Mbuzi dume (beberu) amepata nafasi ya kujiunga rasmi na jeshi la Uingereza na kupata namba kamili ya jeshi akiwa na wadhifa wa ‘kuruta’.
Mbuzi huyo aliyepewa jina la Fusilier Llywelyn alijiunga na jeshi hilo rasmi Ijumaa iliyopita baada ya kuruhusiwa na Malkia, siku kadhaa baada ya kumaliza mafunzo maalum ya gwaride la kijeshi.
Beberu huyo mwenye umri wa miezi 10, amepewa nyumba ya makao makazi ya jeshi kama wanajeshi wengine na anatarajiwa kuhudhuria gwaride maalum la Malkia.
Utamaduni wa kumsajili mbuzi katika jeshi la Uingereza ulianza mwaka 1844. Mbuzi huyo alifahamika kama Billy na alistaafu jeshi kwa heshima kama wanajeshi wengine.