Mimi nimwanamke wa miaka 27 nimeolewa miaka mitatu iliyopita. Katika kipindi cha miaka miwili ya ndoa yetu tulikuwa bado hatujajaaliwa kupata mtoto, tulienda hospitalini na wote hatukua na matatizo ni Mungu tu alikua hajapanga. Mimi nafanya kazi katika shirika moja la kimataifa na mume wangu ni mfanyakazi wa Benki moja kubwa hivi na ana cheo kikubwa tu huko.
Mwaka huu katikati nilikuwa na sagfari ya kikazi Kenya ambapo kulikuwa kama na kongamano flani la vijana na tulikutana na vijana wengi wengi wakiafrika kutoka nachi mbalimbali tulikaa huko kama wiki mbili hivi. Tatizo nikuwa wakati nikiwa huko kuna kijana mmoja kutoka Ghana ambaye tulijikuta tunakuwa marafiki ghafla na kufanya mambo yetu mengi pamoja.
Kusema kweli alikuwa anani treat vizuri kiasi kwamba nikajikuta navutiwa tu kuwa naye, si kimapenzi bali kama rafiki. Sasa wakati tunakaribia kumaliza kongamano tukawa tumefanya kasherehe kaodogo hivyo ingawa si mnywaji sana lakini siku hiyo nilikunywa. Kama unavyojua pombe ukisema unaonja haishii hapo unajikuta unakunywa mazima.
Nilikuwa na yule kijjana na yeye alikunywa , ingawa mwanzoni alikua akiniheshimu kwani nilimuambia nimeolewa lakini siku ile alianza kunishikashika kifuani na sehemu nyingine, nilijikuta napata hamasa na kushindwa kujizuia na tuliporudi hotelini baada ya sherehe sikurudi tena chumbani kwangu, alinipeleka chumbani kwake na tulifanya mapenzi mpaka asubuhi.
Sisemi kwamba ni pombe ilisababisha kwa asilimia 100 lakini imechangia, kwani hakunibaka na nilikubaliana na kila kitu. Kwa mapenzi aliyonionyesha hata saubuhi sikushtuka tulifanya tena ndiyo nikarudi chumbani kwangu kwani nilishakata tiketi ya ndege kurudi Bongo. Wakati huo sikuumiza kichwa kwani nilijua kuwa ilikuwa ni siku moja tu na mtu mwenyewe wambali hivyo sikujisikia vibaya sana.
Kinachoniumiza sasa nikwamba, wiki mbili baada ya kutoka kule nilianza kujisikia vibaya, nilipitisha siku zangu na nilipoenda kupimwa nilikuta nina ujauzito. Mume wangu amefurahi sana mimi kuwa mjamzito kwani ni kitu mabacho alikuwa anakiomba siku zote lakini kila nikipiga mahesabu na nikifikiria vizuri najua kabisa hii mimba si ya mume wangu.
Kwanza kabisa wakati nikiwa kule ile siku tuliyofanya ndiyo ilikuwa siku yangu ya hatari, pili niliporudi kwenye safari nilijifanya kuchoka sana hivyo hatukufanya na mume wangu na alisafiri kama siku tano hivi. Ingawa ni siku chache na naweza kumfanya kuamini kua mimba ni yake lakini bado roho inaniuma, najiona msaliti na nashindwa nifanyeje. Naomba ushauri nimuambie ukweli mume wangu au nivumilie nimuache alee mtoto ambaye si wake?
Habari Mahusiano Live; Naomba ushauri kwa wasomaji wa jarida hili, tafadhali ficha jina langu.
imi nimwanamke wa miaka 27 nimeolewa miaka mitatu iliyopita. Katika kipindi cha miaka miwili ya ndoa yetu tulikuwa bado hatujajaaliwa kupata mtoto, tulienda hospitalini na wote hatukua na matatizo ni Mungu tu alikua hajapanga. Mimi nafanya kazi katika shirika moja la kimataifa na mume wangu ni mfanyakazi wa Benki moja kubwa hivi na ana cheo kikubwa tu huko.