Mlikuwa kwenye mahusiano kwa muda mrefu akakuacha akaoa mwanamke mwingine, halafu bila aibu anakurudia anataka uwe mchepuko wake. Halafu na wewe bila aibu unakubali unataka kushindana na yule aliyeolewa, unaanza mikakati ya kuivunja ndoa yake. Hembu ona aibu, kama alikuacha unapaswa kujiuliza kwanini alikuacha? Si kwabahati mbaya au si kwasababu ulimkosea, mwanaume anayekupenda atakusamehe hata kwa kosa gani.
Lakini hata tuseme kweli alikuwa anakupenda na ulimkosea sana akakuacha kwa hasira. Unafikiri utapata nini sasa? Unafikiri atamuacha mkewe kwajaili yako? Anakuona kama takataka chombo cha starehe lakini hana upendo kwako. Hembu siku muambie amuache mkewe akuoe wewe halafu utasikia majibu yake! Ahca kujidhalilisha na kujizibia riziki, mwenzako ashaendelea na maisha yake na mke wake wewe badala ya kutafuta wakwako unang’ang’ania.
Bila kujali sababu za kuachana kama kakuacha na kuoa mwingine jua wewe ni takataka kwake sasa, mwisho wa siku utaishia kugongwa na usiku ataenda kwa mkewe. Unaweza ukajibebesha na mimba lakini watoto wako hawatakua na haki kama watoto wake wa ndoa, jithamini, uthamini mwili wako na acha kujirahisisha namna hiyo. Kashakudharau, ameshaonyesha kuwa wewe huna hadhi ya kuwa mke wake sasa kwanini uwe jalala za matatizo yake ya ndoa?