Thursday, November 23, 2017

Jinsi familia zinavyoathiriwa na teknolojia


Maendeleo ya kiteknolojia ni muhimu kwa maendeleo ya jamii yoyote duniani Kama inavyoonekana katika nchi zilizoendelea mfano Japan, China na nchi kama Marekani na Uingereza.
Ukuaji wa teknolojia umekuwa na matokeo hasi katika nchi ambazo bado zinahitaji maendeleo zaidi hasa nchi za kiafrika kwani ukuaji wa teknolojia unategemewa kuwa ndiyo njia pekee ya kuzikomboa nchi ambazo bado zipo katika janga la umaskini.
Aidha, Teknolojia mpya ya mitandao ya kijamii imekuja kwa kasi sana katika kuvuruga mahusiano baina ya wanafamilia, marafiki na ndugu na hata katika kubadili mienendo na maadili ya watu.
Hata hivyo, Simu za mikononi zimeleta mapinduzi makubwa katika kuboresha mawasiliano na zimechangia maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa kiwango kikubwa lakini pia zimeleta balaa kubwa katika kupotosha maadili na kuchangia ufisadi katika mahusiano ya familia na ya kimapenzi.