SEHEMU YA KWANZA
1.0 UTANGULIZI
Vipodozi visivyo salama ni vipodozi ambavyo vina kemikali zinadhuru au zinazoweza kuudhuru mwili na kuusababishia matatizo. Maana hii inaweza kuongezewa na kujumuisha vipodozi vyote ambavyo usalama wake unatia mashaka na vinaweza kuleta madhara kwa mtumiaji.
Hivyo hujumuisha :
Vinaweza vikawa ni mafuta, losheni, krimu, pafyumu, poda na kadhalika.
1.1 VIAMBATA (KEMIKALI) VYA SUMU VILIVYOPIGWA MARUFUKU
Vingi vikiwa katika lugha ya kiingereza, hizi ndizo kemikali ambazo huongezewa katika vipodozi ili kufanikisha au kusaidia dhumuni lililolengwa kwa kipodozi husika. Viambato vyenye sumu vilivyopigwa marufuku ni:
1.2 JINSI YA KUJUA KAMA KIPODOZI KINA KIAMBATO (KEMIKALI) CHA SUMU KILICHOPIGWA MARUFUKU
Angalia kwenye lebo ya kipodozi chako sehemu waliyoandika Ingredients au Contents au neno jingine lolote lenye maana ya Vitu vilivyomo ndani. Hapo angalia kama kuna kiamabato au kemikali yoyote ambayo nimeiandika hapo juu kuanzia namba 1 mpaka 12.
Kama kuna kiambato au kemikali ambayo imepigwa marufuku basi jua kipodozi chako sio salama. Acha kukitumia mara moja na toa taarifa kwa mamlaka ya chakula na dawa Tanzania (TFDA).
Kama hakuna kiambato cha sumu basi kipodozi chako kinaweza kuwa salama. Tatizo linakuja pale watengenezaji wanapofanya uhuni kwa kudanganya au kuficha na kuacha kuandika baadhi ya viambato vilivyomo ndani. Ambalo pia ni kosa kisheria.
Mifano
1.0 UTANGULIZI
Vipodozi visivyo salama ni vipodozi ambavyo vina kemikali zinadhuru au zinazoweza kuudhuru mwili na kuusababishia matatizo. Maana hii inaweza kuongezewa na kujumuisha vipodozi vyote ambavyo usalama wake unatia mashaka na vinaweza kuleta madhara kwa mtumiaji.
Hivyo hujumuisha :
- -Vipodozi ambavyo havijasajiliwa na mamlaka ya chakula na dawa Tanzania (TFDA)
- -Vipodozi vyenye viambata (kemikali) vya sumu na vilivyopigwa marufuku na mamlaka ya chakula na dawa Tanzania (TFDA)
- -Vipodozi ambavyo muda wake wa matumizi umeisha
- -Vipodozi ambavyo havioneshi tarehe ya kuharibika (mwisho wa matumizi)
- -Vipodozi ambavyo maelezo yake hayajaandikwa kwa Kiswahili au kiingereza
Vinaweza vikawa ni mafuta, losheni, krimu, pafyumu, poda na kadhalika.
1.1 VIAMBATA (KEMIKALI) VYA SUMU VILIVYOPIGWA MARUFUKU
Vingi vikiwa katika lugha ya kiingereza, hizi ndizo kemikali ambazo huongezewa katika vipodozi ili kufanikisha au kusaidia dhumuni lililolengwa kwa kipodozi husika. Viambato vyenye sumu vilivyopigwa marufuku ni:
- Chloroquinone (Hydroquinone na kemikali zingine)
- Steroids (Mifano ni Betamethasone, Beclomethasone, Hydrocortisone, Clobetasol, na Dexamethasone)
- Mercury (Zebaki) na kemikali zinazotokana nayo
- Chloroform
- Bithionol
- Hexachlorophene
- Mercury (Zebaki) na kemikali zinazotokana nayo
- Vinyl chloride
- Zirconium na kemikali zinazotokana nayo
- Methyelene chloride
- Halogenated salicylanilides (Dimetabromsalan, Trimetabromsalan na Tetrabromsalan)
- Chlorofluorocarbons (Kwenye pafyumu na deodorants)
1.2 JINSI YA KUJUA KAMA KIPODOZI KINA KIAMBATO (KEMIKALI) CHA SUMU KILICHOPIGWA MARUFUKU
Angalia kwenye lebo ya kipodozi chako sehemu waliyoandika Ingredients au Contents au neno jingine lolote lenye maana ya Vitu vilivyomo ndani. Hapo angalia kama kuna kiamabato au kemikali yoyote ambayo nimeiandika hapo juu kuanzia namba 1 mpaka 12.
