Thursday, April 19, 2018

MAMBO MATANO YA KUTISHA YANAYOTOKEA KWENYE UUME UNAVYOZIDI KUKUA KIUMRI.

              
umri wa binadamu unabadilisha kila kitu mwilini, mifumo yote ya mwili hupungua uwezo wa kufanya kazi pale mtu anapoanza kukaribia miaka hamsini, hii huwafanya watu wa umri kushindwa kujikubali na kupambana sana kurudi ujanani lakini sote tunajua uzee hauzuiliki, wakati ukifika lazima yakutokea yatokee..mfumo wa kuona, moyo, upumuaji, figo, mfumo wa chakula, ngozi na kadhalika vyote huishiwa nguvu.
uume wa mwanaume huanza kazi rasmi anavyofikisha miaka 14, hapo hufanya kazi kwa nguvu zote lakini miaka ya mbele baadae mabadiliko huanza kuonekana kama ifuatavyo.
kupungua ukubwa wa uume moja kwa moja; hali hii husababishwa na kubadilika kwa seli nene ambazo zinapatikana kwenye uume na kubadilishwa nyuzi nyuzi za nyama kitaalama kama collagen fibres ambazo ni nyembamba sana lakini hali hii huchangiwa pia na mafuta yanayoziba uume usipate damu ya kutosha, kupungua kiasi cha hormone ya mwanaume ya testosterone na hali hii hufanywa kua mbaya zaidi na uotaji wa kitambi ambao huficha uume ndani kabisa
kupinda kwa uume; shughuli za kushiriki ngono na mazoezi mbalimbali ambayo huumiza uume bila kujijua huleta makovu mengi ndani kwa ndani kwenye uume ambapo baadae uume ukishakua na makovu mengi hupinda kuelekea chini hata wakati ukiwa umesimama, yaani kama uume wako ujanani ulikua kama mshale sasa utakua kama upinde.
kuishiwa nguvu za kiume; tatizo hili linaathiri zaidi ya wanaume milioni 30 dunia nzima, katika hali ya ukuaji hali hii husababishwa na kupungua kwa kiasi cha damu ambacho kinaingia kwenye uume kila siku ukihitaji kuusimamisha sababu ya kuziba kwa mishipa ya damu na mafuta kama nilivyoeleza hapo juu, usitegemee nguvu zako za kiume ulizokua nazo ukiwa na miaka 18 utakuja kuzipata tena kwenye miaka 40.
saratani za sehemu hizo za siri; saratani mbalimbali kama saratani ya uume hasa kwa watu ambao hawajatailiwa, saratani ya korodani na saratani ya tezi dume. utafiti mpya unaonyesha kutoshiriki ngono kwa wanaume mara kwa mara kunaongeza nafasi ya kupata saratani ya tezi dume.baada ya miaka 30 ni vizuri kupima angalau mara moja kwa mwaka kuangalia kama kuna kansa imeanza.
kuchelewa kufika kileleni; mishipa ya fahamu ambayo inatoa taarifa kutoka kwenye uume kwenda kwenye ubongo huishiwa nguvu umri unavyozidi kwenda na hii humfanya muhanga kuchukua muda mrefu sana kufika kileleni swala ambalo linaweza kua baya au zuri kulingana na muhusika na hata akifika kileleni hutoa mbegu kidogo sana.
suluhisho; kuna mambo unaweza kufanya kuchelewesha au kupunguza kasi ya madhara haya ya ukuaji kwa kumeza vichochoe vya kutengeneza hormone ya testosterone mwilini mara kwa mara ambavyo huongeza nguvu za kiume,stamina, mbegu na kupunguza kasi yaa uume kua mwembamba, kufanya mazoezi na kula vizuri kuepusha kitambi na kushiriki mazoezi ya uume ambayo kwa watu wanaozidisha miaka 30 ni muhimu kua sehemu ya maisha yao ili kubaki na uume bora wenye afya