Wednesday, November 8, 2017

HATUA 5 ZA UHUSIANO WA MAPENZI

Kwa nini baadhi ya mahusiano ya mapenzi  huvunjika na mengine hudumu daima?

Je, umewahi kujiuliza “Kwa nini ni uhusiano wetu una shida sana? Mambo yalikuwa mazuri sana tulipoanza,nini kimetokea? “

Jibu ni kwamba mnaweza mkawa mmetoka katika hatua moja na mko katika hatua nyingine ya mapenzi.

Uhusiano wa mapenzi hupitia katika hatua kubwa 5 zinazoenda katika mfuatano,na wakati ungine kujirudia. Ni muhimu sana kwa watu ambao wapo katika uhusiano wa mapenzi kufahamu hatua hizi ili kuweza kukabiliana na changamoto zake ili kufanikisha mahusiano yao.

Katika kila hatua kuna changamoto zake. Watu tofauti hutumia muda tofauti katika kila hatua. Wengine huenda kwa haraka na wengine hukaa katika kila hatua au baadhi yake kwa muda mrefu zaidi.

Makala hii inaonesha hatua hizi na kuangalia changamoto katika kila hatua na jinsi ambavyo wapenzi wanaweza kukabiriana nazo.

Hapa ni hatua 5 ya uhusiano kama ambavyo imebainishwa na watafiti katika mahusiano ya wapenzi:

1. Mahaba(“Romance”)
2. Uhalisia na Ugomvi
3. Kujitathimini na Kujitambua
4. Kujirudi na Utulivu
5. Makubaliano na Kujitoa

Hatua mbili za mwanzo ni hatua ngumu na wapenzi wengi wanaishia hapo. Hivyo ni hatua ambazo wapenzi wanahitaji kuzizingatia zaidi na kujipanga kukabiliana na changamoto zake.
Hatua #1: Mahaba (Ulevi wa Kupenda)

uhusiano-wa-mapenzi_mahaba

Ni asili kila mtu kupenda. Hii ni hatua mabayo kila binadamu anapitia.

Kila mtu anahitaji mtu wa jinsia nyingine kuwa mwenza wa maisha yake. Mapenzi ni mojawapo ya mahitaji mengi ya kimwili, kihisia na hata kiroho kwa mwanadamu.

Mara nyingi tunakutana na watu ambao tunatofautiana sana kuliko kulingana. Hii ni wazi kutokana na kukua katika familia na mazingira tofauti. Kama tofauti hizi zingefahamika mapema basi watu wengi wasingeingia hata katika hatua hii ya awali.

Sayansi ya Kupenda:
Unapoingia katika mapenzi na mtu ubongo wako unatengeneza mchanganyiko wa kemikali na kuziachia mwilini. Kemikali hizi ni pamoja na Oxytocin, Phenylethylamine na Dopamine. Kemikali hizi huongeza mapingo ya moyo na kusisimua mwili. Na hali hii ndiyo tuyoita mapenzi au mahaba.
Hali hii ni sawa kabisa na ile ambayo watumiaji wa madawa ya kulevya wanaipata.

Kama walevi wa madawa,mtu ambaye ameingia katika mapenzi anaanza kuona vitu tofauti ni uhalisia. Vitu vinaonekana ni vizuri sana na ubaya unajificha kabisa. Unaona vile vitu vizuri tu ambavyo vinakufanya ujisikie vizuri na kupuuza vyote ambavyo vinakufanya ujisikie vibaya.
Ulevi huu unakufanya uone vile vitu ambavyo wewe na mpenzi wako mnafanana na kutupilia mbali vile vyote mnavyotofautiana na vibaya.

Unakufanya pia useme na kufanya vile ambavyo vinampendeza na kumfurahisha mpenzi wako pekee.

Hali hii itaendelea mpaka kilevi kikiisha nguvu na huweza kuchukua muda wa miezi 2 hadi miaka 2. Katika hatua hii, ubongo wako unaaacha kuzalisha kemikali hizi za mapenzi na unajikuta unashangaa ilikuwaje umekuwa na mtu huyo.
Hatua #2: Uhalisia na Ugomvi (Mapambano ya Mamlaka)

uhusiano-wa-mapenzi_uhalisia

Asilimia kubwa ya talaka za ndoa na kuvunjika kwa mahusiano hutokea hapa. Ni kipindi cha miaka 3 na 4.

Watu wanaanza kuona mambo kwa uhalisia na mnagundua hamfanani na mnatofautiana sana.

