Tuesday, March 20, 2018

Mapenzi matamu, hisia mwanzo, kati na mwisho!

\
Mpenzi msomaji wa XXLove, tunakutana Jumatatu nyingine kwa rehema za Mwenyezi Mungu. Wiki hii tutaangazia hisia za kimapenzi zinavyotakiwa kuoneshwa kwa wapenzi. Hisia hizo zinatakiwa ziwe mwanzo, kati na mwisho na si katikati tu wakati wa tendo husika kama wafanyavyo wengi. 
Mapenzi ni hisia. Hisia zilizojaa utamu ndani yake. Hisia zenye raha na mshawasha wa ajabu, ambao wahusika wanapaswa wawe nazo. Hisia hizi zinatakiwa zionekane kabla (mwanzo), wakati wa tendo lenyewe na hata baada ya tendo. Siyo kukurupuka kama ambavyo wengi wamekuwa wakifanya.
Kimsingi mwanamke anapaswa aoneshe hisia zake kwa mwenza wake kabla hata hawajaingia kwenye uwanja wa mechi. Kama mihemko na hisia zako ziko jichoni ndiyo ulirembue sasa hilo jicho, mtoto wa kike uoneshe utofauti wako na mwenza wako. Kama ni joto la mwili kuongezeka na uliache basi liongezeke. Kama ni pumzi nyingi kushuka, ziache zishuke. Kama ni kupumua kama umekoswakoswa na mkuki basi acha upumue.
Vivyo hivyo kwa mwanaume, mapenzi hayahitaji haraka wala papara. Utamu wa mapenzi ni maandalizi ya mwili, akili na mazingira.
Kama mtaruhusu miili yenu kuonesha hisia za mapenzi mlizonazo, hata kwa kumwangalia tu mwenza wako, unajikuta ukipata hisia kali sana ambazo zinakufanya usikie utamu wa kile kinachoenda kutokea.
Hisia ninazozungumza hapa ni zile zinazomtofautisha mwanamke na mwanaume. Hisia ambazo huonekana au hutokea wakati wapenzi wanapokuwa faragha.
Wanaume wengi wanaonekana kuwa na haraka sana wanapokuwa katika uwanja wa mahaba na wanashindwa kuwaandaa wenza wao na kutaka kufakamia tu tunda bila hata kuliosha au kulimenya kwanza pasipo kufahamu kuwa maandalizi ya awali ndiyo yatakayokusaidia mwanaume na mwanamke kuweza kufikishana kwenye kilele cha mafanikio.
Cha kufahamu msomaji ni kwamba hisia za baadhi ya wanawake ziko mbali sana tofauti na mwanaume hivyo ni wajibu wa mwanaume kuhakikisha anazifukunyua zilipo. Naye mwanamke ni wajibu wake kuhakikisha anajirembua kadiri awezavyo ili kumruhusu mfukunjuaji aweze kuzifukunyua hisia hizo.
Hisia za kati ni zile zinazotokea au kuonekana wakati wa tendo husika. Mwanamke anapaswa atimize anachopaswa kukifanya na hata mwanaume naye anapaswa afanye yale apasayo kufanya kwa mwenza wake.
Hisia za mwisho ni mara baada ya tendo lenyewe. Mwanamke au mwanaume anapaswa kuendelea kuonesha hisia kwa mwenza wake kuwa bado anampenda, anamthamini na bado anatamani muda ungekuwepo waendelee na ‘kindumbwendumbwe’ chao.