Monday, March 19, 2018

WANAWAKE HUANGALIA NINI KWENYE FIRST DATE?



Sio wote, bali wengi wao huwa wanaangalia mambo haya siku ya kwanza kukutana (au mtoko)

1. Kwanza wanatazama tembea yako, kisela au kiheshima ili wajue kama una kazi au la.

2. Kama viatu vina vumbi moja kwa moja wanajua gari huna.

3. Kama pesa hutoi kwenye waleti hujazoea kuwa na pesa tena yawezekana hata laki moja hujawahi kushika (miliki).

4. Kama hunukii vizuri basi wanawake huwajui vizuri, na hujui romance, hata hug hujawahi kupewa.

6. Kama hutunzi nywele zako hata zake hutazigharamia.

7. Ukiongea naye muda mrefu na maswali mengi, hata kama hujamtongoza, basi anajua umempenda.

8. Usipomtazama usoni au machoni, yawezekana ni muongo au hujiamini na unamuogopa.

Je vitu gani vingine huwa wanaangalia?