Mwanaume anaweza kukusamehe kitu chochote kile, anaweza asijali kuwa ulichepuka hasa kama yeye labda ndiyo alikuwa sababu ya wewe kuchepuka lakini pale utakapochepuka na marafiki zake itakuwa ni ngumu sana kwake kukusamehe. Ni wanaume wachache sana ambao unaweza kutembea na rafiki zake na akakusamehe.
Tofauti na wanawake ambao mwanamke anaweza kumnyanganya rafiki yake mwanaume au akamfumania rafiki yake na mpenzi wake kisha akamsamehe mpenzi wake na kugombana na rafiki, kwa wanaume si hivyo. Wanaume wana pride, yaani ile hali ya kujiona bora na kutaka kuheshimiwa. Wana uanaume ndani yao ambao unaondoleka pale anapokufumania na rafiki yake.
Unapotembea na rafiki wa mume au mpenzi wako haiishii pale tu anapokufumania na labda kukusamehe lakini itaenda mbali kwa mwanaume kujisikia vibaya. Kila akikutana na yule rafiki yake na wakiongea chochote akili yake itawaza “Huyu jamaa kagonga mke wangu, anajua kila kitu kwa mke wangu…” Hiyo itamuumiza sana na kumfanya kukuchukia kila mara.
Anaweza kukusamehe kwakuwa anakupenda sana lakini mbele ya yule rafiki yake atajiona mnyonge na itakuwa ngumu sana kusahau. Kwa wanaume wengi hakuna kitu kinachokera kama kukutana na mwanaume mwingine ambaye anajua kila kitu kuhusu mkewe. Nikama wanaambiwa “Utaniambia nini wewe mkeo mwenyewe yuko hivi na vile!”
Lakini haiishii hapo, karibu kila mwanaume anaamini kuwa ukishatembea na mwanamke mara moja basi hana thamani tena na hata mkiachana bila kujali sababu za kuachana kwenu akikomaa sana anaweza kumrudia yule mwanamke au hata kupata mechi. Kwa maana hiyo basi akijua umempa rafiki yake kila siku atakua na wasiwasi kuwa anaweza kuchapiwa tena.
Hata akikuona unaongea tu au unapita maeneo yale, ukimtaja tu au kumzungumzia ataumia. Ningumu sana kwa mwanaume kusamehe kitu cha namna hiyo. kwa maana hiyo basi kama unampenda kweli epuka na kaa mbali kabisa na marafiki zake. Hata kama yeye kakusaliti kwa rafiki yako lakini kama bado unataka kumrudia usilipe kisasi kwa kumchukua rafiki yake.
Pia usijidanganye kua hatajua, duniani hakuna siri na ipo siku huyo rafiki yake atamuambia rafiki mwingine na meingine na hatimaye ikamfikia. Unaweza kutembea na rafiki wa mume wako leo lakini akaja kujua baada ya miaka kumi na akakuacha kwani kwake itauma kama ndiyo umefanya siku hiyo hiyo, ndiyo akili za wanaume zinavyofanya kazi hivyo kuwa makini.
Ataanza kukumbuka namna mlivyokua mnaongea, namna rafiki yake alivyokua anakusifia, namna alivyokuwa namkuta nyumbani na mambo mengine ambayo rafiki yake alikua anayafanya na kipindi hicho hakua na mashaka ila miaka kumi baadaye anakua na mashaka na hata ukimuambia ilikuwa kabla ya ndoa hatakuelewa.