Watafiti hufanya kazi usiku na mchana kutatufa ukweli wa mambo ambayo yamekuwa mafumbo au tatizo kwa jamii husika kwa kipindi fulani.
Hiyo imepelekea kuwepo tafiti nyingi. Nyingine hupingwa kwa nguvu kutokana na kuwa na matokeo yanayowaacha midomo wazi watu wengi. Hata hivyo, kitaaluma tafiti hupingwa kwa tafiti.
Utafiti ulifanywa na wataalamu wa saikolojia nchini Malaysia umeonesha kuwa wanaume ambao hujichukulia kama watu wasio na pesa na mali kama walivyotarajia hupenda kuwa na wanawake wenye ‘maziwa na makalio makubwa’ zaidi ya wanaume ambao wanaishi katika maisha walioridhika nayo kifedha na mali.
Katika utafiti huo uliofanywa kwa kutumia sampuli ya wanaume 266 nchini humo, wanaume wengi kutoka jamii ya watu wa kipato cha chini waliwataja wanawake wenye maziwa makubwa kama wanawake wenye mvuto zaidi huku wale waliotoka kwenye maisha bora walichagua wenye maziwa madogo/wastani.
Kwa mujibu wa watafiti hao, sababu kubwa iliyowapelekea wanaume hao kuchagua wanawake wenye maziwa makubwa ni ishara ya kisaikolojia inayoonesha kuwa wanawake wenye maumbile hayo ni ishara ya kuwa na hazina kubwa ambayo huwafanya watengeneze picha ya ukubwa wa hazina kwenye ubongo wao.