Tuesday, April 24, 2018

ZIFAHAMU DAWA 5 ZINAZOTUMIKA KUWAACHISHA WATU SIGARA

moja ya vitu vigumu zaidi kuacha duniani ni sigara, ni watu wachache sana wenye juhudi kubwa hufanikiwa kuacha sigara kutokana na kiasi cha kemikali ya nicotine kilichoko ndani ya sigara ambacho kinamfanya mtumiaji apate kiu kali ya kutaka kuvuta sigara pale anapojaribu kuacha. ukiwa unaanza kuvuta sigara huwezi ukajua kua ipo siku utakuja kua mtumwa wa sigara lakini baada ya miaka kadhaa ndio utagundua kwamba umekua mtumwa na kuacha huwezi..
watafiti wamejitahidi kutafuta suluhisho la sigara na kugundua baadhi ya dawa , pamoja na kutumia dawa hizi mtumiaji lazima pia atumie njia kadhaa za kuacha ambazo sio za dawa kama kuamua moyoni kwamba ameamua kuacha, kukaa mbali na wavutaji sigara, kuanza mazoezi yeyote ya mwili ambayo kimsingi husaidia sana kuponya addiction, kula vizuri na kupumzika, kuepuka kutumia vilevi vyovyote ambavyo vitamrudisha huko na hata kuonana uso kwa uso na mshauri wa afya.
dawa zifuatazo zimesaidia baadhi ya watu kujikomboa na uvutaji wa sigara
bupropion; hii ni dawa ya mgandamizo wa mawazo ambayo pia hutumika kutibu watu wanaotaka kuacha sigara, hufanya kazi kwa kuondoa kiu kali ambayo huipata pale tu anapoacha sigara. mgonjwa hutumia dozi ya 100mg kutwa mara tatu huku akiendelea kuvuta sigara kisha wiki ya pili mgonjwa huacha sigara na kuendelea na dawa hizi angalau kwa muda wa wiki saba.
nicotine; hii ni kemikali inayopatikana ndani ya sigara ambayo inamfanya mtumiaji wa sigara ashindwe kuacha, hivyo wataalamu wameichukua kemikali hii na kuiweka kwenye jojo au big g ili mtumiaji aweze kuila kwa kutafuna jojo hizi kama mbadala wa sigara na baada ya muda fulani apunguze dozi ya jojo hizi mpaka pale atakapokua ameacha kabisa na mwili kuzoea kuisha bila nicotine. hutakiwi kutumia zaidi ya jojo 20 kwa ndani ya saa 24.
clonidine; hii ni dawa inayotumika kutibu presha ya kupanda lakini pia imethibitika kwamba inasaidia watu kuacha kuvuta sigara, matumizi yake ni kidonge kimoja kutwa mara mbili....unaweza kuanza kutumia dawa hii siku ya kuacha au siku tatu kabla ya kuacha na kuendelea nayo huku ukipunguza dozi kwa siku nne mpaka tano. hutakiwi kuacha dawa hii ghafla kwani huweza kupandisha presha ghafla.
varenicline; baadhi ya watafiti wanahisi dawa hii inafanya kazi kuliko dawa nyingi za kuacha sigara, hufanya kazi kwenye ubongo kwenye sehemu inayoitwa kitaalamu kama nicotine receptors kwa kumfanya mtumiaji asione raha kuvuta sigara lakini pia huondoa ile kiu mtumiajia anayoipata pale anapokosa kuvuta sigara. matumizi yake ni wiki mbili kabla ya kuacha sigara na kidonge kimoja humezwa na maji mengi baada ya kula. dawa hii huendelea kutumika mpaka wiki 12 na zaidi ili kumsaidia mtumiaje aache kabisa.
notriptyline; hii ni dawa inayotumika kutibu mgandamizo wa mawazo, ambayo pia husaidia kutuliza ile kiu mtu anayoipata anapokosa sigara. huanza kutumiaka siku 10 mpaka 28 kabla ya kuacha kuvuta sigara..dawa hii hupunguza uwezo wako wa kutumia mashine yeyote ya moto kwa kipindi hiko.. ni vizuri usitumie mashine yeyote ya moto au kuendesha gari.
mwisho; dawa hizi zina madhara madogo madogo na makubwa kama ilivyo kwa dawa zingine, ni vizuri kabla ya kuanza kuzitumia au kuzinunua uonane na daktari ili ujue kama wewe zinakufaa kwani kuna baadhi ya dawa hazifai wagonjwa fulani fulani kama wa moyo, kisukari au madonda ya tumbo. bahati mbaya hata kuzipata hapa nchini kwetu ni changamoto kidogo lakini kwa watanzania walioko nje wanaweza kuzipata hata watanzania wa ndani ya nchi wanaweza kuagiza nje kama wanaweza.