Friday, January 19, 2018

MAMBO 15 AMBAYO WANAUME WANAYATAKA KATIKA MAHUSIANO (LAKINI WANAWEZA WASIKUAMBIE)


Tunakupenda, tunakuhitaji, tunakutaka.lakini ni nini hasa tunatafuta kwa mwanamke?
Hatutapiga kelele,au kuandika, au kuweka  na kuonyesha katika profile,au kuongelea hilo sisi wenyewe.
Hapana. Wanaume wengi hawana tabia ya kusema wanachohitaji, lakini naweza kukuambia kutokana na uzoefu wangu mwenyewe, ingawa sio yote, wanaume wanakutaka  na kukuhitaji  uwafanyie vitu kama vifuatavyo.
1.WEMA WAKO.
Ulimwengu unaweza ukawa na ukatili na uonezi na adhabu ,kazi zetu zinaweza kuwa mbaya, na kukawa na ushindani mwingi, tunashughulika na kuhukumiana na kutofautiana kwa wale walio karibu yetu, kuhukumiana kidogo, kusameheana kidogo na uelewa kutoka kwa wanawake tunaowapenda  umeenda mbali.
2.FURAHA YAKO.
Tuambie umefurahi, tuonyeshe furaha, tunahitaji kuwepo karibu yako  unapokuwa na furaha, tutakuwepo wakati ukiwa na hali mbaya, kwenye tatizo lolote, lakini furaha yako ndio itakayokuwa inatuvuta  kuwepo karibu na wewe, pamoja na kwamba  yanatuhusu sisi  hayo.
3.SIFA NA SHUKRANI ZAKO.
Muda mwingine tunafanya vitu vizuri,  tuambie kuwa unashukuru  na unathamini  hicho na jinsi ulivyopendezwa na  na hicho na kukufanya uwe mwenye furaha, Onyesha  kuwa umeshukuru  kuwa na wao katika maisha yako, na unakubali company yao, mchango wao, na ushirikiano.
4.IDHINI YAKO.
Hatupendi kukubali, lakini mara nyingi  huwa hatufikirii kuwa kibali chako ndicho tunachohitaji, jinsi tunavyoishi au kutenda.Chukua hio nafasi  wakati tunapokuwa sahihi  kuturuhusu kufahamu kwamba umekubali.Tuambie umekubali maamuzi yetu, uchaguzi wetu,au jinsi tunavyoshughulikia vitu, tuambie  unafurahishwa na sisi na unaona fahari kuwa na sisi.
5.MGUSO WAKO.
Tunahisi mguso wako , kujali kwako, mabusu yako, urafiki wako kwetu ni muhimu sana-yawezekana  ni kidogo lakini ni muhimu .unapotugusa tunahisi kupendwa, unapokuwa muwazi kwetu kwa upendo mwingi,unatufanya tujisikie  ulimwengu ni wetu wote.
6.SHAUKU YAKO.
Tunakutaka wewe ututake sisi, tuambie kwamba uko ndani, jielezee shauku yako kwetu.
7.NGUVU YAKO NA KUSAIDIA.
Tunakuhitaji sana pale tunapopita katika changamoto nyingi za maisha yetu. Hata kama hatuwezi kuongelea hicho, tunahitaji mtu  mwenye nguvu ya kimya kimya, tunahitaji mtu wa kutuweka sawa, kusaidia,na kututia moyo, tuambie tuko nyuma yako   tunapokuwa tunapita katika matatizo mbalimbali.tunaweza tusiongelee hilo , lakini uwepo  wako pale tunapokuhitaji ni muhimu kwetu.
8.UELEWA NA UWEPO WAKO.
Sisi ni watatuzi na tunapenda kutatua mambo.tunaposhughulikia matatizo, hatuhitaji ufumbuzi  zaidi ya kukuhitaji uelewa wako na uwepo wako.inaweza kuwa hatuongei ni kitu gani kinatutatiza, lakini ukiwepo, na kuelewa na kuwa msaada hicho ndicho tunachotaka. Tunachotaka ni kujua kuwa hatupo peke yetu.
9.UNYENYEKEVU WAKO NA UWEZO WA KURUHUSU.
Tunataka mwanamke mwenye kutuheshimu na  anaeleta usawa, tunataka mwanamke  anaekubali kufikia mwafaka na ambaye anakubali kwa upesi bila kinyongo tunapoharibu.hashikili neno, anaweza kuachia bila kinyongo na kutoa nafasi  tena.
10.UKWELI WAKO.
Kama wewe,  tunahitaji tujisikie  kuwa sisi ni pekee katika maisha yako. Tusaidie tujisikie tunahitajika zaidi kwako kwa kutuonyesha  kwamba  una wajibu kwetu. Uwepo pale tunapokuhitaji, tusaidie kuliko mtu mwingine yeyote.
11.UAMINIFU WAKO.
Tunathamini uaminifu wako na kutuamini sisi, tunakutaka uwepo na sisi pale tunapokuhitaji , na kutuonyesha kuwa unajali.Kwa inshara hio hio  tunataka uamini kwamba tunategemewa, tunawajibika,na tutakuwa pale unapohitaji tuwepo.
12.UVUMILIVU WAKO.
Sisi sio wakamilifu,inawezekana sio mwanaume ambae ulimtarajia, tunakubali  uvumilivu wako kwa kutusaidia kukua katika mtazamo tunaoweza kuwa,hatuwezi kubadilika mara moja . msisitizo wako na uvumilivu wako utatufanya kubadilika jinsi unavyotaka tuwe.
13.MOYO MSIKIVU NA UCHESHI.
Maisha ni ya muhimu  na ya kuchukulia umakini sana,  watu hufanya makosa, hujikwaa,na hata kumsikitisha mtu, tunapopita katika magumu, mambo yanapotuchanganya ulimwenguni, tunahitaji kuwa na mtu fulani ambae atakupa furaha katika mambo madogo, ucheshi wako,furaha yako na kuonyesha kujali hutufanya tufurahie maisha zaidi.
14.URAFIKI WAKO.
Tunahitaji urafiki wako kila siku na kila mara.tunataka kufurahia muda na wewe, tunahitaji  kushiriki   mvuto wako, kutengeneza urafiki na kuteka mioyo yetu.
15.UMBALI WAKO (WAKATI MWINGINE).
Sio kwamba sisi ni wanaume wanaopenda kuishi kwenye mapango, wale wanaohitaji muda mwingi kuwa peke yao  kama tunavyotaka kufanya kwako, Lakini tunahitaji  kupata muda kidogo tu ili kucharge hisia  wakati mwingine, zawadi kubwa ambayo tunataka kutoka kwako ni kutoa  muda ili tuwepo peke yetu ili kujiona kuwa tunakuhitaji. Inatupa  balance na nafasi ya kukuhitaji zaidi.
Jipange .
mimi nimeanza kuelewa , kuvuliana , kuamini,kuwa mkweli , kuwa mnyenyekevu n.k . je wewe?

washirikishe na wengine makala hii wajifunze pale wanapokosea . Kisha toa maoni yako.