Tuesday, October 31, 2017
KUDUMU KATIKA NDOA YAKO
Zipo changamoto ambazo zinazosababisha ndoa nyingi kufa. Hata hivyo kufa kwa ndoa hizo husababishwa na vitu vidogovidogo ambavyo watu wengi wamekuwa hawavitilii maanani. Hata hivyo siku ya leo nimeona ni vyema nikujuze siri ya kudumu katika mahusiano ya ndoa. Je ni vitu gani? Twende sawa:
1 mapenzi ya kweli.
Ili uweze kudumu katika ndoa yako ni lazima uwe na mapenzi ya kweli kwa mwezi wako. Upendo wa kweli mara kadhaa huwa haupimwi kwa maneno tu bali ni kwa vitendo. Hivyo katika kuhakikisha unafurahia maisha ya mahusiano hakikisha unajua ni kipi kitokachomfanya mpenzi wako ajue ya kwamba unampenda. Hilo ni suala la msingi ambalo ni vyema ukalijua.
2. uvumilivu.
Kitu ambacho pia kitakusaidia kuweza kukaa kwa muda katika ndoa yako ni kuhakikisha unalijua lile somo la uvumilivu. Kama ambavyo siku ya ndoa yenu mliampa ya kwamba mtadumu katika ndoa yenu katika shida na laha. Hivyo ili kuweza kulitimiza hilo ni lazima ukumbuke kiapo chenu. Hii itawasidia sana kuweza kutengeneza maelewano ndani ya nyumba.
3 hofu ya mungu.
Ndoa yeyote ile ambayo inataka kuwa imara ni lazima iwe na hofu ya Mungu ndani yake. Kama mliapa ya kwamba mtaishi pamoja mpaka kifo kitakapo watenganisha, hivyo ili yote hayo yawe kweli ni lazima Mungu atawale katika ndoa yenu ili muweze kutimiza lile ambalo mlikuwa mmeliahidi mbele ya Mwenyezi Mungu pamoja na mashaidi wengine.
4 uwezo wa kujishusha.
Hakuna kitu muhimu katika mahusiano kama hiki. Kuwepo na uwezo wa kujishusha katika mahusiano kunafanya mahusiano hayo kuimarika. kwani ndoa nyingi hufa kwa sababu ya kutokuwa na mtu mmoja ambaye anajishusha. Hata ugomvi wa wanandoa wengi hutokea kwa sababu ya kutokuwepo kwa kitu hicho. Hivyo ili uweze kudumu katika ndoa ni kazima uwe na uwezo kujishusha hasa pale unapokosea. Pia katika suala la kujishusha ni lazima ujue matumizi ya samahani. Neno samahani lina thamani kubwa katika kuongeza upendo kwa mwenzi wako.
5 Matumizi mazuri ya pesa.
Hili ni la muhimu kwa wanandoa. Kwa upande wa wanaume ili uweze kuwa bora, ni lazima uweze kuepuka matumizi mabaya ya fedha ambayo kwa mkeo yatakuwa ni kero. Na pia kwa mwanamke ili kumfurahisha mwanaume ni lazima awe na nidhamu ya fedha, hapa nikiwa na maana ya kwamba fedha za matumizi ambazo unaachiwa au kutafuta mwenyewe ni lazima uweze kuzitumia katika mpangilio.
6. Uchaguzi mzuri wa marafiki.
Ukiwa katika ndoa ni lazima uwe na marafiki sahihi ambao mwezi wako watampendeza kitabia, kwani wapo baadhi ya marafiki wao kazi yao ni kuvunja ndoa za watu. Watu hawa kazi yao ni kichwa maneno kutoka upande A kwenda upande B.
Marafiki wa aina hii hawafai hata chembe. Hivyo ili kudumu katika mahusiano ya ndoa lazima ufanye uchaguzi sahihi wa marafiki.
Mpaka kufikia hapo sina la ziada tukutane hapa hapa tunazungumzia kuhusu elimu ya mahusiano