Tuesday, July 3, 2018

INAKUHUSU MWANAUME!! UKIFANYIWA KITU MBAYA USILALAMIKE

Ulimuona binti ukampenda ama ukamtamani mie sijui, ukamfuata na kumtongoza lakin akakukataa kwa vile alikuwa hajui kama unampenda kweli, lakini kutokana na umahili wako wa ulaghai ukamdanganya weee mpaka akakubali.
Alipokubali tu ukataka umlale, lakini kwa vile alikuwa hajawahi kufanya Mapenzi (bikra) akagoma, ukaamua kutumia PHD yako ya ufuska ukafanikiwa kumvua chupi na kumaliza haja yako. wakati huo mtoto wa watu alikuwa na chuchu saa sita.
Haukuishia hapo ukataka tena na tena na tenaa, mpaka ukampatia mimba, lakini alipokueleza nina mimba yako naomba unioe. ukamjibu bado hujajipanga kuoa na ukamshauri mkaitoe, kwa kuwa binti aliwahi kusikia kuwa ukitoa mimba waweza kufa akagoma. hapo ndipo ukatumia ujuzi wako woote wa umalaya kumdanganya mpaka akakubali, makatoa mimba kwa bahati mbaya shuleni wakagundua akafukuzwa shule, wazazi wake wakahuzunika sana lakini wakashindwa wafanye nini.
Ulipoona wazazi wametulia, ukamfuata tena na kudai muendelee na Mapenzi kwa vile alikuwa anakupenda kweli, akakubali na Mapenzi yakaendelea. katika Mapenzi yenu sasa ukampachika mimba ya Pili mkatoa ya Tatu pia mkatoa na hatimaye mimba ya nne.
Binti akawa ameanza kuchoka, sura inakuwa ya kizee na maziwa yake yamelala kama sox za mgambo kwenye kamba, umbo lake la namba 8 halipo tena. wewe mambo yako yamekunyokeea sasa unataka kuoa mwanamke nwingine na kusema huyo demu wako siyo wife Material. UNAFIKRI HUYU BINTI ATAKUFANYAJE? TUBADILIKE WANAUME!