Kama haungi mkono kila hatua unayopiga kwenye maisha yako na yote unayotaka kufanya ni muda wa kufikiria upya uhusiano huo. Haijalishi ni kitu gani unafanya, ni muhimu awe nyuma yako kukupa support.
2. Anakupa muda wa kupumua
Kuna tofauti kati ya kujali na kuwa kupe. Ni kawaida kwake kukuangalia hapa na pale kujua siku yako inaendaje, lakini kama anatokea tu hovyo kazini kwako kila siku, hiyo inaweza kuwa ni issue.
3. Anakubali marafiki zako – ama walau anajifanya kuwajali
Kama hawapendi marafiki zako, hakuna jinsi utaweza kuchagua kati yao na yeye. Kama anakulazimisha kuchagua kati ya pande hizi mbili basi ni muda wa kumwacha aende. Kama anakupenda kweli hatakufanya uchague kati yao na yeye.
4. Anaipenda familia yako kama unavyoipenda
Hili ni muhimu. Kama haelewani na ndugu zako ni ngumu sana kudumu naye. Kama familia yako ni muhimu zaidi kwako atapenda kuwa karibu nao kama unavyopenda. Kama huleta ugomvi kila mnapoenda kwa wazazi wako ama anapokupa visingizio vya kutoenda, basi hakufai.
5. Yuko tayari kwa lolote, ilimradi yuko nawe
Hii ina maana kuwa anakuwa tayari na ameridhika kuwa nawe. Kama kila siku analalamika juu ya vyote unavyotaka kufanya huenda hamko kwenye ukurasa mmoja.
6. Anakupenda kama ulivyo
Kama mara zote huudhiwa na vitu kuhusu kadhaa kuhusu wewe, huenda akawa anataka kukubadilisha na sio kukupenda kama ulivyo. Kama huna uhakika kuwa anakupenda ulivyo, basi ni muda wa kusonga mbele.