwa ni pamoja na marafiki zake na familia yake.
10. ANAKUJUMUISHA KWENYE MIPANGO YAKE YA BAADAYE
Bila shaka miongoni mwa ishara kubwa kabisa zinazoonesha kuwa mwanaume amezama kwenye mapenzi ni pale anapokujumuisha kwenye mipango yake ya baadaye. Hiyo inaonesha kuwa anataka kuwa nawe daima.
Shauku ina nafasi kubwa sana katika uhusiano….. ndiyo hatua ya kwanza kuelekea kwenye maisha ya pamoja. Kadiri muda unavyosonga mbele, shauku hiyo hubadilika na kuwa hisia pevu na iliyokomaa, ambayo ni upendo. Kujua namna ya kuweka mizania kati ya upendo na shauku ni jambo muhimu sana kwa uhusiano imara na wenye furaha.