Sunday, October 29, 2017

HIZI NDIO TABIA TISA ZINAZOSABABISHA VIJANA WA SIKU HIZI KUZEEKA HARAKA

sasa hivi ukifanya utafiti mdogo tu hakuna mtu anayependa kuzeeka, iwe mwanaume au mwanamke lakini pia uzee ni kitu ambacho kinaleta sana msongo wa mawazo kwani ukiangalia picha zako kipindi una miaka 18 na sasa hivi una miaka 35 au 40 tayari umeshaona mabadiliko makubwa sana kwenye mwili yako lakini pia hofu ya kifo kwani unajua kinachofuata baada ya uzee ni kifo tu. japokua uzee haukwepeki leo hii kuna watu wana miaka 20 lakini wanaonekana wana miaka 30. hii ni dalili mbaya sana na huambatana na tabia zifuatazo mara nyingi.
kutofanya mazoezi kabisa; kiasili sisi binadamu ni wavivu, yaani watu wote wanaofanyakazi ni kwasababu wanajua wasipofanya kazi watalala njaa. lakini vizuri haviji bure hata utajiri unataka mateso kuupata. maana yangu ni kwamba mazoezi ndio yanafanya ngozi zetu na miili yetu iendelee kua kakamavu lakini pia huzuia uzito ambao ndio moja ya vyanzo vikuu vya unene.binadamu yeyote  anatakiwa afanye mazoezi angalau dakika 20 kwa siku. usisingizie kazi au kwamba uko bize sana.unashindwa hata kununua kamba uruke hata mara mia moja au mara hamsini kwa siku ukitoka kazini au kabla ya kwenda? kumbuka mtu ambaye hatakiwi kufanya mazoezi ni hule ambaye hali chakula.kutofanya mazoezi ni sawasawa na kujaza gari mafuta kisha unapaki afu asubuhi utegemee ukute yameisha.
kutopata usingizi wa kutosha; binadamu anatakiwa alale masaa saba mpaka nane kila siku haijalishi yuko bize kiasi gani, hata kama uko bize unatafuta pesa jua kwamba unautafutia mwili wako kwani ukiugua na kushindwa kufanya kazi hizo pesa hazina maana tena kwenye maisha yako.hapa duniani hatuishi milele kua mjanja na maisha yako.
uvutaji wa sigara; tafiti zinaonyesha uvutaji wa sigara unaongeza makunyazi ya ngozi hata kwa vijana wadogo na kuwafanya waanze kuonekana wana umri mkubwa kuliko miaka yao halisi. achana na sigara na tafuta wataalamu wakusaidie kuacha sigara kwani hicho ndio kifo chako.
kutokula mboga za majani na matunda; mfumo wa ulaji wetu ni mbovu sana. kawaida nusu ya sahani ya chakula inatakiwa iwe na mboga za majani na mtunda lakini ulaji wa wanga na vyakula vinavyoongeza sumu ndio chakula chetu kikuu hasa afrika.mfano kula chipsi,nyama nyingi,mayai,ugali mwingi,wali,biskuti,soda na vingine vingi bila kukumbuka umuhimu wa mboga mboga.ukienda hotelini mboga za majani na matunda unapewa kidogo sana lakini ugali mkubwa na nyama hii ni hatari sana.
kubeba visasi moyoni; ni vizuri kujifunza kuwasemehe watu ambao wamekukosea maishani hata hawajatuomba msamaha... inaweza kua wapenzi wa zamani, wazazi, ndugu, marafiki na jamaa kwa ujumla kwani hii huponya mtu kimwili na kiroho. yafiti zinaonyesha watu ambao wanabeba visasi na vinyongo hupata makunyazi ya ngozi na kuzeeka haraka.
msongo mkubwa wa mawazo; matatizo uliyonayo sasa hivi kama ni ya kifamilia, mahusiano, kufiwa, kukosa kazi na kadahalika yasikufanye uwe wa huzuni muda wote, tafuta jinsi ya kuyatatua matatizo hayo na kama huyawezi tafuta njia ya kuondoa stress zake hii itakufanya uwe na amani na uonekane kijana.
kunywa pombe sana; kitaalamu bia mbili kwa mwanaume na bia moja kwa mwanamke kwa siku. unywaji zaidi ya hapa humfanya mtu aharibu viungo muhimu vya mwili wake na kuanza kuonekana mzee akiwa mdogo.ushahidi wa wazi hata mtaani kwako, walevi wote wanaonekana wazee sana hata kama vijana.
kutaka kupunguza uzito ghafla; ni muhimu sana kupungua uzito, lakini pungua taratibu wakati ngozi na mwili wako vikipokea mabadiliko taratibu. pale unapolazimisha kilo thelathini kwa mwezi mmoja tena kwa chakula bila kufanya mazoezi basi utaanza kuzeeka mapema.
ulaji wa mkubwa wa chakula; kula sana kunasababisha unene, vijana wengi amabao wameanza kazi tayari utawakuta wana vitambi ndani ya muda mfupi sababu ya uroho usio kua na sababu au kutoka familia maskini lakini pia wakidhani wataonekana wana pesa. hebu fikiria..unafikiri wewe una pesa kuliko bill gait au mmiliki wa facebook? mbona wote hawana vitambi?.hebu kizoee chakula na ule kidogo kwani kadri umri unavyozidi kwenda mwili wako pia unahitaji chakula kidogo. ndio maana chakula kilekile ulichokuwa unakila ukiwa na miak 16 au 18 bila kuota kitambi leo ukikila kinakunenepesha.sasa hivi kuna virutubisho ambavyo vinapunguza hamu ya kula kabisa hii hufanya tumbo lipungue ukubwa na ku adopt ulaji wako mpya na kukusaidia kupungua kwani watu wengi hawawezi kabisa kula kidogo.nitafute kama unahitaji virutubisho hivi nitafute kwa namba hizo hapo chini. kwa maelezo zaidi bonyeza hapa kusoma