Friday, November 17, 2017
JIFUNZE JINSI YA KUKONTROL HISIA ZAKO(lean how to control your feelings and emotions)
Karibu mpenz msomaji ndugu,kaka,dada.baba,mama rafiki na wengine wote katika makala hii fupi inayozungumzia namna ambavyo unaweza kuzitambua hisia zako na kuziongoza katika kukuletea faida na si hasara. Kama ambavyo unafahamu HISIA ni moja ya vitu ambavyo vinachukua nafasi kubwa sana katika maisha ya mwanadamu yeyote na ni moja kati ya mabo nyeti sana na yenye kuleta matokeo makubwa sana katika maisha ya kila siku. kwa wale wasiofahamu HISIA hutia ndani Mapenzi,chuki,wivu,tamaa, hamu ya ngono n.k hivi vyote na vinginevyo vingi ni vitu vinavyounda kituu kinachoitwa HISIA.
Awali ya yote acha tutambue hisia nini na ina nafasi gani katika maisha ya mwanadamu kwa kuwa kitaalamu ili kutatua tatizo yapasa kwanza kulifahamu tatizo halisi pamoja na uzito lilio nao hivyo basi pia ili tuweze kutambua namna ya tutakavyoweza kucontol hisia zetu ni lazima tutambue maana halisi ya hisia na nafasi yake katika maisha yetu ya kila siku.
HISIA&AKILI
Kwanza kabisa maisha ya mwanadamu yeyote yule yanaongozwa na vitu vikuu viwili. Vitu hivyo vinafanya kazi mithili ya mapacha wawili wasiofanana. mkubwa kati ya mapacha hao anaitwa AKILI na mdogo ndio anaitwa HISIA tunaemzungumzia hapa. Wawili hawa wote ni sawa na wote ni muhimu sana katika maisha ya mwanadamu na wote wanafanya kazi kwa bidii kubwa kila siku katika maisha ya mwanadamu ili kuhakikisha mwanadamu anaishi kwa amani na furaha ni kama zawadi ya pekee ambazo mungu amempatia mwanadamu ili aweze kujiendesha na kufurahia maisha.
TOFAUTI ZILIZOPO
Tofauti kubwa zilizopo kati ya hawa mapacha wawili ni kuwa AKILI ni mwenye busara na siku zote hupenda mambo mema na yanayomfaa mwanadamu na mara nyingi hufanya maamuzi sahihi. Tatizo kubwa linalomsumbua bwana AKILI ni kwamba hana nguvu za kutosha.
HISIA yeye hana busara wala hafikiliagi chochote. ni mwenye pupa na mara nyingi huwa analazimisha apate anachokitaka hata kama haiwezekani, lakini kitu pekee anachojitambia huyu bwana HISIA ni kuwa ana nguvu nyingi sana kuliko ndugu yake AKILI.
TATIZO
Tatizo kubwa linatokea ni kuwa muda wowote pale ambapo AKILI anatumia busara zake kufanya maamuzi sahihi na yenye tija HISIA anatumia nguvu zake nyingi kumpinga na kwakua AKILI hana nguvu za kutosha anajikuta anashindwa kupambana na HISIA na hivyo mwanadamu anajikuta ameshatumbukia katika tatizo bila kutaka. mfano; (Unaweza kuta mtu anateswa sana katika mahusiano yake na AKILI yake inamuonyesha waziwazi kuwa hahitajiki tena na kumtaka aachane na mahusiano hayo na kujipumzisha na mateso lakini HISIA anatumia nguvu zake nyingi akisema kwamba bado anapahitaji sana mahali hapo au mahusiano haya na AKILI anashindwa nguvu na mwanadamu kujikuta akiteseka kufanywa mume/mke bwege na huku akili ikimwuonyesha waziwazi kua hatakiwi lakini bado anabaki kung'ang'ana palepale. anayefanya kazi pale ndio huyu HISIA tunaemzungumzia
WHAT IS A SOLUTION NOW
Souttion sasa ni kijifunza namna ya kumzoeza AKILI yako kumshinda HISIA zako. Tukutane tena katika maada ijayo ambapo sasa tutaweza kuona ni namna gani unaweza kumzoeza AKILI yako kupambana na nguvu za nduguye HISIA zako....