Tuesday, January 9, 2018

ZIJUE SIKU ZA HATARI NA SALAMA ZA MWANAMKE WAKATI WA MZUNGUKO WA HEDHI.



MZUNGUKO WA HEDHI.


Katika mizunguko yangu ya kutoa ushauri wa afya kwenye mahusiano
nimekutana na watu wengi ambao ninagundua ya kwamba hawajui kuhesabu
 siku zao za hedhi au hawajui mzunguko wao ni wa siku ngapi. 
Wanaume wengi ndio hawajui kabisa. Hivyo Health 
Point imeamua kuandika japo kidogo kuhusu uhesabuji wa siku za hedhi.

BAADHI YA SABABU ZINAZOPELEKEA WANAWAKE NA 
VIJANA WA LEO KUTOKUJUA KUHESABU SIKU ZAO ZA HEDHI.

1- Kupotea kwa elimu ya jando katika makabila yetu
2- Kupotea kwa elimu ya afya katika mashule na nyumba za kuabudia
3- Kuwa na familia za kisasa zisizojali maisha ya kiasili ya kifamilia 
na kujali zaidi maisha ya kisasa
4- Tabia mbaya kwa vijana kama vile ulevi, usagaji na ndoa za jinsia moja
5- Upatikanaji hovyo wa dawa za kuzuia mimba
6- Uvivu na uzembe wa kutokutaka kujifunza
7- Elimu isiyotolewa kwa mpangalio katika vyombo vya habari na katika
 mitandao.

Kwa nini ni muhumi sasa uwe na uelewa mzuri wa wa Mzunguko wa Hedhi ?.

1- Ili ujue siku zipi ni muhimu kwa ajili ya kupata mtoto
2- Ili ujue namna ya kuzuia kupata mimba zisizotarajiwa.

JE UNAANZIA WAPI KUHESABU SIKU YA KWANZA YA MZUNGUKO WAKO?.

Mzunguko wa kawaida wa hedhi ni siku 28 – 32. Kama zitakuwa chini ya siku 
28 hadi 24 basi huo ni mzunguko mfupi na kama zitakuwa zaidi ya 32 -35 
huo ni mzunguko mrefu. Ili kujua mzunguko wako ni mrefu au ni mfupi ni
 LAZIMA upate wastani wa mizunguko yako ya hedhi ya miezi mitatu 
Namna ya kuhesabu
1- Anza kuhesabu mzunguko wa hedhi yako kuanzia siku ya kwanza
 umepata hedhi yako
2- Na kisha malizia na siku moja kabla ya kupata hedhi nyingine ya
 mwezi mwingine.
3- Mfano umepata hedhi leo tarehe 8 basi nenda katika kalenda yako 
andika siku ya kwanza, kisha subiria mpaka unapopata hedhi nyingine, 
kama utapata hedhi nyingine tarehe 06 mwezi wa saba mana yake
 mzunguko wako wa hedhi umeisha tarehe 05 mwezi wa 7 na ni
 mzunguko wa siku 28
4- Baada ya hapo tafuta wastani wa mzunguko wako kwa miezi 
yako mitatu yaani mwezi wa 6-7, mwezi wa 7-8 na mwezi wa 8-9.

MAKUNDI MATATU YA SIKU ZA ZAKO NDANI YA MWEZI.

Ili tuelewane vizuri tutatumia mzunguko wa wastani wa siku 28 
ambao umegawanyika katika makundi matatu – Siku za hedhi – Siku
 Kupata Mimba – Na Siku Zisizokuwa za Kupata Mimba.

1- Siku yako ya kwanza ya mzunguko wako wa mwezi ndio siku ya
 kwanza ya hedhi
Siku za hedhi au SIKU ZA DAMU katika mzunguko wa siku 28 huwa ni 4-5. 
Hesabu kuanzia siku ya kwanza umepata hedhi mpaka siku ya mwisho ya
 kutokwa damu. Zinakuwa siku 4 hadi siku 5 lakini zinaweza badilika. 
2- Baada ya kumaliza siku 4-5 za damu, siku ya 6 hadi 10 NI 
SIKU AMBAZO kupata mimba NI VIGUMU, ingawa inaweza kutokea 
ukapata ujauzito.

Pia siku ya 19 hadi siku ya 28 ni siku ambazo sio rahisi au tuseme 
kwa ujumla haiwezekani kupata ujauzito
3- Siku ya 11 hadi ya 18 ni siku zenye UWEZEKANO MKUBWA wa 
kupata mimba. Katika siku hizi kama wewe unatafuta mtoto na huna 
matatizo yeyote ya kiafya basi inafaa kuongeza bidii katika tendo la 
ndoa ili kuongeza uwezekano wa kupata ujauzito.

NINI HUTOKEA KATIKA MZUNGUKO HUU?.

Kawaida ukipata hedhi basi jua ya kwamba yai lako liliokuwa
 limekomaa limekosa mbegu ya kiume hivyo ule ukuta uliokuwa
 umejengwa na damu kwa ajili ya kupokea mtoto na kumkuza umebomoka…
. Baada ya hapo mwili unaanza kuandaa yai lingine la mwezi unaofuata.

NOTE 1 – Tangu yai kutoka katika mfuko wake linaweza kukaa
 masaa 12 hadi siku 2 likiwa bado linauwezekano wa kurutubishwa
 na mbegu ya kiume na kuanza kuunda mtoto. 
NOTE 2 – Mbegu za kiume zinaweza kaa siku 3 hadi siku 7
 zikiwa na uwezo wa kurutubisha yai la uzazi.
NOTE #1 na NOTE #2 ni muhimu kuzifahamu ili ujue ya kwamba 
unaweza kosea masaa kadhaa na ukakosa kupata mimba hata 
kama huna matatizo yeyote ya kiafya au matatizo ya mzunguko 
wa hedhi. Ndio mana unatakiwa uwe na bidii sana katika tendo
 la ndoa kuanzia siku ya 11 hadi ya siku ya 18. Na hapa swala la 
urijali wa mwanaume ni muhimu pia kwa kuwa kama mwanaume 
utakuwa na mbegu hafifu zisizokuwa na mbio, mbegu chache, mbegu
 zenye kukaa muda mfupi na ambazo hazijakomaa vizuri basi ni rahisi
 sana kuyakosa masaa hayo ya uhai wa yai yaani masaa 12 hadi siku 2. 

KWA NINI SIKU ZA HEDHI HUBADILIKA BADILIKA. 

Katika maisha ya sasa ni rahisi sana siku za hedhi kubadilika kwa
 sababu mbalimbali lakini sababu kuu ni hali ya hewa (mabadiliko ya nchi au kusafiri), magonjwa na dawa kali za magonjwa, kuvurugika kwa homoni, 
msongo wa mawazo na unene uliopitiliza. Sababu zingine ni pamoja na hizi:
- Historia ya kutumia madawa makali ya uzazi wa mpango
- Ulevi, uvutaji sigara na madawa ya kulevya

USHAURI KUTOKA HEALTH POINT
1- Kumbuka ya kwamba unaweza kukosa kushika mimba 
kwa muda hata wa miezi sita lakini wewe na mwenzio mkawa
 wazima wa afya. KUPATA UHAKIKA LAZIMA UPIME.

2- PUNGUZA UNENE: Kama wewe ni mnene na una matatizo ya hedhi, 
Ukifanikiwa kupunguza uzito, utakuwa umemaliza asilimia kubwa ya
 matatizo ya hedhi.
3- Acha kabisa kutumia perfume, vipodozi na madawa ya kuongeza maumbile