Kama kuna kiambato au kemikali ambayo imepigwa marufuku basi jua kipodozi chako sio salama. Acha kukitumia mara moja na toa taarifa kwa mamlaka ya chakula na dawa Tanzania (TFDA).
Kama hakuna kiambato cha sumu basi kipodozi chako kinaweza kuwa salama. Tatizo linakuja pale watengenezaji wanapofanya uhuni kwa kudanganya au kuficha na kuacha kuandika baadhi ya viambato vilivyomo ndani. Ambalo pia ni kosa kisheria.
Mifano
- Sabuni ya JARIBU ina kiambato MERCURY. Sabuni hii sio salama, haifai kwa matumizi na imepigwa marufuku.
- Losheni/krimu ya MEKAKO ina kiambato HYDROQUINONE. Losheni/krimu hizi sio salama, hazifai kwa matumizi na zimepigwa marufuku
- Krimu za FAIR & LOVELY SUPER CREAM, VISIBLE DIFFERENCE CREAM, SKIN SUCCESS FADE CREAM, DEMOVATE NA DIPROSON CREAM zina viambata Krimu hizi sio salama kutumika kama vipodozi na zimepigwa marufuku
SEHEMU YA PILI
2.0 MADHARA YA VIPODOZI VISIVYO SALAMA
Vipodozi visivyo salama vina madhara mengi sana kwa afya ya mtumiaji. Na kama mtumiaji ni mjamzito basi madhara hayo yanaweza kumpata na mtoto aliyepo tumboni.
Pia vipodozi hivi vina athari nyingi sana kiuchumi kwani vitapelekea mtu kutumia pesa tena kugharamia matibabu ya matatizo atakayopata. Madhara hayo ni pamoja na:
- -Ugonjwa wa saratani (kansa) ya ngozi, maini, ubongo, mapafu, mfumo wa damu, utumbo mpana na kibofu cha mkojo
- -Uharibifu wa ngozi, macho, ini, mapafu na figo
- -Magonjwa ya moyo na kutopumua vizuri
- -Kutokwa na chunusi kubwa kubwa
- -Ngozi kuungua, maumivu makali, ngozi kuwa nyekundu na kutokwa na vipele
- -Ngozi kuwa nyembamba sana na laini na endapo ngozi itapata jeraha au kufanyiwa upasuaji, kidonda kitachelewa kupona au hakitapona
- -Mzio (Allergy) na muwasho wa ngozi
- -Kichefuchefu, kutapika, kusikia usingizi na kizunguzungu
- -Magonjwa ya akili, mishipa ya fahamu (hasa kichwani)
- -Uharibifu wa ubongo na mtindio wa ubongo kwa watoto wachanga na waliopo tumboni
- -Ngozi kuwa laini na kusababisha kupata magonjwa kama fangasi kwenye ngozi au maambukizi ya vimelea vya maradhi
- -Kuchubuka kwa ngozi
- -Ngozi kuwa na mabaka meusi na meupe au rangi mbalimbali
- -Upofu, uziwi na upotevu wa fahamu wa mara kwa mara
- -Kuumwa kichwa, kusikia kizunguzungu na kupoteza fahamu
2.2 USHAURI
Kama tulivyoona hapo juu mengi ya madhara ya vipodozi visivyo salama ni makubwa na huhatarisha kabisa afya za watumiaji na watoto. Hivyo ni vyema kuvijua na kuviepuka kabisa ili usiweze kupata madhara.
Pili msaidie kumuelimisha ndugu, jamaa na rafiki nay eye ajue na asitumie kabisa vipodozi visivyo salama
Pia ukiona mtu au duka ambalo linauza vipodozi visivyo salama acha kununua vipodozi kutoka kwake na toa taarifa kwa mamlaka ya chakula na dawa (TFDA) ili hatua zaidi ziweze kuchukuliwa
Epuka kabisa vipodozi visivyo salama. Hata kama vinakuletea matokeo mazuri kiasi gani.
SEHEMU YA TATU
3.0 ORODHA YA VIPODOZI VISIVYO SALAMA NA VILIVYOPIGWA MARUFUKU TANZANIA
Vifuatavyo ni vipodozi visivyo salama na vimepigwa marufuku kutumika. Epuka kabisa kutumia vipodozi hivi hata kama vinakuletea matokeo mazuri kiasi gani.
