chipsi; hiki ni chakula kinacholiwa sana na watu duniani, kwani ni rahisi kuandaa na kukiuza na ukiwachunguza walaji wa chakula hichi hua wana vitambi sana au ni wanene..chips husababisha mazoea yaani addiction ambayo humfanya mlaji atamani kuzila kila siku na kunenepa zaidi kwani ukizila husikii kushiba na kula nyingi zaidi..
vinywaji vitamu; unywaji wa vinywaji vitamu sana kama soda na ice cream au kuweka sukari nyingi sana kwenye chai au juisi husababisha homoni ya insulini kutengenezwa nyingi sana, baada ya muda homoni hii inakua nyingi muda wote kwenye damu na kubadili sukari kua mafuta na kuiingiza ndani ya seli badala ya kuiacha itumike kwa kazi za kuupa nguvu mwili.
nyama; ulaji wa nyama nyingi hasa nyekundu yaani nyama za nguruwe, mbuzi na ngombe husababisha kuhifadhika kwa mafuta mengi sana mwilini na kuongezeka kwa lehemu au cholestrol ambayo ndio chanzo kikuu cha magonjwa ya moyo.kitaalamu mtu anatakiwa ale 70 gram ya nyama tu kwa siku sawa na finyango tatu tu ndogo lakini pia nyama hukaa masaa 20 kwenye mfumo wa chakula kabla ya kutolewa nje kama kinyesi.
viazi; viazi vitamu au viazi vya kawaida vinanenepesha sana bila kujali kwamba unavichemsha au unavikaanga kwani vina kiasi kikubwa sana cha nguvu au calories ambazo baadae hugeuka kua mafuta ndani ya mwili hivyo ulaji wake unatakiwa ue mdogo sana..
vyakula vya kukaangwa; vyakula vyote vya kukaangwa kama maandazi, vitumbua, chapati,sambusa, soseji, nyama na mikaango yote unayofahamu hua na mafuta mengi ambayo mafuta hayo huingia mwilini na kumfanya muhusika awe mnene sana.
juisi za viwandani na kuandaa nyumbani; hizi mara nyingi hua zina sukari nyingi sana ambazo kama nilivyoelezea hapo juu, sukari hii ni hatari sana na itakunenepesha tu. hakikisha unaandaa juice yako nyumbani na kuweka sukari kidogo na usinunue juice za viwandani au zinazouzwa vijiweni na mama ntilie kwani zina sukari nyingi sana.
mafuta ya kuganda; haya ni mafuta yanayoandaliwa na kua kama ya mgando...ulaji wa mafuta haya kwa mfumo wowote ule kama blue band, mayonise, kimbo au siagi hunenepesha na kuongeza kiasi cha lehemu au cholestrol mwilini, mafuta hayo yakiingia mwilini huganda kama yalivyokua nje kabla haujayala...ni vizuri kuyaepuka na kutumia mafuta ya maji kama alizeti, korie na kadhalika..
pipi, biskuti, keki na chocolate; hivi ni vyakula ambavyo vinaonekana vina umbo dogo sana lakini vina kiasi kikubwa cha sukari na nguvu[calories] kiasi kwamba ukila inabidi ufanye mazoezi makali sana kuondoa mafuta yanayoingizwa mwilini na vyakula hivi.
wali; wali unaopita kiwandani kurekebishwa na kuonekana mweupe zaidi, ni moja ya vyanzo vikuu vya unene na unaliwa sana dunia nzima na bei yake ni rahisi lakini hata huu wali wa kawaida tunaochukua mashambani unatakiwa uliwe kwa kiasi kidogo sana, angalau kikombe kimoja kidogo cha wali uliopikwa kwa mlo mmoja...ukila zaidi ya hapo kitambi na unene huwezi kukwepa.
tambi; ulaji wa tambi angalau mara moja au mbili kwa wiki hauna shida, tatizo linakuja pale mtu anapoamua kuzila kila siku..hapo unene hauwezi kukwepeka kwa mlaji huu kwani zenyewe zina wanga mwingi na pia huongezewa chumvi au sukari na kufanya vinenepeshe zaidi..
mwisho; vyakula vya wanga ni chanzo kikuu cha unene ulipindukia duniani na ni vyakula vikuu vinavyoliwa na watu...ni vizuri kujenga tabia za kutokula wanga kila siku yaani sio lazima kila siku ule wali, ugali au viazi na mboga...unaweza ukala mboga tu kama dagaa, samaki,bamia, mboga za majani,matunda siku nzima bila kula wanga kabisa.