Monday, November 20, 2017
UTOFAUTI WA MTAZAMO BAINA YA MWANAUME NA MWANAMKE KWENYE MAHUSIANO
Katika kipindi cha urafiki au uchumba ukisikia mwanaume anasema “huyu mwanamke hana future” kwake anamaanisha huyu mwanamke sio wakumtegemea kwenye masuala ya kimaendeleo huko mbeleni tukianza maisha, kiu ya mwanaume huyu ni kuona mwanamke anaye mchumbia anauwezo wa kujitegemea na kujisimamia, sio kuwa mke tegemezi, hapa “future” kwa mwanaume inamaanisha uimara wa maisha ya baadae. Kwa upande wa pili ukisikia mwanamke anasema “huyu kaka hana future” anamaanisha huyu kaka sio muoaji, hofu ya dada huyu ni kujikuta anatumia muda mwingi kuendelea kwenye mahusiano halafu mbeleni huyu kaka akasepa, au asiwe na mawazo ya kuoa na kuwa na familia. Hapa neno “future” kwa mwanamke linamaanisha kuwepo au kutokuwepo kwa utayari wa kuanza maisha ya pamoja “kuoana”. Hali hii au mtazamo huu uko vile vile hata pale mzazi wa kiume “baba” anapomuuliza kijana wake kuwa “huyo mchumba wako ana future?” au mzazi wa kike “mama” anapomuuliza binti yake “huyo kijana ana future?”