3.1 Krimu, Losheni na Jeli zenye kiambato cha Hydroquinone
- Mekako Cream
- Rico Complexion Cream
- Princess Cream
- Butone Cream
- Extra Clair Cream
- Mic Cream
- Viva Super Lemon Cream
- Ultra Skin Tone Cream
- Fade-Out Cream
- Palmer’s Skin Success (Pack)
- Fair & White Active Lightening Cream
- Fair & White Lightening Cream
- Fair & White Strong Bleaching Treatment Cream
- Fair & White Body Clearing Milk
- Maxi-Tone Fade Cream
- Nadinola Fade Cream
- Clear Essence Medicated Fade Cream
- Peau Claire Body Lotion
- Reine Clair Rico Super Body Lotion
- Immediate Claire Maxi –Beauty Lotion
- Tura Lotion
- Lkb Medicated Cream
- Crusader Skin Toning Cream
- Tura Bright & Even Cream
- Claire Cream
- Miki Beauty Cream
- Peau Claire Crème Eclaircissante
- Sivoclair Lightening Body Lotion
- Extra Clair Lightening Body Lotion
- Precieux Treatment Beauty Lotion
- Clear Essence Skin Beautifying Milk
- Tura Skin Toning Cream
- Madonna Medicated Beauty Cream
- Mrembo Medicated Beauty Cream
- Shirley Cream
- Kiss – Medicated Beauty Cream
- Uno21 Cream
- Princess Patra Luxury Complexion Cream
- Envi Skin Toner
- Zarina Medicated Skin Lightener
- Ambi Special Complexion
- Lolane Cream
- Glotone Complexion Cream
- Nindola Cream
- Tonight Night Beauty Cream
- Fulani Cream Eclaircissante
- Clere Lemon Cream
- Clere Extra Cream
- Binti Jambo Cream
- Malaika Medicated Beauty Cream
- Dera Heart With Hydroquinone Cream
- Nish Medicated Cream
- Island Beauty Skin Fade Cream
- Malibu Medicated Cream
- Care Plus Fairness Cream
- Topiclear Cream
- Carekako Medicated Cream
- Body Clear Cream
- A3 Skin Lightening Cream
- Ambi American Formula
- Dream Successful
- Symba Crème Skin Lite ‘N’ Smooth
- Cleartone Skin Toning Cream
- Ambi Extra Complexion Cream For Men
- Cleartone Extra Skin Toning Cream
- O’nyi Skin Crème
- A3 Triple Action Cream Pearlight
- Elegance Skin Lightening
- Clere Cream
- Clear Touch Cream
- Crusader Ultra Brand Cream
- Ultime Skin Lightening Cream
- Rico Skin Tone Cream
- Baraka Skin Lightening Cream
- Fairlady Skin Lightening Cream
- Immediate Claire Lightening Body Cream
- Jaribu Skin Lightening Lotion
- Amira Skin Lightening Lotion
- A3 Clear Touch Complexion Lotion
- A3 Lemon Skin Lightening Lotion
- Kiss Lotion
- Princess Lotion
- Clear Touch Lotion
- Super Max-Tone Lotion
- No Mark Cream
- Body Clear
- Top Clear
- Ultra Clear
- Peau Claire Lightening Body Oil
- G &G Dynamiclair Lotion
- G & G Teint Uniforme
- G & G Cream Lightening Beauty Cream
- Dawmy – Lightening Body Lotion
- Maxi White Cream
- Bioclare Lightening Body Lotion
3.2 Vipodozi vingine vyenye Hydroquinone
- Fair & White Powder (Exclusive Whitenizer & Serum)
- New Youth Tinted Vanishing Cream
- Skin Success Fade Cream Regular
- Teint Clair Clear Cpmplexion Body Lotion
- Mareme Cream
- Si Clair Plus Cream
- Clair & White Body Cream
- Body White Lotion
- Bio Claire Cream
- Forever Aloe MSM Gel
- Kroyons Baby Oil
3.3 Sabuni zenye kiambato cha Hydroquinone
- Body Clear Medicated Antiseptic Soap
- Blackstar
- Cherie Claire Body Beauty Lightening & Treating Soap
- Immediate Claire Body Beauty Soap
- Lady Claire
- G.C Extra Clear
- Top Clear Beauty Complexion Soap
- Ultra Clear
3.4 Vipodozi vyenye Hydroquinone pamoja na Steroid
- Clear Essence Skin Beautifying Milk For Sensitive Skin
- Fair & White Clarifiance Fade Cream
