DALILI ZA MATATIZO YA HEDHI
Siku chache kabla ya hedhi, baadhi ya wanawake hupatwa na hofu na huwa wenye hasira. Husumbuliwa na mfadhaiko wa akili, huumwa na kichwa, matiti hujaa maziwa, hukosa usingizi na kuvimba sehemu za siri. Hali hii husababishwa na kukosekana kwa uwiano wa homoni (Homone imbalance) na hali hii huweza kukoma ndani ya saa 24 baada ya kuanza hedhi.
MAUMIVU MAKALI YA HEDHI
Wengine hupatwa na maumivu makali sana wakati wa hedhi. Maumivu hayo huwapata akina mama ama siku mbili ama tatu kabla au mara tu waanzapo siku zao. Hali hii pia inasababishwa na kutokuwepo kwa uwiano wa homoni mwilini, ambako kumesababishwa na ukosefu wa virutubisho fulani.
Wengine hutokwa na damu nyingi kuliko kawaida au kukaa katika siku za hedhi kwa kipindi kirefu kuliko kawaida. Kuna sababu nyingi zinazoweza kuchangia hali hii, ikiwemo kuugua kwa muda mrefu, kupatwa na hofu, huzuni, mshtuko na sababu nyingine za kitabibu.
JUISI YA MBOGA MBOGA HUTIBU
JUISI YA MBOGA MBOGA HUTIBU
Kwa kutumia vyakula asilia unaweza kuepukana na maumivu ya mara kwa mara wakati wa siku zako. Katika orodha ndefu ya juisi za mboga zinazotibu kwa uhakika matatizo yote ya hedhi, ni Kotimiri (Parsley), mboga ya majani ambayo upatikanaji wake ni rahisi. Kwa mujibu wa watafiti, Kotimiri ina uwezo wa kurekebisha uwiano wa homoni hivyo kuondoa matatizo kadhaa ya hedhi.
Inaelezwa kuwa uwezo wa Kotimiri kurekebisha matatizo ya hedhi unatokana na kuwa na aina ya kirutubisho kiitwacho ‘Apiol’ ambacho pia kimo miongoni mwa homoni za jinsia ya kike (estrogen). Maumivu na mvurugiko wa siku hurejea katika hali ya kawaida kwa kunywa juisi ya Kotimiri mara kwa mara. Aidha, juisi hiyo inapochanganywa na juisi ya viazi pori (Beet Root), karoti au matango huwa na nguvu zaidi. Kiwango kinachoshauriwa kuchanganya kiwe na ujazo sawa kwa kila aina ya juisi utakayochanganya. Juisi yenye mchanganyiko huo ni rahisi kutengeneza na ni dawa inayoweza kumsaidia mwanamke wakati wote wa maisha yake bila kuhitaji kutumia dawa zingine kali za kuzuia maumivu (pain killers) ambazo huwa na madhara baadaye.
TANGAWIZI NAYO HUTIBU

Tangawizi nayo ni dawa nzuri sana ya kutibu matatizo yatokanayo na hedhi, hasa katika tatizo la maumivu makali na kutokupata hedhi. Chukua kipande cha tangawizi mbichi, kiponde na kiweke kwenye kikombe cha maji ya moto kwa dakika chache, kisha tia sukari kiasi na unywe mchanganyiko huo, kwa siku mara mbili kila baada ya mlo.
UFUTA NAO NI DAWA
Ufuta (Sesame) nao ni miongoni mwa mbegu za asili unazoweza kula na kutibu matatizo ya hedhi. Saga ufuta na pata unga wake kisha uchanganye na maji ya moto, kunywa mara mbili kwa siku. Kinywaji hiki huondoa maumivu wakati wa hedhi kwa wasichana wadogo.
Ukitumia mara kwa mara kinywaji hiki cha ufuta, hutibu pia tatizo la kupata hedhi kidogo. Pia unaweza kuchangaya maji ya kuoga ya uvuguvugu na mbegu za ufuta zilizopondwa pondwa kiasi cha kiganja kimoja, nayo hutoa nafuu kubwa kwa wanaosumbuliwa na maumivu, hasa ukitumia siku mbili kabla ya siku zako.

PAPAI NALO NI DAWA
Mungu ametuumba na kutupa mazao mengi ambayo yana uwezo wa kutatua matatizo yetu ya kiafya, iwapo tutagundua siri hiyo. Papai bichi nalo linaelezwa na watafiti wetu kuwa lina uwezo wa kulainisha misuli ya njia ya uzazi hivyo kufanya utokaji wa hedhi kuwa mwepesi usio na maumivu. Papai huwa na manufaa zaidi kwa wasichana haswa kwa wale wenye tatizo la kutopata siku zao kutokana na kuwa na ‘stress’ au mawazo. Utapata faida hiyo kwa kula mara kwa mara tunda hilo bichi (ambalo halijaiva lakini limekomaa)