Wednesday, January 10, 2018

Zijue Dalili Za Kuonyesha Kuwa Mpenzi Wako Amechoshwa Nawewe, Na Vipi Utauepuka Majanga Ya Kuachwa....Soma Hapa


Naamini kuwa mahusiano yako na mpenzi wako siku za kwanza kukutana na yeye yalikuwa ya kufurahisha kila wakati mnapokuwa pamoja.  Halafu muda ulivyokuwa ukisongea mumejiona mukipunguza moto ambao mlikuwa nao awali. Naongea ukweli? Hivi wewe na mpenzi wako mahusiano yenu yamefikia kilele cha kuanguka

Ni kawaida katika mahusiano kufikia pahali ambapo lazima kutatokea sintofahamu kati wa wapenzi wawili. Lakini habari njema ni kuwa pindi utakapomaliza kuzima hili chapisho utakuwa na nafasi nzuri ya kutatua matatizo yako na mpenzi wako.
 
Kutatua matatizo katika mahusiano yanahitaji kazi na kujitolea na baada ya muda mfupi matatizo yenu yatakuwa yametatuliwa bila shida yeyote kutokea. Baadhi ya matatizo makuu ambayo hutokea katika mahusiano ni kama yafuatayo:
 
1. Malumbano na vioja 
Hili ni tatizo kuu ambalo hutokea katika mahusiano na pia ni rahisi kulitatua. Ukimwona mpenzi wako kila mara yeye anapenda majibizano ama kurusha vitu huku na kule, ujue kuwa hii ni dalili ya kuwa anataka kuona mapya kutoka kwako. Kwa wanawake, wakianza majibizano ujue kuwa wanataka mabadiliko katika mahusiano aidha chanya ama hasi.
 
Tatizo ni kuwa kuboesha huua mahusiano kati ya wapenzi wawili. Na ukisema kuwa utajitenga ili upoeshe mahusiano yenu utakuwa unafanya makosa makubwa. Ukiona kuwa mpenzi wako anaanza majibizano ama vita vya kila wakati, kwa urahisi anajaribu kukuambia: "kama vitu havitaenda vile nataka mimi hakutakuwa na amani mimi na wewe kamwe". 
Vitu vya kufanya: 
- Akianza vita, fanya kukubali aendelee, hii itamsaidia kuitoa kwa damu yake
 
- Akianza drama ambayo haijulikani chanzo wewe jifanye hamnazo, na usikubali akuhusishe nayo
 
- Toka nje ya nyumba. Fanya vitu vya kufurahisha na yeye. Mnaweza kuenda kuangala sinema, sehemu za mapumziko ama hotelini
 
- Usionekane mtu ambaye una shauku ya kutaka kutatua matatizo yenu kwa uharaka
 
- Mjeuzie mchezo. Waweza kumrudia drama zote kwake. mfanye aingiwe na wivu.
 
2. Mpenzi wako hana muda na wewe 
Ni kawaida kwa mtu kuwa na sababu za kuwa bize ama kuwa na shughli nyingi, lakini kama utaona ya kuwa wakati kama huu biashara zake zimeongezeka kiasi cha kuwa hana muda na wewe, ni dalili tosha kuwa anajaribu kukutenga.
 
Kumbuka: Kama unapenda kufanya kitu ama kupenda mtu kawaida unajipa nafasi ya ili kukutana na vitu kama hivyo na si kungojea wakati mwafaka wa kupata muda
 Vitu vya kufanya: 
- Kuwa mtulivu. Usipayuke wana kumlalamikia.
 
- Mpatie nafasi. Usitumie nguvu, kumbabaikia ama kuonekana mwenye kutotosheka bila yeye.
 
- Mwonyeshe kuwa wewe una maisha yako na huwezi kupatika masaa 24/7 (hata kama unaweza kupatikana)
 
- Ukikutana na yeye mkumbushe kitu ambacho kilimfanya muanze mahusiano. Labda inaweza kuamsha hisia zake
 
3. Mpenzi wako amepoiteza hamu ya kufanya mapenzi 
Mpenzi wako akianza kudai ya kuwa hana mood ya kufanya mapenzi na wewe ama kuonekana hayuko mchangamfu mkiwa na yeye chumbani, uko na tatizo. Kutaka kurudisha mambo kama awali inahitaji kazi kubwa sana.
 
Jaribu kutafuta chanzo cha nyinyi wawili kupoteza hamu ya mapenzi. Inaweka kuwa labda imetokana na:
 
- Umekuwa mtu wa tamaa na atenshen yote inataka ielekezwe kwako
 
- Umepoteza ubinafsi wako na maisha yako yote yamefana na yake, umepoteza marafiki wako na vitu ambavyo umekuwa ukipenda kufanya
 
- Umepoteza umbo lako la zamani.
 
4. Miondoko yake ya mwili 'body language' inajielekeza kutoka kwako. 
Miili yetu haiwezi kuficha mambo ambayo tunapenda ama kuchukizwa nayo. Baadhi ya mambo ambayo yanawakilishwa na miondoko ya miili yetu ni kama:
 
- Hapendi kusmama kando yako mkiwa sehemu za hadhira
 
- Kila wakati anajaribu kujiepusha kumgusa sehemu yeyote yake ama harudi hisia wakati unapoanza
 
- Mkiwa pamoja mnakula anaangalia madirishani na milangoni
 
- Mkiwa mmeketi pamoja ataegemea upande wa kando na kwako na kuikumbata miguu yake
 
- Macho yake hayaingiwi na jazba ya furaha anapokuona, na uso wake unajeuja jiwe
 
KUMALIZIA: Baada ya kuorodhesha haya yote, unafaa kufahamu pia hapa duniani watu ni tofauti tofauti na tabia za mtu hubadilika kadri siku zinaposongea. Kama unaona kuwa mpenzi wako anahizi tabia tangu ukutane naye basi hio itakuwa ni swala jingine. Lakini wakati mwingi ni kuwa tabia hizi hudhahirika wakati ambapo mahusiano ya wawili yamekuwa taabani.