Tendo la ndoa limezungukwa na mambo mengi sana ambayo hata wataalam wa mahusiano na madaktari bingwa wameshindwa kuyamaliza. Tafiti mbalimbali zimekuwa zikija na matokeo mapya na hata kubadili matokeo ya tafiti za awali kutokana na muda husika.
Leo, nimeamua kukueleza kuhusu mambo matano tu kati ya hayo mengi, unayopaswa kuyafahamu kwa ajili ya ufahamu wako tu lakini pia kwa afya yako ili yakusaidie katika maamuzi unayochukuwa unapokuwa eneo la tukio au unapopanga kufanya tukio hilo. Hii imewalenga zaidi watu walio kwenye ndoa na kuwaandaa wanaotaka kuingia kwenye ndoa.
Kumbuka tendo hili ni ‘la ndoa’. Najua hii ngumu kumeza!
- Mwanaume hutoa mbegu hadi milioni 300 kwa tendo moja tu la ndoa, lakini mbegu moja pekee hutumika kuzalisha mtoto inapokutana na yai la mwanamke lililotayari.
- Kufika kileleni kwa mwanamke ni msaada mkubwa kiafya kwake. Huweza kumsaidia mwanamke kupunguza hatari zaidi ya kupata magonjwa ya moyo, kupooza, kansa ya matiti pamoja na msongo wa mawazo.
- . Mwanamke anapokuwa kileleni hukaa takribani sekunde 20 hadi 14, tofauti na wastani wa mwanamme ambaye hukaa kwa wastani wa sekunde 6 tu. Hata hivyo, tofauti na mwanamke, mwanaume anapokuwa kileleni hupitiwa na giza zito katika ubongo wake kwa sekunde takribani tatu (blackout).
- 4. Tendo la ndoa hupunguza maumivu ya kichwa.
-Utafiti uliofanywa na wa wataalam wa saikolojia na uhusiano kutoka Chuo Kikuu cha Munster chini Ujerumani umebaini kuwa tendo la ndoa husaidia kupunguza maumivu ya kichwa. Utafiti huo uliochapishwa mwaka 2013, ulibaini kuwa mtu mmoja kati ya watano waliofanya mapenzi wakiwa na maumivu ya kichwa, alimaliza akiwa hana maumivu hayo tena.- Kwenda haja ndogo muda mfupi kabla ya tendo la ndoa ni hatari zaidi kwa afya.
UTI hutokea pale kibofu cha mkojo kinapopata bakteria wanaoingia kupitia njia ya mkojo. Na tendo la ndoa linaweza kusaidia maambukizi wa bakteria hao kuwatoa kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine.
Kwa mujibu wa Dk. David Kaufman wa New York Marekani, kwenda haja ndogo kabla ya kufanya tendo la ndoa ndio chanzo cha kupata athari kubwa zaidi ya bakteria ikiwa kutakuwa na maambukizi.
Alieleza kuwa kwenda haja ndogo kunasaidia kuweka nafasi kubwa zaidi kwenye kibofu cha mkojo kiasi cha kutunza bila kusumbuliwa, bakteria wengi zaidi.
Hata hivyo, ni salama zaidi kwenda haja ndogo muda mfupi tu baada ya kufanya tendo la ndoa kwasababu inasaidi ku-flash bakteria kwa kiaisi kikubwa waliotokana na tendo la ndoa (sio virusi vya ukimwi).