Sunday, October 29, 2017

YAFAHAMU MADHARA MAKUU MATATU YA KUTUMIA PAFYUMU, DEODERANT NA SPRAY MWILINI.

                                                                  
mtu mmoja rafiki yangu sana, nilisoma naye sekondari miaka ya nyuma kidogo aliwahi kunipigia simu na kuniuliza madhara ya kutumia haya marashi ya kunukia kama perfum, deodorant, body spray na kadhalika. alinigusa sana kwani ni moja ya janga kubwa kwenye jamii ambalo halifahamiki na leo naenda kutumbua jipu hili mapema kabisa ili utumie ukijua..marashi haya yanaleta matatizo magonjwa yafuatayo kutokana na kemikali ya aluminium iliyoko ndani ya aina nyingi za marashi kama ifuatavyo...
kansa ya matiti: utafiti uiofanyika hivi karibuni umegundua kwamba kansa nyingi za matiti yaani kwa wanaume na kwa wananawake zinatokea upande wa juu wa titi kwa nje, karibu kabisa na pale unapopaka marashi yako.. utafiti huu uliongeza kwamba kemikali hizi ikiwemo aluminium huzuia harufu kwa kuziba matundu ya jasho na kufanya mwili ushindwe kutoa uchafu wake, lakini pia kemikali hizi mara nyingi huingia kwenye damu wakati mtu amenyoa na kuacha michubuko kwenye ngozi ya kwapa,  kemikali hizi zikiwa ndani ya damu huingiliana na DNA na HOMONI za mwili na kuzaa kansa.
ugonjwa wa alzeheimers; huu ni ugonjwa unaoshambulia ubongo hasa kipindi cha uzee, mgonjwa hupata hali ya kusahau kia kitu mpaka jina lake wakati mwingine. utafiti uliofanyika nchini marekani ulikuta watu hawa wakiwa na kiasi kikubwa sana cha kemikali ya aluminium kichwani ambazo kwa hali ya kawaida iligundulika wagonjwa hao walizitoa kwenye marashi yao ambayo wakipaka kwa maisha yao yote. 
ugonjwa wa figo; ugunduzi huu ulifanyika miaka ya nyuma kidogo ambapo wagonjwa wengi wenye shida ya figo hua wana kiasi kikubwa sana cha phosphorus kwenye damu zao na matokeo yao walianza kupewa alumimium hydroxide kupunguza kiasi cha phosphorus mwilini, lakini baadae wakagundua aluminium ile ilikua haitoki mwilini vizuri hivyo ikaamuliwa na shirika la viwangovya  dawa na chakula marekani, kwamba marashi yote yenye aluminium yawekwe wazi ili watu hawa wasitumie.lakini je? unafikiri wewe ambaye kwa sasa ni mzima hupati madhara yeyote ya figo kwenye aluminium zilizoko kwenye marashi yako?
mwisho; sijaandika maka hii ili watu waanze kunuka. hapana, kuna njia za asili za kuzuia harufu ya kikwapa kwa kutumia vitu asili au kutumia marashi yaliyotengenezwa bila kemikali hizi..zipo kampuni zinatoa marashi yasiyokua na kemikali hizi japokua hapa kwetu ni adimu sana. kampuni nayoifahamu yenye bidhaa hizi ni kampuni ya FOREVER LIVING ambao bidhaa zao wanazitengeneza kiasili na kuweka mmea wa aloe vera. kampuni hii ina wasambazaji mikoa mbalimbali unaweza onana nao na kutumia marashi yao ili kua salama au ukatafuta vyanzo vingine unavyoviamini.