- Fair & White Exclusive Whitenizer Body Lotion
- Fair & White Exclusive Whitenizer Cream
- Fair & White Exclusive Whitenizer Gel
- Fair & White Maxitone Lightening Lotion Sun Block
- Fair & White So White Skin Perfect Gel
3.5 Sabuni zenye kiambato cha Mercury (Zebaki) na michanganyo yake
- Movate Soap
- Miki Soap
- Jaribu Soap
- Binti Jambo Soap
- Amira Soap
- Mekako Soap
- Rico Soap
- Tura Soap
- Acura Soap
- Fair Lady
- Elegance
- Block & White Skin Whitener Germicidal Bath Soap
- Rose Beauty Soap
- Maxi-Tone Soap (Skin Lightening Soap)
- Margostara Soap (New Tannin)
- Rusty – Whitening Soap (New Formula)
- Emani Natural Fair Pearls Soap
3.6 Krimu zenye kiambato cha Mercury na michanganyiko yake
- Pimplex Medicated Cream
- New Shirley Medicated Cream
Dexamethasone nk)
- Amira Cream
- Jaribu Cream
- Fair & Lovely Super Cream
- Neu Clear Cream Plus (Spots Remover)
- Age Renewal Cream
- Visible Difference Cream (Neu Clear Spots Remover)
- Body Clear Cream
- Sivo Clair Fade Cream
- Skin Balance Lemon Cream
- Peau Claire Cream
- Skin Success Cream
- M & C Dynamic Clair Cream
- Skin Success Fade Cream
- Fairly White Cream
- Clear Essence Cream
- Miss Caroline Cream
- Lemonvate Cream
- Movate Cream
- Soft & Lovely Cream
- Mediven Cream
- Body Treatment Cream (Spots Remover)
- Dark & Lovely Cream
- Sivo Clair Cream
- Musk – Clear Cream
- Fair & Beautiful Cream
- Beautiful Beginning Cream
- Diproson Cream
- Demovate Cream
- Top Lemon Plus
- Lemon Cream
- Beta Lemon Cream
- Tenovate Cream
- Unic Clear Super Cream
- Topifram Cream
- First Class Lady Cream
3.8 Vipodozi vingine vyenye kiambato cha Steroid
- Fashion Fair Gel Plus
- Hot Movate Gel
- Hyprogel
- Mova Gel Plus
- Secret Gel
- Secret Cream
- Peau Claire Gel Plus
- Hot Proson Gel
- Skin Success Gel Plus
- Skin Clear Gel Plus
- Soft & Beautiful Gel
- Skin Fade Gel Plus
- Ultra – Gel Plus
- Zarina Plus Top Gel
- Action Demovate Gel Plus
- Prosone Gel
- Skin Balance Gel Wrinkle Remover
- TCB Gel Plus
- Demo – Gel Plus
- Regge Lemon Gel
- Ultimate Lady Gel
- Topifram Gel Plus
- Clai & Lovely Gel
- Fair & White Serum Exclusive Whitenizer
- Maxi White Lightening Body Milk
- Maxitone Cleansing Milk
- Avoderm Cream
- Niomre Cream
- Niomre Lotion
- Nyala Lightening Body Cream
- Si Clair Cream
- Cute Press White Beauty Lotion
- White SPA Rose Lotion
- White SPA UV Lightening Cream
3.9 Vipodozi vya kupunguza unene vilivyopigwa marufuku
- Bio Valley Sliming Gel
3.10 Vipodozi vya nywele vilivyopigwa marufuku
- African Gold Super Glo
- Sofn Free Hair Foodblue Cap Shampoo
- Marhaba Anti-Dandruff Hair Cream
- Blue Cap Spray
- Blue Cap Cream
3.11 Vipodozi vinginevyo vilivyopigwa marufuku
- Bio Light Cream
- Salon Dermaplex Amazon Clay 9Normal To Dry Skin)
- Beauty Secrets Body Cream
- Swiss Soft N White Lightening Gel
- Whitening Complex Mask
3.12 Vipodozi Vinavyosababisha muwasho vikitumika karibu na macho
- Eye Shadow Gel
- Eye Shadow Gel 02
- Eye Shadow Gel 07
- Eye Shadow Gel 08
- Eye Shadow Gel 09
- Eye Shadow Gel 10
TAHADHARI : VIPODOZI VISIVYO SALAMA VIPO VINGI ZAIDI YA HIVYO AMBAVYO VIMEORODHESHWA HAPO JUU NA VINGINE VINGI ZAIDI VINAWEZA VIKAFIKA SOKONI.
Mara zote kuwa makini na vipodozi na pata taarifa, elimu na ushauri kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) na wataalam wa afya, urembo na vipodozi.