Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, Kamishna Msaidizi, Francis Massawe alisema tukio hilo lilitokea usiku kwenye Kitongoji cha Qendangonyi, Kata ya Ganana wilayani Hanang’.
Kamanda Massawe alisema chanzo cha tukio hilo ni wivu wa mapenzi na majeruhi amepata kilema cha maisha baada ya sikio kutolewa.
Alisema wanamshikilia dereva teksi kwa uchunguzi wa tukio hilo kabla ya kumfikisha mahakamani.