Zifuatazo ni hatua za maendeleo ya mtoto katika kutumia lugha kwa mawasiliano
Tangu kuzaliwa hadi miezi 3
Maendeleo ya lugha kwa mtoto huanza punde tu baada ya kuzaliwa ,kwa muda wa mwaka mzima wa maisha ya mtoto huweza kupata uwezo wa kutofautisha sauti mbalimbali zinazotumiwa kwenye lugha,katika kipindi cha miezi 3 ya kwanza watoto huanza
- Kusikiliza sauti na kumtazama mzungumzaji
- Kutofautisha sauti za wazazi na sauti za watu wengine
- Kuonyesha tofauti ya miitikio ya kiasi cha sauti inayotolewa mfano sauti kubwa, sauti ya ukali,upole,furaha na kadhalika
- Kuwasiliana kwa njia tofautitofauti kama kulia, kucheka na tabasamu na kuanza kuiga sauti.
Miezi 3 hadi 6
Wakati mtoto hajaanza kuongea haimaanishi kuwa mtoto hajaanza kuwasiliana,mawasiliano ya mwanzo ya mtoto huegemea kwenye matumizi ya sauti,vitendo,lugha ya macho na huanza kusaidia maendeleo ya lugha kwa muda unaofuata.
Kuanzia miezi 3 hadi 6 mtoto huanza kufanya baadhi ya mambo haya yafuatayo;
Kubadilisha mionekano ya uso kuonesha tabasamu inayoashiria furaha kwa mlezi wake ama mzazi,kusikiliza mazungumzo ya watu wengine wanapozungumza
Miezi 6 hadi 9
Kwa kipindi hiki wazazi hushuhudia watoto wao kuongeza misamiati yao,wakati huu watoto huanza na maneno rahisi kama ‘’mama’’ dada’’ na bye katika kipindi watoto wengi huanza kurudia maneno anayoyasikia kutoka kwa watu wanaomzunguka
Miezi 9 hadi 12
Wakati mtoto anakaribia umri wa mwaka mzima uwezo wake wa kutumia lugha huongezeka kwa haraka watafiti wamebainisha kuwa wakati huu watoto hupata uwezo wa kuelewa lugha mara mbili zaidi katika kipindi hiki mtoto hupata uwezo mkubwa wa mambo kam;
- Kuelewa majina ya watu wengi na majina ya vitu
- Kutumia lugha ya mwili (facial expressions) kuonesha namna anavyojosikia mfano kutabasamu au kuhuzunika .
- Kuacha kitendo anachofanya mtoto wakati mtoto anapoambiwa ‘’acha’’ au ‘’hapana’’
- Kuweza kutamka maneno machache
Miaka 2 hadi 3
Katika kipindi cha mwaka wa pili watoto huanza kutumia lugha katika namna tata,katika umri wa miezi 24 ni kipindi kinachokadiliwa kuwa angalau nusu ya watoto wote hupata uwezo wa kutamka vizuri sentensi ndefu angalau maneno zaidi ya mawili,katika kipindi hiki mtoto huweza;
- Huweza kubainisha neno halisi katika kuelezea vitu mbalimbali
- Maongezi yake huweza kueleweka kwa wanafamilia wote
- Hupata uwezo wa kutumia vizuri aina ya maneno kama kielezi na kivumishi
- Kuweza kutumia maneno mawili hadi matatu kwenye sentensi
- Huweza kupata uwezo wa kueleza mambo mbalimbali yanayotokea mchana, katika wakati huu mtoto hupendelea kumsimulia mzazi ama mlezi vitu vilivyotokea mchana hasa mzazi pindi anavyotoka kazini.
Miaka 3 hadi 4
Katika umri huu mtoto huweza kuelewa lugha kiundani zaidi na huweza kuelewa vizuri mbinu mbalimbali za mawasiliano watu wengi zaidi nje ya familia huweza kuelewa zaidi lugha ya mtoto mwenye umri huu ,mtoto mwenye umri huu mara nyingi hupata uwezo wa ;
- Kutumia lugha bila kukosea matumizi ya maneno yanayoelezea wakati uliopita au wingi
- Kutumia vizuri matumizi ya nyakati kwenye sentensi
- Kujifunza kuimba nyimbo
Miaka 4 hadi 5
Watoto katika umri huu huongeza uwezo wa kumudu mazungumzo si kwamba tu huweza kuelezea kisa na mkasa pekee ila vilevile humudu kuelezea maneno katika ulinganifu uliosahihi mfano taratibu ,haraka na haraka zaidi,hatua zingine za kimawasiliano zinazofikiwa na watoto wenye umri huu ni kama ifuatavyo;
- Huweza kupata uwezo wa kutoa maelekezo zaidi ya matatu yasiyorandana
- Watoto katika umri huu hupendelea kusikiliza hadithi ndefu na hupata uwezo mzuri wa kuzikumbuka
- Huweza kutumia sentensi zenye wastani wa maneno manne hadi matano
- Hupata uwezo wa kuweka kwenye sentensi mawazo tofautitofauti
- Hupata uwezo wa kuuliza maswali mbalimbal kama kivipi,lini na kwanini vitu hivi vinatokea ?
- Anao uwezo wa kuongelea kuhusu taswira anazozijenga kichwani mwake za mambo yajayo,mfano natumaini baba atanipa hela nikimweleza shida yangu