Sunday, May 6, 2018

KUOLEWA NI NDOTO KUU YA KILA MWANAMKE ALIYEKAMILIKA ILA KAMA UNA TABIA HIZI UTAZEEKEA NYUMBANI

*1. Tamaa ya utajiri*
fedha na mali nyingi pasipo kutambua kuwa vitu hutafutwa, hapa wengi hupoteza nyota zao kwa kukataa wengi wenye kipato cha kawaida na kujirahisisha kwa wenye nazo ambao kwa bahati mbaya wengi wao sio waoaji bali ni wahuni tu na watu wa anasa na kula bata mjin.

*2. Dharau,*
maringo, kiburi na mashauzi yaani we kila mtu akikusogelea na kujaribu kuzungumza na wewe unaanza kumpandisha na kumshusha kisha una msonya. Wengi huishia kukupotezea wakijua either umewadharau au tayari una mtu wako ndio maana nyodo nyingi.

*3. Husali*
hakika lazima wahuni watapata nafasi kwako na kukuchezea mpaka uchakae kama mtumba wa uvira. MWENYEZI MUNGU ndo anaetoa BARAKA ukimuomba hakika atakuepushia kuingia midomon mwa dubu na fisi wanaokuwa wakikuvizia na kuja kama MALAIKA. Atakupa ufahamu wa kuwatambua na kuwashtukia mapema.

*4. Kuvaa nguo za ajabu ajabu kama changudoa*
. Sijui ni nani aliyewaambia kuwa mkivaa hivyo mnapendeza! Unakuta binti unavaa kama mcheza show za Casino yaani ukipita nguo yaonyesha kila kitu ukiinama ndio balaa kabisa yaani kimin kinafunuka kila kitu nje nje kwa style hiyo nani atakupeleka kwao?

*5. Kujipaka marangi ya ajabu ajabu usoni kama mwali wa kibembe*
au kizaramo kwanza mnatutisha tu.

*6. Kupenda kujirahisisha au kujipendekeza pendekeza kwa wanaume,*
yani ukiguswa kidogo tu twende.

*7. Kuwa na picha karibia 500 Facebook,* Twitter nk halafu picha zenyewe hazieleweki yani zimepigwa katika mavazi au mapozi ya ajabu ajabu, mara umebinua makalio, mara tumbo, mara mdomo,

*8. Kila unachofanya basi unakimbilia kupost mfano kwenye Facebook* na kadhalika
nyinginezo hata ukienda haja basi lazima upost.

*9. Ni mtu wa maneno maneno*
yani we kila unachokiona unaongea na kuropoka ropoka tu hauna break! mwanamke gani?

*10. Huna mawazo ya malengo*
endelevu yani we kwenye kichwa chako kumejaa umbea tu sijui leo Wema Sepetu amefanya nini? Sijui Kim, Lupita amefanya vile na upuuzi mwingine.

*11 Mizinga.*
Yani siku ya pili tu baada ya kukutongoza unaanza " honey nataka galaxy" Htc" Huawei" mara baby nimeona nguo nzuri mara ooh baby yaani njaa inauma'' , utasindikiza harusi za wenzio hadi upigwe alama..

Waswahili husema, "Kama mzuri, Olewa"

Jihadhari na tabia hizi.
_Maneno makali ila ujumbe umefika.