Mwanaume anaweza kukupenda sana na wewe ukaona kabisa kuwa anakupenda. Lakini unapaswa kujua kitu kimoja, wanaume wengi hawaoi kwasababu wanapenda, kwasababu wana pesa na wanadhani wanaweza kuhudumia familia au kwasababu wanahofia kukupoteza.
Wanaume wengi huoa kwa sababu kuu mbili, sababu ya kwanza ni ya ngono, kwamba wanaoa kwakua wanataka mtu wakufanya naye mapenzi kila wakati wanapohitaji. Hii nimeiweka sababu ya kwanza lakini si sababu kubwa sana kwa wanaume, wanaume wengi huoa kwa sababu ya kazi za ngumbani.
Hapa nifafanue kidigo na wanawake muwe makini, wanaume wengi ni wavivu katika kufua, kufanya usafi wanyumba, kupijka, kuosha vyombo, kutandika kitanda na vitu kama hivyo. Wanapenda kuona hivyo vitu vinafanyika na wanaamini kuwa wanawake wana nguvu za ajabu kuvifanya vitu hivyo.
Anaweza kupata ngono sehemu yoyote, anaweza kuzaa na mwanamke yoyote lakini kama akirudi nyumbani anakutana na nguo chafu, anakutana na vyombo vya juzi, anakutana na vumbi kila sehemu na anakila kitu cha kumfanya aoe basi ataoa.
Hii ndiyo maana kama mwanamke ukijifanyisha mke ukahamia kwake na ukawa unamfanyia yote hayo miaka itaenda bila ndoa, unamtimizia kila kitu, unamfanyia kila kitu ambacho angependa mke amfanyie sasa akuoe wanini. Lakini hiyo sio mada yangu ya leo.
Mada yangu nikuwa unapoingia kwenye ndoa acha kiburi, eti kwakua una kazi na una kakipato unajifanya hufui, unajifanya hupiki, eti unataka nayeye asaidie kazi za ndani au mfanyakazi wa ndani ndiyo afanye kila kitu. Unanunua chakula kila siku hotelini au kila siku anakula chakula cha house girl!
Nikuambie kitu utaachika au atatafuta sehemu ambayo anafanyiwa vitu hivyo. Kwa mwanaume mpaka ajihisi mwanaume nilazima awe na mwanamke wa kumpikia, wakumfulia, wakumfanyia usafi ndani na vitu kama hivyo usipo vifanya wewe atavitafuta kwa mtu mwingine kwani ndiyo ambavyo vinamfanya ajihisi mwanaume.
Kama ambavyo wewe ukiwa na mwanaume ambaye hatoi matumizi na hakuhudumii kwa chochote hujisikii kupendwa hata kama kitandani shughuli yake ni pevu ndiyo hivyo hivyo kwa mwanaume. Lazima awe na mtu wa kumuambia kuwa leo nataka kula kitu flani akatoa pesa na kikapikwa, kama hufanyi hivyo jua kuna anayefanya kwaajili yako.
Usijifanye uko bize sana, eti kwakua una mfanyakzi basi unafurahia, eti kwakua na yeye hakuulizi kwanini hupiki hata mara moja moja, kwanini nguo zake anafua Dada wakazi, kwanini Dada wakazi anaingia mpaka chumbani na mambo kama hayo.
Usidhani anafurahia, usidhani hapati wivu pale rafiki zake wanapoongelea kuhusu wake zao kufua na kupika. Pale rafiki zake wanapowapigia simu wake zao kuwaambia wanataka kula nini. Namna unavyoumia shoga zako wakisema namna wanavyoletewa zawadi, namna wanavyohudumiwa ndivyo anavyoumia.
Ukiolewa hata kama wewe nia Raisi jua kuwa kazi za nyumbani ni zako. Sikwamba ufanye kila kitu bali ufanye angalau kitu kimoja, mfanyakazi wa ndani asiisngie chumbani kwako au kufua nguo za mumeo, mpikie mumeo hata mara moja kwa wiki chakula anachokipenda, hayo ndiyo majukumu ya mke wa mtu.
Usifanye hivyo kama adhabu au kwakuhisi kama ni kitu cha kukudhalilisha eti kwakuwa na wewe unaingiza pesa, eti una elimu kuliko yeye, kipato chako ni kikubwa kuliko chake na mambo kama hayo. Fanya hivyo kwakua wewe ni mke na unajisikia fahari kumfanyia hivyo.
Kama hujisikii fahari kumpikia mumeo, hujisikii fahari kumfulia na kutandika kitanda ili akione kisafi basi jipime, humpendi huyo mwanaume na uko kwenye ndoa kwasababu nyingine zaidi ya mapenzi. Mwanamke anayependa anajua huo ni wajibu wake na sio kwamba tu atautimiza bali pia atautimiza kwa mapenzi.