Hiki ni kipindi kigumu kwa wapenzi wengi,ni kipindi cha kukata tamaa na hasira. Ni kipindi ambacho ndoto zenu za kupendana daima zinaingia dosari.

Hivyo, unapata kazi ya kuanza kujaribu kumbadirisha mwenza wako ili awae kama ulivyofikiri alikuwa au kama ambavyo ungependa awe.

Ugomvi na na hata kupigana kunatokea katika hatua hii.

Hatua hii inaweza kuchukua miezi michache hadi miaka mingi, kutegemea na hatua ambazo wapenzi hao wanazichukua au kupata masaada toka kwa wengine.

Bila maarifa ya kupambana na ugomvi huu wa mamlaka na kutatua tofauti zao na kujitambua,wapenzi watarudi katika hatua hii mara kwa mara katika uhusiano wao.

Namna ya Kukabiliana na Hatua Hii

Kuna njia kadhaa ambazo wapenzi wanaweza wakachukua kukabiliana na matatizo yao wao wenyewe au kwa msaada wa watu wengine wa nje.

    Kukubali na kufahamu tofauti ya kila mmoja
    Kujifunza kugawana mamlaka, na kutambua kwamba kutumia nguvu kamwe hakutasaidia kupata unachokitaka
    Kutambua nafasi yako katika mahusiano
    Kukubaliana na maisha kwa jinsi yalivyo

Vyovyote vile ilivyo kukabiriana na kushinda hatua hii si kazi rahisi na walio wengi wanashindwa na kuvunja mahusiano ya muda mrefu.
Ukweli ni kwamba kushinda hatua hii ni muhimu sana kushirikisha na kupata msaada wa watu wengine,iwe ni ndugu rafiki au wataalamu wa ushauri wa mahusiano.
Hatua #3: Kujitathimini na Kujitambua

uhusiano-wa-mapenzi_Kujitahmini

Katika hatua hii kila mmoja anajitathmini kama anahitaji kuendelea na mahusiano au la.

Wapenzi wanatengeneza utengano kati yao na upendo unapungua sana kipindi hiki. Kujitenga na kuwa mbali kihisia kunatokea kati yao.

Ni rahisi kwa wapenzi kudanganya na kujihusisha na wapenzi wengine.
Hatua #4: Mapatano

uhusiano-wa-mapenzi_mapatano

Baada ya kipindi kirefu cha tathimini na wakafanikiwa kubaki pamoja,wapenzi wanatambua namna ya kushughulikia matatizo yao kwa namna ambavyo wote wanafaidika.

Katika hatua hii, hatimaye inakuwa wazi kuwa huwezi kubadili tabia ya mwenza wako na unaamua kumpokea na kumpenda kama alivyo.

Unakubali ukweli kuwa mpenzi wako yuko tofauti na wewe. Mnaamua kuweka mipaka yenu wazi na kujifunza kuheshimiana. Kama hii haiwezekani basi mnarudi tena katika hatua ya nyuma ya ugomvi.

Msisimko wa kuwa katika mapenzi unarudi zaidi ya ilivyokuwa katika hatua ya kwanza.

Katika hatua hii hasa ndio unakuwa tayari kuingia katika ndoa na kuwa na mipango ya pamoja ya muda mrefu.
Hatua #5: Makubaliano na Kujitoa

uhusiano-wa-mapenzi_makubaliano

Katika hatua hii ya uhusiano wa mapenzi wapenzi wanakuwa wameamua kuwa pamoja na kama timu wanafanya mambo pamoja.

Wapenzi wanapendana ki kweli na wameamua kuwa pamoja ukiachia tofauti zao.

Wapenzi wanakuwa marafiki katika hatua hii. Inasemekana asilimia ndogo sana ya wapenzi wanafika katika hatua hii (inakadiliwa kuwa chini ya 5% ya wapenzi wote)


Kuhitimisha..

Hatua hizi haziendi moja ka moja katika mfuatano. Mara nyingi huenda mbele na kurudi nyuma tena kama wapenzi hawazingatii na kuelewa mambo ya muhimu ya kukabiliana na changamoto za jatua husika.
Wapenzi wengi wanafunga ndoa wakiwa bado katika hatua za mwanzo. Wengi wanakuwa katika ulevi wa mapenzi na wanaishia kuachana. Ni muhimu sana kupitia hatua hizi na kuzifahamu.

Unapofahamu changamoto za kila hatua ni rahisi kwa wapenzi kuwa wavumilivu na kutafuta mbinu za kuatatua matatizo yao na kukua katika uhusiano wa mapenzi.

Je unafahamu wewe na mpenzi wako mko katika hatua gani?