Sunday, January 7, 2018

MADHARA YATOKANAYO NA PICHA ZA NGONO MITANDAONI.

  
Mapenzi ni kitu nyeti sana katika tamaduni zetu za kiafrika, mapenzi ni kitendo cha faragha sana katika maadili ya kitanzania ambapo tunapaswa  kuheshimu, kukitunza na pia kukihifadhi sehemu husika kama vitabu vya dini vinavyosema.

Utandawazi ni kitu kipana sana kinachopaswa kutumika kwa mipaka kulingana na sheria za nchi na taratibu zilizowekwa na vyombo mbali mbali vya kisheria na kiserikali pia. Watu wengi wanajikuta wakiathiliwa na kutazama picha za ngono mitandaoni bila kujua.

Madhara ya kwanza ya kuweka picha za ngono katika mitandao yetu ya kijamii ni kubadilisha misimamo ya kimahusiano kwa walio wengi na kujikuta ukitawaliwa na tamaa za kimwili.

2. Kuongeza kiu ya kufanya mapenzi wakati wote umuonapo mwanamke au mwanaume kwa namna moja ama nyingine akiwa amevaa nguo fupi, za kubana nk.

3. Kutoka nje ya ndoa mara kwa mara kwa wale waliooa na hata walio bado kuoa huongeza idadi ya kuwa na wapenzi tofauti tofati kulingana na tamaa yao; kwa mfano weupe/weusi, warefu/wafupi, wanene/wembamba nk kwani kile ukionacho ndicho huingia akilini.

4. Kuongeza idadi ya kufanya mapenzi zaidi ya kawaida, kitu ambacho ni hatari kwa afya zetu na kwa maendeleo ya taifa letu.

5. Kufanya mapenzi kinyume cha maumbile kutokana na yale unayoyaona yakifanyika katika mitandao mbali mbali ya ngono. Jambo ambalo ni kinyume na vitabu vya dini na kisheria pia.

6. Wanafunzi wengi kuanza kufanya mapenzi wakiwa chini ya umri, kitu ambacho kuwaathiri kisaikolojia na ni hatari kwa afya zao.

MTAZAMO HURU kwa wanaomiliki website, blogs na mitandao ya kijamii kama Facebook, Folum Tweeter nk. hapa nchini tuwe wabunifu wakupata wasomaji, tukemee picha za ngono katika mitandao yetu kwani taifa la leo na kesho ni vijana na vijana wadogo.