Sunday, January 14, 2018

JE, UNAFAHAMU KAMA KUNYONYESHA UPUNGUZA HAMU YA KUFANYA NGONO??


 TAGS



Kunyonyesha hupunguza hamu ya sexKukosa hamu ya tendo la ndoa ni jambo la kawaida baada ya kujifungua mtoto na wakati mwingine huendelea hadi baada ya mwaka mzima hasa kwa mwanamke anayenyonyesha mwenyewe.
Wanandoa wengi hawajajua nini hutokea baada ya mtoto kuzaliwa na hasa mke anaponyonyesha mtoto na kujiona mke hana hamu tena ya tendo la ndoa.
Mwanamke anayenyonyesha huzalisha homoni ya Prolactin ambayo husaidia mwanamke kutengeneza maziwa ya mtoto na pia hupunguza hamu ya tendo la ndoa ingawa wanasayansi bado hawajaweza kutoa majibu kwa nini inakuwa hivyo.
Mwanamke anayenyonyesha mara nyingi hujisikia amechoka na wakati mwingine huchoka kama ng’ombe.
Hata hivyo kitu cha ajabu ni kwamba kwa upande wa mwanaume hamu ya tendo la ndoa hubaki palepale kama kawaida.

Na jambo kubwa zaidi ni kwamba mwanamke huelekeza nguvu zake zote kwa ajili ya mtoto ambaye amezaliwa.
Mtoto sasa ndiye anayekumbatiwa, anayepata busu na cuddling na mwanaume anakuwa kwenye reserve list na matokeo ni kwamba kuna kuwa na gap kubwa kati ya mke na mume wa kile mume anataka na mke anataka.

Wanandoa wengi iwe ni kunyonyesha kwa kawaida au kwa chupa huamini kwamba baada ya mtoto kuzaliwa itachukua kama miezi 2 tu na watarudi katika hali yao ya kwaida kusherehekea tendo la ndoa tena hata hivyo hujikuta wanakutana na roadblock ya mke kukosa hamu na matarajio makubwa ya aina hii husababisha mwanaume kuwa na big disappointment, frustrations na conflict.

Mwanamke aliyezaa kurudi kwenye hali yake ya kawaida ya kutaka tendo la ndoa kwa kwenda mbele hurudi baada ya miezi kadhaa baada ya kuacha kunyonyesha na wakati mwingine hata baada ya mwaka mmoja baada ya kuacha kunyonyesha.
Kama wanandoa watafahamu kwamba hili ni jambo la kawaida basi wanaweza kuwa na mazungumzo mazuri lini mke aweze kuacha kunyonyesha au pia kusimama pamoja kulea mtoto huku kila mmoja akifahamu kwamba sherehe za tendo la ndoa zitakuwa kwa mwendo wa kobe until further notice