Friday, October 27, 2017
KWANINI NI BORA KUNYWA BIA LAINI[LIGHT BEER] KULIKO BIA YA KAWAIDA[REGULAR BEER]?
bia ni nini?
bia ni kilevi cha zamani zaidi kinachotumiwa sana duniani, ni kinywaji cha tatu kunywewa na watu duniani baada ya maji na chai. kinywaji hichi hutokana na kuchachishwa kwa kwa mazao kama mahindi,mchele na ngano.
bia huangozewa aina ya maua kwa jina la hops ambayo huifanya bia kua chungu na kuitunza isiharibike ikiwa ndani ya chupa.
siku hizi kuna bia laini ambazo ni rahisi kuzitambua kwa sababu zinaitwa light mfano castle light lakini pia kuna bia za zamani ambazo hua na majina ya kawaida tu mfano castle lager, safari lager, serengeti na kadhalika.
bia ina mchanganyiko gani?
bia ya aina yeyote hua na mchanganyiko wa maji, maua ya hops ambayo huifanya isiharibike na kuifanya chungu, ngano, mchele au mahindi ambavyo huchacha na kuleta ladha ile ya bia, uyoga ambao ndio chanzo kikuu cha kuchacha kwa bia, lakini bia huongezewa kemikali zingine ambazo huifanya kua iwe safi na kung'aa.
kwanini inashauriwa kunywa bia laini kuliko bia ya kawaida?
kwa hali ya kawaida watu wanajua bia ni bia tu lakini kitaalamu kuna utofauti, ukiwa unataka kunywa bia ni bora unywe bia laini au light beer kwasababu za tofauti zifuatazo.
kiwango cha cha nguvu au calorie; hii ni nguvu inayopatikana kwenye bia ambayo inatokana na kiasi cha ngano, mahindi au mchele kinachowekwa, bia za kawaida zina calorie nyingi kuliko bia laini mfano chupa moja ya bia ya kawaida lina calorie 150 wakati chupa moja ya bia laini ina calorie 110. hivyo mtu anayekunywa bia ya kawaida atanenepa zaidi na kuota kitambi kuliko yule anayekunywa bia laini.
kiwango cha kilevi au alcohol; bia za kawaida zina kilevi kikubwa zaidi kuliko bia laini na mnywaji hujikuta amelewa sana kwa kunywa bia chache tu hivyo kama unahitaji kunywa kiwango kidogo cha kilevi, kukaa sehemu muda mrefu bila kuchoka, kua salama bila kuibiwa, au kuweza kuendesha gari baadae na kufurahia ni bora kunywa bia laini kwani hata ukiamua kunywa maji mengi sana baada ya kuinywa inaisha haraka mwilini.
hang over au uchovu wa asubuhi; bia laini huisha mwilini haraka sana, mtu anaweza kunywa bia hizi na bado kesho yake akaamka vizuri na kwenda kazini lakini bia za kawaida ukizinywa basi kesho yake yote utaipoteza ukiwa katika hali ambayo sio ya kawaida na hana ufanisi wako wa kazi hautakua mzuri.
bei ya bia; kwa hali ya kawaida bia laini hua ina bei kidogo kuliko bia ya kawaida japokua hapa nchini kwetu ni kama zinalingana bei lakini kwa nchi zilizoendelea bia laini zina bei ndogo ila kwa sababu dunia imeanza kujua bia laini ni nzuri zaidi kiafya basi uhitaji wa bia hizi umekua mkubwa mpaka zinaanza kupanda bei. mfano nchini marekani kati ya bia 10 zinazonunuliwa basi 7 ni bia laini.
ladha ya bia; bia za kawaida zina kiwango kikubwa sana cha pombe au alcohol hivyo ina ladha kali sana kuliko bia laini...bia laini zina ladha nyepesi sana na ni nzuri kwa watu ambao hua sio watumiaji wa pombe kama wakihitaji kunywa kwa siku hiyo.
mwisho; pamoja kua kitaalamu inashauriwa kunywa bia laini kuliko hiyo ya kawaida, bado ukinywa kupitiliza kiwango utapata matatizo hata kama ni laini hivyo kunywa kwa kujiheshimu na isiuzwe chini a miaka 18