Kitendo cha kutongoza kina ufundi wake, na wanaume walivyo wajanja (kwa wale wenye uelewa) wana maarifa yao ya kutongoza. Maarifa hayo hutofautiana tegemeana na aina ya mwanamke ambaye wananiya ya kumtongoza. Licha ya kuwa maarifa haya yametofautiana, mwisho wa siku sababu za yeye kutongoza mwanamke huwa mle mle – sababu za msingi hufanana na moja ambayo ni kubwa kuliko zote ni tamaa.
Katika ulimwengu wa utongozaji mambo yamebadilika sasa to the extent hata akina dada/mama huwa tunajilipua once in a while. Ila ukweli unabaki bado kwa kiasi kikubwa wanao ongoza kutongoza ni akina kaka/baba. Na katika kutongoza huko wengi huwa na sababu mbali mbali za kumtongoza huyo mtongozwaji.
Zinazofuata ni sababu hizo zinazomfanya huyo kaka/baba afanye maamuzi na kufanyia kazi malengo yake ya kumpata huyo anae kuwa kadaka jicho lake. Hizi ni sababu tokana na mtazamo wangu ambazo huwa vigezo vya sababu ya kutongoza mwanamke:-
Anakujaribu
Ni mara nyingi nimesikia kaka/baba zetu wakiweka wazi kukubaliwa na mwanamke aliye mtongoza na kukubaliwa bila kutarajia. Ni kuwa just for the sake of it, mazingira yanakuwa yanaruhusu anajikuta kutongoza kwa kujifurahisha na kujaribu alafu anajikuta mwanamke kakubali. Kama hajajipanga anatahamaki na hata kushindwa kuendeleza azma ya kukutana naye kimwili hasa kwa vinajana ambao hawana makazi badala yake hulelewa na familia hivyo kuwa na sehemu ya kukutania na mwanamke kwa ghafla ni mtihani kwake. Mwingine akikujaribu ukakubali atalala na wewe na hali mwingine atakupotezea na mwanamke akibaki akishangaa inakuwa kakubali na hatafutwi.
Kakutamani
Hii ndio sababu inayo ongoza kwa sababu zote za akina baba/kaka kutogoza. Uzuri, Urembo, Mvuto wa dada/mama husika hucheza nafasi kubwa ya mtongozaji kuvutiwa hadi akataka kuwa na wewe. Hii hutokana na ukweli kuwa kiasi kikubwa cha wanaume anapotongoza malengo yake inakuwa kukupata na kuweza kufanya sex na mwanamke huyo. Hata hivyo vivutio vimetofautiana, kuna wale wanafutiwa na miguu, wengine sura, wengine midomo na wengine weengi makalio (kwa kaka/baba zetu hawa wa kibongo).
Kakupenda
Hii ni mara chache, mara nyingi kigezo cha kwanza mwanaume kutongoza huwa kuvutiwa na huyo mwanamke then kupenda kunakuja baadae. Hata hivyo kuna exceptions; mfano kama vile huyo mwanaume anapokuwa yupo mahala ambapo anakutana na huyo dada mara kwa mara. Siku ya kwanza alipo muona hakuwa na wazo kabisa la kumtongoza, ila with time kwa kuendelea kumuona pengine hata kwa kuendelea kuwasiliana kama wana mazoea anajikuta kampenda tokana na tabia or sababu zozote zile alizonazo hivyo kuamua kutongoza. Hii sababu ina probability kubwa ya kuishia kwenye ndoa.
Ana ngunge (Horny) Anahitaji pa kupooza haraka
Ana hitaji kwenda kupoza hamu ya ngune alilo nalo. Pengine anakuwa hajakutana na mwanamke muda mrefu au tu ni aina ya mtu ambaye ana hamu kila mara au kila akiona aina ya mwanamke ambae kamtamani. Hivyo mwanaume kutongoza kwa kigezo hiki ina maana huyo mtongozwaji ndiyo akaonekana chaguo zuri la kuweza kuubali haraka bila uchelewefu wa kwenda kukutana kimwili. Mara nyingi hii hutokea kwa mwanamke ambae ni kazi yake hio (yaani dada poa) au yule anayejulikana mtaani kama mama Huruma.
