Kuwa na mwili wa mazoezi inachukua muda na unahitaji adabu ya hali ya juu kuupata, hii inamaanisha unatakiwa uyapende mazoezi na lazima uzingatie kile unachokula ili haya mazoezi unayoyapiga yakupe matokeo mazuri zaidi.
Sheria #1: Punguza kula vyakula vya sukari...
Tumeshasikia wote kuwa vyakula vya sukari ni adui wa mazoezi, ila tunachotaka kukwambia punguza utumiaji wa vyakula vyenye sukari na sio uviache kabisa maana sukari ni muhimu sana kwa maisha yetu, ubongo na mfumo wa fahamu unahitaji sukari ili ufanye kazi zake vizuri, kwa hio hakikisha unapunguza sio kuacha kabisa.
Sheria #2: Kula mafuta zaidi...
Ndio, umeisoma vizuri!, kula mafuta zaidi, mafuta hayakufanyi unenepe, ila ukiwa unakula kula sana ndo kunakufanya unenepe, ukila mafuta zaidi itakusaidia kupunguza hamu ya kutamani vyakula vyenye cabohydreti(sukari) mara baada ya kupunguza milo yenye sukari, Homoni zinaitajika sana mwilini, mafuta hutumika kutengeneza homoni na kuzipa usawa na kuufanya mwili ufanye kazi kwa usahihi, na hasa yanahusika sana kwenye homoni ya testosterone ambayo ni homoni ya kujenga na kuipa uimara misuri.
Sheria #3: Badilisha matunda kwa majani ya mboga mboga...
Matunda yana cabohydreti(Sukari) nyingi, ila pia yana virutubisho vingine ambavyo mwili unaviitaji, ambavyo pia vinapatikana kwenye majani ya mboga mboga, hii njia inakufanya upate virutubisha vyote ila unakuwa umepunguza ulaji wa sukari au vyakura vya cabohydreti.
Sheria #4: Achana na pombe...
Pombe inasababisha mafuta kutunzwa mwilini badala ya kutumiwa kuleta nguvu, kwa hio kama upo makini na kutaka kujenga mwili wako itakubidi uachane na pombe, mwili huacha kumeng'enya chakula kwa muda, mpaka ini itakapoitoa pombe nje. Pia pombe huumiza mwili kwa kuufanya upungukiwe na maji pamoja na kuishiwa nguvu, hushusha kiwango cha homoni ya testosterone ambayo hujenga misuli, kwahio iwapo siku ukinywa pombe, hakikisha unakunywa na soda zenye dayati.Comment