Wa ku beep/Hamaanishi
Huyu ni aina ya yule mwanaume ambae hayupo committed. Yeye siku zote anakuhitaji wewe siku akitaka kukutana kimwili. Yaani mara nyingi anacheza na hisia zako.. Anakuwa anakujua vema… Namna ya kukuweka sawa, namna ya kuahakikisha huna wasi wasi juu yake na namna ambavyo kukutana na wewe ni lazima siku ambayo anataka kufanya na wewe uone kawaida. Anaweza akawa hata na galfriend/mke huko but akawa na mwingine kwa ajili ya sex tu.
Kukuoa
Hii utokea pale mwanaume anapokuta mwanamke katimiza vigezo anavyotaka kwa mke wake, kama vile utulivu, upole, usafi, aina ya kazi n. k. Inakuwa kamjua tabia yake (iwe kwa muda mrefu ama mfupi) na zikamvutia kutaka kuwa nae kwa muda mrefu zaidi tena kama mke na mume kabisa. Hii ni mara chache, mwanaume huja mpole sana, sex inakuwa si priority sana. Yupo haraka kutaka kukufahamu zaidi wewe na familia yako na anakuwa na bidii ya kutaka kuhakikisha hata upate mimba mara moja.
Mahusiano
Huyu anapenda kuwa safe. Anataka mwanamke wa kuwa nae pamoja kama partner, awe rafiki, waweze kukutana kimwili na wawe waaminifu. Mara nyingi anakuwa kalenga wewe ndio uwe the special lady. Hata ikitokea ana wengine mwisho wa siku huyo mwanamke wa kujenga nae mahusiano anakuwa makini zaidi na invest zaidi katika huo uhusiano.. Mara nyingi ikienda vizuri hata huishia katika ndoa.
Kukuchuna/Kukutumia
Huyu mwanaume anataka mwanamke anae onekana una uwezo wa kujikimu kila kitu. Unaonekana independent na huoni taabu kum support mwanaume. Hivyo hutaka wepesi… Haoni taabu siku ya kwanza mmetoka ama siku zingine zote wewe ukitop up the bill ziku zote. Kwake anakuwa so set on enjoying bila kujali partnership ya kweli katika mahusiano hayo.
Kukuzalisha
Hii ni nadra.. Siku hizi kaka/baba zetu anakutamkia kabisa… Hasa hawa ambao hawataki ku commit na kuoa. Ma senior bachelors. Inafika wakati anajua kabisa mke sitaki, but nataka niwe na mtoto so the shortcut anatafuta mwanamke mwenye mwelekeo wa kuwa mama mzuri, tena kwa kiasi kikubwa awe anajiweza kuweza kulea mtoto na anakushawishi ubebe mimba. Pengine hata kwa uongo wa nitakuoa. Ingawa hii ni wachache sana.
Wa kuzugia
Mwanaume wa namna hii ni yule anataka mwanamke kwa sababu si ya dhati. Kwa kiasi kikubwa anakuwa na huyo mtu kwa sababu maalum. Mfano; anaweza kuwa yupo gay, hayupo tayari sexuality yake ijulikane hivyo anatongoza mwanamke wa kuwa nae (wengine hata kuoa kabisa) ili nae aonekana ana mwanamke na hivyo mwanaume wa kawaida katika macho ya watu.
Ujumbe kwa akina dada/mama wenzangu:-
Kuna wakati ni mtihani kujua mwanaume anakutongoza kwa ajili gani. Ila siku zote tunacheza na insticts na pengine kuingia katika mahusiano kana kwamba wacheza kamali. All in all kuna wale ambao wapo so obvious na ni rahsi kujua sababu ya yeye kukutongoza. Faida ya kujua hilo ni wewe kutoa maamuzi kama upo tayari uwe nae kwa vigezo ambavyo vimemfanya aje kwako.
Usikose kukutana namimi katka makala ijayo….